BBA, Accountancy vs procurement

Sitta juma

Member
Oct 4, 2016
44
24
Habar za asbh,
nauliza kati ya kozi 3 hapo juu, ni ipi ambayo ipo more marketable zaid kwa ngazi ya bachelor?
 
naona BBA kwasababu kama lengo lako ni kupata ajira unakuwa na wigo mpana kuliko hizo zingine ingawa sizidharau. Accountancy itakubidi uwe na CPA pia ambayo inasemekana ina ugumu katika kuipata. Procurement pia itakubidi uwe certified PSPTB ila nahisi kwao sio kugumu kama NBAA.
 
Nahic mtu wa BBA anaweza Fanya kazi zote zizikiwemo za acc,procurement na HR,cjui km Niko sahh
BBA ni mama wa kozi zote za biashara kuhusu ajira kila sehemu inamuitaji mtu specific so mhasibu atafanya yake na mgavi naye hivo hivo usisahau na watu w masoko n mauzo pia nihivo
 
BBA ina majors (specializations) zake, huwezi soma just BBA in general. Ndani ya BBA unaweza major kwenye Accountancy na ukawa a pure accountant, au Banking and Finance, pia unaweza major kwenye Procurement and Logistics/Materials Management, au ukaamua kwenda Markerting na pia Human Resources Management. Mara nyingi inategemea na chuo unachosoma. Vyuo vyenye degree za Accountancy kama Mzumbe University's Bachelor of Accounting and Finance, BBA yao haina major ya Accountancy. Ila vyuo kama SAUT nafikiri na St. John, kuna specialisation ya Accountancy kwenye BBA sababu hawana degree tofauti ya accountancy.

Kama utajua chuo unachopendelea kwenda, then hapo unaaweza kuamua. Ila kila moja ya hizo specialisation ina greener pastures somewhere out there, ingawa to be honest, specialisation ya Human Resources Management openings sio nyingi saana.
 
Mie nitakushauri upige BBA.
Tena BBA general, ambayo ina cover almost field zote muhimu za biashara kuanzia Accounting, Finance, Economics, Human Resource management, Risk and Insurance, International business na marketing.

Ukisoma hii course vizuri tena ukatulia, ukisha graduate wala huta taka kuajiriwa.

Kuna vyuo vichache sana vinavyotoa BBA general hapa Tz. kutokana na ubora wa chuo, ningekushauri u apply UDBS (UDSM).
 
BBA inabeba zote hizo mbili accountancy na procurement unasoma vitu vingi ila mwaka wa mwisho utabeba kitu kimoja either market, accountancy or procurement , ila to me nakushauri to specialise its what makes you an expert nilimaanisha bora uchukue procurement kama procurement kutokana na fursa eg job market, knowledge wise pia inaweza kukupa fursa ya kufungua ofisi yako yani ukajiajiri ukawa tendering consultant etc
 
Nenda NIT Chukua bachelor degree in logistics and Transport management

Au chukua Accounts and Transport Finance pale NIT ni course Unique sana kibongo bongo
 
Back
Top Bottom