Naomba kuweka wazi kuwa mimi ni mwana taaluma wa Manunuzi (procurement expert). Sikubaliani na 24hrs hata kidogo. Na naomba uache kupotisha watu. 10% ni maneno ambayo yanaongelewa bila kufikiri na mwisho huleta shida kwenye taaluma. Shida hizo ni kama ifuatavyo: kwanza wanajitokeza wanataaluma bandia ambao lengo ni kutafuta 10%. Ukimuuliza kitu gani kimekufanya usome procurement kama ni mkweli, jibu atakalo kupa ni kama maneno yako 24hrs. Ukimuuliza maswali ya kitaaluma ndo utagundua alisoma ili afaulu tu. Kazini nimekutana na watu wana masters, ila mwambie aandae nyaraka za zabuni itachua mwezi na bado hajui kitu. Hiyo ni uvamizi wa taaluma na watu wanaoshawishika na maneno kama yako. Pili kuna watu wa taaluma nyingine maofisini ambao hutaka kulazimisha imani hizo na kuamini kupata hela kupitia manunuzi hivyo kuishia kuwashawishi wahusika wa procurement kuongeza bei au wakikataa kuwalaumu wanakula peke yao. Ifike muda sasa wewe na wengine mtambue kuwa nchi hii inaendeshwa kwa sheria, kanuni, taratibu na kiongozi. Wapi panaruhusu 10%? Procurement ni taaluma kama nyingine hivyo taaluma hiyo ina miiko yake yaani code of ethics. OMG natamani kuongea na kufafanua umma uelewe na wewe ukiwemo pia