BBC Swahili imedanganya kuhusu nchi wahisani kurejesha misaada BAADA ya hotuba ya Jakaya Kikwete?

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
Awali,kupitia akaunti yake ya Twitter, Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) iliripoti ifuatavyo=> [h=1]Wahisani wafurahishwa na hotuba ya Kikwete[/h]

Hata hivyo, baada ya kuzongwa na baadhi ya WANAHARAKATI huko Twitter walioonyesha kukerwa na hatua hiyo ya nchi wahisani, Mwenyekiti wa nchi wahisani, Balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila (@SinikkaAntila) alifafanua kwa tweet ifuatayo

_20141224_022923.JPG

Kwa lugha ya taifa, Balozi huyo anaeleza kwamba "vyombo vya habari havipo sahihi. Asilimia 15 ya msaada ulioahidiwa kwa bajeti ya mwaka 2014/15 ilitolewa kabla ya hotuba ya Rais (Kikwete)."

Hata hivyo, licha ya kauli hiyo ya Balozi Antila kutanabaisha kuwa BBC Swahili waliripoti ndivyo sivyo kuwa wafadhili wameamua kutofa fedha hizo baada ya kuridhishwa na hotuba ya Rais Kikwete, bado kuna swali gumu kuhusu suala hilo, nalo ni JE NCHI WAFADHILI ZILITUHADAA ZILIPODAI KUWA ZIMESITISHA MISAADA HADI HATUA ZITAKAPOCHUKULIWA KUHUSU SUALA LA ESCROW?

Swali hilo linatokana na kauli ya Balozi huyo wa Finland kuwa fedha hizo zilishatolewa hata kabla ya hotuba ya Rais Kikwete, ikimaanisha aidha nchi hizo wahisani zilikuwa zina hakika kuwa Rais Kikwete angechukua 'hatua hizo za kuwaridhisha wafadhili' au 'walituzuga tu' kuhusu kusitishwa misaada hiyo.

Kadhalika, kauli ya Balozi Antila haikanushi kuridhishwa kwa wafadhili na hotuba ya Rais Kikwete, ambayo Watanzania wengi wanaamini kuwa imewalinda mafisadi hasa ikizingatiwa mzigo mkubwa wanaoubeba kutokana na sakata la muda mrefu la IPTL. Kwa Rais Kikwete kushindwa kumaliza sakata hilo, na kuridhia kuwa pesa za Tegeta Escrow ni za IPTL/ PAP, ina maana Watanzania wataendelea kulipa mamilioni ya shilingi kila siku kwa huduma ya umeme ambayo kimsingi ni hewa.

Binafsi ninaguswa na uamuzi wa nchi wahisani kwa sababu kama mkazi wa Uingereza, ninalipa kodi mbalimbali, ambazo sehemu ya kodi hiyo ipo katika misaada inayotolewa na nchi hii kwa Tanzania. Wakati sina kipingamizi kwa nchi hizo kuisaidia Tanzania, siungi mkono kabisa kuendelea kutoa fedha zinazoishia kuwaneemesha mafisadi kwa kunenepesha akaunti zao, kuongeza idadi za mahekalu na magari yao ya thamani na kukuza idadi ya nyumba zao ndogo.

Ufadhili usiozingatia maslahi ya nchi fadhiliwa sio tu ni upuuzi bali pia ni ku-abuse fedha za walipakodi katika nchi wafadhili.

Habari zaidi, soma=>Wahisani bado wanaikaba Tanzania
 
$84billion!!!!!!!!!!!!!!!!...I cant buy that.... our 2014/2015 budget is only TZS 19.6 trillion(Appr. $ 11.4billion)
a matter of fact it is only 15% of the commited budget already given out..
 
Bbc sio Tanzania Daima au Itv. Mbona hakukanusha kuridhishwa na hotuba ya Rais? Pesa za escrow si za umma,na kama zilikuwa umma kwa nini tanesco hawakuweka Nbc,Crdb au benki nyingine yoyote? Ni kwa vipi bunge likubaliane na idadi ya pesa kuwa ni bil 306 kumbe zilikuwa ni Bil 201, uongo huu ulikuwa kwa faida ya nani? Ingawaje sasa wanageuza maneno kuwa nyingine zililipwa na Tanesco nje ya akaunti ya escrow,kwa nini ufafanuzi huu wautoe nje ya bunge kwa kutumia mitandao ya kijamii? Ukweli wa sakata la escrow kuhusu pesa umeisha fahamika na bado Tanesco inadaiwa, kwa nini mnahoji tozo la Iptl tuu wakati kuna makampuni mengine pia yanatoza? Kwanini mnahoji pesa zilizotolewa Mkombozi na kuwataja waliochukua huku waliopewa Stanbic mnaminya? Acheni kuweka siasa majitaka kila sehemu na wenye vyombo vya habari wenye chuki na baadhi ya viongozi waache kutumia vyombo vya habari kuwachafua wengine

tafadhali wahusika wa jamii forum usibadilishe kitu hapa au kuiondoa,kuna katabia mmekaanzisha hapa kwa kuondoa uzi moto au kuumoove
 
