BBC Swahili na maswali kwa TCRA: JamiiForums Mbuzi wa Kafara?

BBC Swahili na maswali kwa TCRA: JamiiForums Mbuzi wa Kafara?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Ni takribani masaa 12 sasa tangu BBC Swahili kuchapisha habari inayomhusu mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Chivayo, ikiwemo picha yake akiwa Ikulu ya Tanzania. Tukio hili limeibua mjadala mzito huko mitandaoni: watu wanahoji je, TCRA itachukua hatua sawa na zile ilizochukua dhidi ya JamiiForums hivi karibuni, au huenda JamiiForums ndiyo ilitumika kama mbuzi wa kafara?

Screenshot_20250923_185215_Lite.jpg

Ikumbukwe, juzi juzi hapa mwaka huu TCRA iliiwekea vikwazo JamiiForums kwa kile kilichotajwa kama “makosa ya kimaadili na kushindwa kufuata taratibu za huduma za mawasiliano.” Hatua hiyo ilizua maswali mengi, kwani JamiiForums imekuwa ikichukuliwa kama jukwaa la kidemokrasia la mijadala na uhuru wa maoni nchini.

p019qtgr.jpg

Lakini sasa, BBC Swahili—chombo kikubwa cha kimataifa—imechapisha maudhui ambayo kwa vigezo vilevile, yanaweza kuchukuliwa kuwa yamekiuka taratibu. Swali kuu ni: TCRA ina ujasiri wa kutumia kipimo sawa kwa taasisi yenye nguvu ya kimataifa kama BBC, au kanuni hizo zinatumika kwa DOUBLESTANDARDS?

images (63).jpeg

Wadau wa habari na uhuru wa vyombo vya habari wanahoji iwapo uamuzi wa TCRA dhidi ya JamiiForums ulikuwa wa kulinda “heshima ya kitaifa” ama "heshima ya mtu" au ulikuwa ni pigo la makusudi kwa sauti za wananchi. Ikiwa BBC Swahili haitaguswa, hoja ya “mbuzi wa kafara” itapata mashiko zaidi.

IMG_7238.webp

Kwa upande mwingine, ukimya wa Mamlaka unaweza kutafsiriwa kama ishara ya upendeleo au hofu ya kugusana na taasisi kubwa za kimataifa.

Katika zama hizi za kidigitali, ambapo habari husambaa kwa kasi ya ajabu, mamlaka za udhibiti zinapimwa kwa usawa wa maamuzi yao.

Screenshot_20250923_185215_Lite.jpg

Je, TCRA itaonesha uthabiti wa kanuni zake kwa kuishughulikia BBC Swahili, au JamiiForums itaendelea kubaki mfano wa namna taasisi za ndani ambazo zinaweza kudhibitiwa kirahisi?

Wakati ndio utakaojibu.
 
Ni takribani masaa 12 sasa tangu BBC Swahili kuchapisha habari inayomhusu mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Chivayo, ikiwemo picha yake akiwa Ikulu ya Tanzania. Tukio hili limeibua mjadala mzito huko mitandaoni: watu wanahoji je, TCRA itachukua hatua sawa na zile ilizochukua dhidi ya JamiiForums hivi karibuni, au huenda JamiiForums ndiyo ilitumika kama mbuzi wa kafara?
View attachment 3477920
Ikumbukwe, juzi juzi hapa mwaka huu TCRA iliiwekea vikwazo JamiiForums kwa kile kilichotajwa kama “makosa ya kimaadili na kushindwa kufuata taratibu za huduma za mawasiliano.” Hatua hiyo ilizua maswali mengi, kwani JamiiForums imekuwa ikichukuliwa kama jukwaa la kidemokrasia la mijadala na uhuru wa maoni nchini.
View attachment 3477921
Lakini sasa, BBC Swahili—chombo kikubwa cha kimataifa—imechapisha maudhui ambayo kwa vigezo vilevile, yanaweza kuchukuliwa kuwa yamekiuka taratibu. Swali kuu ni: TCRA ina ujasiri wa kutumia kipimo sawa kwa taasisi yenye nguvu ya kimataifa kama BBC, au kanuni hizo zinatumika kwa DOUBLESTANDARDS?
View attachment 3477923
Wadau wa habari na uhuru wa vyombo vya habari wanahoji iwapo uamuzi wa TCRA dhidi ya JamiiForums ulikuwa wa kulinda “heshima ya kitaifa” ama "heshima ya mtu" au ulikuwa ni pigo la makusudi kwa sauti za wananchi. Ikiwa BBC Swahili haitaguswa, hoja ya “mbuzi wa kafara” itapata mashiko zaidi.
View attachment 3477924
Kwa upande mwingine, ukimya wa mamlaka unaweza kutafsiriwa kama ishara ya upendeleo au hofu ya kugusana na taasisi kubwa za kimataifa. Katika zama hizi za kidigitali, ambapo habari husambaa kwa kasi ya ajabu, mamlaka za udhibiti zinapimwa kwa usawa wa maamuzi yao.
View attachment 3477920
Je, TCRA itaonesha uthabiti wa kanuni zake kwa kuishughulikia BBC Swahili, au JamiiForums itaendelea kubaki mfano wa namna taasisi za ndani ambazo zinaweza kudhibitiwa kirahisi? Wakati ndio utakaojibu.
Papas Msofe wa Zimbabwe Wicknell Chivayo ameanzia mishemishe pale Zimex Mall alipokuwa bado anaupigaji mdogomdogo baadaye fumu likafuma fuba akaingia michongo mkubwa, amejipatia umaarufu baada ya kuwa baba wakambo wa UVCCM na chawa wote kwa ujumla. Anaitafuna TZ kilaini kwa sasa huyo muhuni wa mipango, mwamba huyo ambaye ni baba wa Abdul wa kufikia amempatia mwanae container la arsenals hivi sasa wasiojulikana hakuna anayeweza kuwamudu.
 
