- Bachelor of Accounting - 81
- Bachelor of Banking and Finance - 103
- Bachelor of Science in Insurance and Risk Management - 553
Ni kweli taifa linahitaji vijana wenye taaluma za Insurance na tunaipongeza IFM kuwa na hii kozi lakini ukweli mchungu ni kwamba uhitaji wake ni mdogo mno sokoni.
Kwa uhalisia, nafasi za ajira za Insurance ni nadra sana na zikitokea, ni za kampuni chache za bima pekee. Ukiingia ajira portal ya serikali, hakuna kipengele cha insurance, na mara nyingi ajira zinazotangazwa hazihitaji taaluma hiyo kabisa.
Hata ukiangalia vyuo vinavyotoa kozi hii viwili tu nchi nzima, IAA na IFM (Udsm iliwahi kuwepo wakaifuta), kwa IAA ni moja ya kozi yenye wanafunzi wachache sana, IFM main campus ya Dar ipo lakini bado haimo top 4 kwenye kozi zenye wanafunzi wengi, Dodoma campus hii kozi haipo kabisa.
MAPENDEKEZO
- degree za insurance zinahitajika lakini zipunguzwe ziwe hata 100 wanatosha,
- wanafunzi wa accounting waongezwe wafike hata 300
- ziongezwe degree za ziada kama Procurement, HR na IT, demand ipo both serikalini na Private sector