$84billion!!!!!!!!!!!!!!!!...I cant buy that.... our 2014/2015 budget is only TZS 19.6 trillion(Appr. $ 11.4billion)
a matter of fact it is only 15% of the commited budget already given out..
Na hiyo ni budget maandishi tu,but kiuhalisia labda ni trillion 11 tu
 
Nadhani inabidi tusisaidiwe ili watakaonusurika na hali hii watatia akili ya kuishi bila kusaidiwa, vinginevyo tutaendelea kudumaa kiakili na kuamini kuwa hatuwezi kuishi bila misaada. Hii inawadumaza vizazi vyetu vilevile.
 
Viongozi wako hyo hoja yako wataishangaa,wao source ya pesa ni kutembeza bakuli wamezidiwa akili hata na wakinga ambao wengi wao hawakusoma but ni creativ ajabu
 
mmezoeshwa kupewa misaada mpaka inafika mahala mnaona kama kupewa misaada ni haki yenu wapumbavu wakubwa nyie,alafu nashangaa Leo mnaona sawa tupewe misaada ila inapotokea raisi akasena anaenda kuhemea nyote humu mnajifanya kumponda,acheni UNAFIKI
 
Bbc sio Tanzania Daima au Itv. Mbona hakukanusha kuridhishwa na hotuba ya Rais? Pesa za escrow si za umma,na kama zilikuwa umma kwa nini tanesco hawakuweka Nbc,Crdb au benki nyingine yoyote? Ni kwa vipi bunge likubaliane na idadi ya pesa kuwa ni bil 306 kumbe zilikuwa ni Bil 201, uongo huu ulikuwa kwa faida ya nani? Ingawaje sasa wanageuza maneno kuwa nyingine zililipwa na Tanesco nje ya akaunti ya escrow,kwa nini ufafanuzi huu wautoe nje ya bunge kwa kutumia mitandao ya kijamii? Ukweli wa sakata la escrow kuhusu pesa umeisha fahamika na bado Tanesco inadaiwa, kwa nini mnahoji tozo la Iptl tuu wakati kuna makampuni mengine pia yanatoza? Kwanini mnahoji pesa zilizotolewa Mkombozi na kuwataja waliochukua huku waliopewa Stanbic mnaminya? Acheni kuweka siasa majitaka kila sehemu na wenye vyombo vya habari wenye chuki na baadhi ya viongozi waache kutumia vyombo vya habari kuwachafua wengine

tafadhali wahusika wa jamii forum usibadilishe kitu hapa au kuiondoa,kuna katabia mmekaanzisha hapa kwa kuondoa uzi moto au kuumoove
unatumia nini kufikiri?au upo kwenye mgao????
 
Mwenyekiti wa nchi wahisani, Balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila ameushukia mtandao wa kiswahili wa Shirika la Utangazaji la BBC kuwa umepotosha taarifa waliyokuwa wameitoa hapo jana akibainisha kuwa asilimia 15 (dola mil 84) ya msaada ulioahidiwa kwenye bajeti ya Tanzania mwaka 2014/15 ilitolewa kabla ya hotuba ya Rais Jakaya Kikwete.
Mapema hapo jana shirika hilo liliripoti kuwa baada ya nchi wahisani kufurahishwa na hotuba aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete hapo juzi alipokuwa akizungumza na wazee wa mkoa wa Dar es salaam, wameamua kutoa asilimia 15 ya msaada wa dola mil 500 ambazo wahisani hao walitarajiwa kuzitoa kwa Tanzania.
Taarifa hiyo ya BBC iliibua mjadala mpana kwa wadau mbalimbali kwenye mitandano ya kijamii hasa twitter hata kupelekea kumtafuta Balozi Sinikka Antila ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo.
Hata hivyo Shirika hilo lililazimika kufanya marekebisho kufuatia taarifa hiyo na kuwaomba radhi wasomaji wake kwa kutoa taarifa ambayo haikuwa sashihi kupitia makala yao ya Sahihisho : Wahisani bado wanaikaba Tanzania
Nchi hizo zilisitisha kutoa msaada huo kumshinikiza Rais ashughulikie suala la ufisadi pamoja na rushwa hasa baada ya kuibuka kwa sakata la uchotwaji wa zaidi ya bil 306 kwenye akaunti ya Tegeta ESCROW iliyokuwa Benki kuu ya Tanzania.
 
Siku ya arobaini imewafikia.
15% ilishagawiwa kabla ya speech ya jk.
Na wanasema media got it wrong, looks like nao hawajaridhishwa na hotuba.
 
BBC wamwajibishe mwakilishi wao wa Tanzania maana haya ni matokeo ya ule mwaliko wa Ikulu asbh ya siku ambayo jioni JK alikuwa anahutubia.
 
Back
Top Bottom