Duuh
 
Hilo halita kuja kutokea. BBC ni chombo kikubwa duniani.

Jamii Forums ni kajukwaa ka hapa Tz.
Hapo ndipo utaona kua Hakuna haki ya usawa hapa tz
Jaribu kuwa na staha kidogo unapoiongelea Jamii Forums na kutumia maneno ya kuibeza. Tatizo ni zaidi ya ‘ukubwa’ au ‘udogo’ wa Taasisi husika, na tukijaribu kuliangalia kwa mlengo huo tutawa tunafeli zaidi. Haihusiani na kuogopwa kwa chombo kimoja cha habari kwa kuwa ni cha ‘kimataifa’ lakini zaidi tuliangalie zaidi katika hali halisi ya namna habari zinavyopatikana na kuchakatwa katika platform husika.

Jamii Forums ni mimi na wewe ndio tuna umiliki wa habari na taarifa zilizopo katika jukwaa hili. Ni sisi wenyewe tunajadili na kuchambua yote yaliyomo humu. Ni sisi ndio tunaojadili na matokeo ya mijadala yetu yanaakisi hisia za Watanzania katika masuala yanayowahusu moja kwa moja.
 
Kwani hizi picha zilikuwa ni za siri, au za kutengeneza? Na kama zilipigwa na wao wenyewe! (Tena mpaka huyo Chivayo nasikia aliziweka kwenye akaunti yake ya Instagram!) Je, ni jamii forums ndiyo walizichukua na kuzisambaza/kutuonesha sisi raia mnao tuchukulia kama ng'ombe tusio na utashi?

Na kuhusu ishu ya Polepole! Je, alitumia jamii forums kwa ajili ya zile hotuba zake, au alitumia online platforms ambazo kila mtu alikuwa na uwezo wa kuzipata? Na kwa nini jamii forums ifungiwe, na wakati huo huo Rostam Aziz alihojiwa na Tido Mhando baadaye kupitia UTV ya Azam Media na kutolea ufafanuzi juu ya shutuma alizotuhumiwa!

Sasa nyinyi TCRA ambao mpo mpaka humu jukwaani, mmeufungia huu mtandao kwa makosa gani yenye mashiko? Je, mliwapa nafasi uongozi kujitetea?

Hivi ni kwa nini watawala na watu wenye mamlaka mnajiona mko kuu ya kila kitu kwenye hii nchi, ambayo ni ya kwetu sote?
 
Kwani hizi picha zilikuwa ni za siri, au za kutengeneza? Na kama zilipigwa na wao wenyewe! Tena mpaka huyo Chavayo aliziweka kwenye akaunti yake ya Instagram! Je, ni jamii forums ndiyo walizichukua na kuzisambaza/kutuonesha sisi raia mnao tuchukulia kama ng'ombe tusio na utashi?

Na kuhusu ishu ya Polepole! Je, alitumia jamii forums kwa ajili ya zile hotuba zake, au alitumia online platforms ambazo kila mtu alikuwa na uwezo wa kuzipata? Na kwa nini jamii forums ifungiwe, na wakati huo huo Rostam Aziz alihojiwa na Tido Mhando baadaye kupitia UTV ya Azam Media na kutolea ufafanuzi juu ya shutuma alizotuhumiwa!

Sasa nyinyi TCRA ambao mpo mpaka humu jukwaani, mmeufungia huu mtandao kwa makosa gani yenye mashiko? Je, mliwapa nafasi uongozi kujitetea?

Hivi ni kwa nini watawala ma watu wenye mamlaka mnajiona mko kuu ya kila kitu kwenye hii nchi, ambayo ni ya kwenu peke yenu?
Mkuu hayo maswali yako yanahitaji akili kubwa sana 😢 nilitegemea TCRA wakiwafungia na BBC Swahili wasitoe habari ndani ya Tanzania kwa makosa yale yale waliyoyasema kwa Jamii Forums
 
Ngoja wajaribu kuiwekea vikwazo BBC Swahili waharibu zaidi, muingereza hatavumilia upuuzi huo
 
Back
Top Bottom