BBC - Kunani vyuo vikuu vya Afrika Mashariki?

BBC - Kunani vyuo vikuu vya Afrika Mashariki?

njiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2009
Posts
13,259
Reaction score
7,109
Vyuo vikuu vya Afrika Kusini ndio bora zaidi na maarufu barani Afrika

Orodha kamili

1- Chuo kikuu cha Cape Town - Afrika Kusini
2- Chuo kikuu cha Witwatersrand - Afrika Kusini
3- Chuo kikuu cha Makerere - Uganda
4- Chuo kikuu cha Stellenbosch - Afrika Kusini
5- Chuo kikuu cha KwaZulu-Natal - Afrika Kusini
6- Chuo kikuu cha Port Harcourt - Nigeria
7- Chuo kikuu cha Western Cape - Afrika Kusini
8- Chuo kikuu cha Nairobi - Kenya
9- Chuo kikuu cha Johannesburg - Afrika Kusini
10- Chuo kikuu cha Cadi Ayyad - Morocco

Source - BBC SWAHILI
 
Tatizo ni siasa mpendwa,kila kitu siasa hadi kwenye elimu?.
Toka kuzaliwa hadi uzee nilo nao sijawahi kusikia nchi yoyote duniani inaingiiza mambo ya siasa kwenye elimu.
Nakumbuka zama za waziri MAKWETA,hakukuwa na uhuni wa jinsi hii labda wenye nchi wameamua kuivuruga kupitia siasa ili kutengeneza mazingira kwa watoto wao kuja kuendelea kutawala nchi iliyo jaa mitoto ya mikulima kama nchi ya kifalme.
UKITAKA KUMTAWALA MTU KWA JINSI UNAVYOTAKA,MNYIME ELIMU.
 
Tena kigezo kilichotumika (publishing quality scholarly works - citation) kinafaa sana kupima ubora wa PhD holders and Professors wa Bongo.
 
hahaha 30 hakuna chuo cha tanzani ni aibu maprof wa bongo wapimwe wote wamekimbilia kwenye siasa
 
Huwezi kuamini kuna watu wamesoma vyuo vikuu Tanzania na wanashabikia Ukawa. Sasa kwa nini vyuo vyetu visiwe hovyo

kama maendeleo hayapatikan ccm basi yatafutwe nje ya ccm haya tunayoyaongea hapa ni matokeo yenu ccm mmeleta siasa had kwnye elimu hata 100 bora hatupo labda 100 chafu
 
tatizo sio ukubwa au ubora wa majengo kama udom au udsm tatizo quality ya elimu na uwekezaj wa serikali katika elimu yaan hali za wanafunzi na wakufunzi vyuoni
 
Tatizo ni kwamba siasa Tanzania ina tawala kila sector maskin udsm
 
prof rwekaza mkandala mzee wetu please irudishe udsm kundini achana na hao akina kitila mkumbwa kutwa kwenye siasa hata mustakabali wa chuo hawajui
 
Watu wanadhani unaweza kupata elimu bora kwa kwenda chuo bora bila kujenga msingi kuanzia shule ya msingi na sekondari. Lazima tutakua wageni kwenye nchi yetu siku za mbeleni
 
prof rwekaza mkandala mzee wetu please irudishe udsm kundini achana na hao akina kitila mkumbwa kutwa kwenye siasa hata mustakabali wa chuo hawajui

Sasa atairudishaje bila kurudishwa kwanza msingi huku nyuma? mtu anaingia chuo na passmark nzuri ila uwezo wa kuchambua na kuhoji mambo hana, na tuapima mtu aliesoma na kuelemika kwa jinsi anavyotumia elimu yake kuishi na jamii kwa kutoa michango chanya na pia kujikomboa mwenyewe.

Mfano utamkuta mhitimu wa chuo kikuu hana shida ya kuangalia taarifa ya habari, hana habari na mambo ya kujiandikisha kwenye daftari ya kupiga kura, je atamwambia nini mtu ambae hana kiwango cha elimu ya chuo aliejiandikisha na kila mara taarifa ya habari anasikiliza? mchango wake kwa jamii kuusu elimu ya uraia ikoje?

Lazima tuanze kujifunza uraia tena tokea shule za msingi kama zamani, tuache kulaumu vyuo vikuu ambapo mtu anakaa miaka miwili tu.
 
Tatizo ni kwamba siasa Tanzania ina tawala kila sector maskin udsm

Nakereka sana kwa nchi yenye watu 45's kutegemea chuo kimoja tu..hata nchi kama japan unaweza kuwakosa kwenye top ten ila kiwastani wako juu kuliko nchi ilitoa top ten kidunia.
 
Vyuo vikuu vya Afrika Kusini ndio bora zaidi na maarufu barani Afrika

Orodha kamili

1- Chuo kikuu cha Cape Town - Afrika Kusini
2- Chuo kikuu cha Witwatersrand - Afrika Kusini
3- Chuo kikuu cha Makerere - Uganda
4- Chuo kikuu cha Stellenbosch - Afrika Kusini
5- Chuo kikuu cha KwaZulu-Natal - Afrika Kusini
6- Chuo kikuu cha Port Harcourt - Nigeria
7- Chuo kikuu cha Western Cape - Afrika Kusini
8- Chuo kikuu cha Nairobi - Kenya
9- Chuo kikuu cha Johannesburg - Afrika Kusini
10- Chuo kikuu cha Cadi Ayyad - Morocco

Source - BBC SWAHILI

Wa S.A Historia inawabeba hao mzee.. Kumbuka hadi now bado wazungu wanawabeba kule walijenga vyuo na viwanda kibao walipoweka makazi yao miaka hiyo.. Ila naona Udsm hawajaitendea haki hapo..
 
Tanzania Tanzania Nchi yangu Tanzania nakupenda kwa moyo wote......! Ninapo kwenda safarin kutazama maajabu BIASHARA....
 
Tatizo ni siasa mpendwa,kila kitu siasa hadi kwenye elimu?.
Toka kuzaliwa hadi uzee nilo nao sijawahi kusikia nchi yoyote duniani inaingiiza mambo ya siasa kwenye elimu.
Nakumbuka zama za waziri MAKWETA,hakukuwa na uhuni wa jinsi hii labda wenye nchi wameamua kuivuruga kupitia siasa ili kutengeneza mazingira kwa watoto wao kuja kuendelea kutawala nchi iliyo jaa mitoto ya mikulima kama nchi ya kifalme.
UKITAKA KUMTAWALA MTU KWA JINSI UNAVYOTAKA,MNYIME ELIMU.

umenongea pointi ya maana sana mkuu.
tatizo sisi usanii sanii hadi kwenye mambo
nyeti na muhimu kama Elimu (sasa kwa product za
shule ya kata / kayumba
kweli utaweza toa chuo bora Afrika kweli)
wakuu tuacheni masihara kwenye suala la Elimu.
 
Nilisikiloza uchambuzi wao, wakasema kigezo kikubwa kilichotumika pamoja na mambo mengine ni Ukongwe wa chuo!

Lakini siku hizi BBC nao wamekuwa kama Uhuru Fm! habari nyingi ni za wakenya na kenya tu hata watangazaji wao wanajisahau na kuonesha ukenya wao. Jana katika mjadala huo mtangazaji akasema"chuo chetu cha Nairobi...bla bla bla"

Wamekuwa shalow hakuna habari za uchunguzi wala sio tena wakwanza kutoa habari mpasuko!

Nadhani walifanya kosa kuhamishia utangazaji Nairobi!
 
Back
Top Bottom