Bazoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bazoka

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Che Kalizozele, Dec 29, 2008.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Waheshimiwa naomba kupatiwa jina halisi la kiswahili la bazoka au big G.Maana haya yote ni majina yaliyotolewa na makampuni yanayotengeneza bidhaa hii.
   
 2. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 60
  Ubani wa kutafuna.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa nini hili jina la ubani sio maarufu huko bara?
   
 4. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 60
  lipo na linatumika hasa mkoa wa Arusha nitokako mimi, pia nimewahi kusikia sehemu za singida baadhi wa watu wakiita ubani, sijui maeneo mengine.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa Arusha naona jina bazoka ndio maarufu zaidi, aidha wengi utumia Big G kwa aina zote za chew gum mkoani hapo... Kama linatumika basi ni kwa sehemu chache sana mjini humo..

  Ama kwa Singida sijapata kabisa kusikia matumizi ya ubani wa kutafuna, labda katika miaka hii, kwani nilipita huko kitambo kidogo.
   
 6. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 60
  Ubani wa kutafuna
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Nadhani maneno 'Bazoka' , 'Bigijii' na 'Chingamu' (chewing gum!) yamepata mashiko zaidi baina ya wazungumzaji wa kiswahili wa sasa kuliko neno 'ubani wa kutafuna'.

  Ni kweli ni maneno ya kukopa/kutohoa - tena ni mali za makampuni (trade marks/names) - lakini, lugha ndivyo ilivyo. Wanajamii wakikubalina neno basi linakuwa sehemeu ya lugha yao.Hakuna ubaya katika hilo! Kuna maneno mengine mengi tu ya jinsi hii ambayo nayo yamepata mashiko japokuwa ni trademarks/names: bukta (Bukta),themosi (Thermos), katapila (Caterpillar), sheli (Shell) nk
   
Loading...