BAWACHA wanunua kesi ya mwanamke kujifungua Polisi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
DSC_0127-620x308.jpg

UONGOZI wa Baraza la wanawake CHADEMA (BAWACHA)limelaani vikali kitedendo cha udhalilishaji kilichofanywa na jeshi la polisi dhidi ya Amina Mapunda (26) mkazi wa Kiswanya kijiji cha Mgundeni, tarafa ya Mang’ula wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Uongozi huo ulisema kuwa kitendo cha mwanamke huyo kujifungulia nje ya kituo cha polisi bila msaada wowote ni kitendo cha kinyama na kinatoa picha ni kwa jinsi gani jeshi la polisi linafanya kazi yake bila ueledi wa kutosha.

Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa BAWACHA, Grace Tendega na mbunge wa Viti maalumu amesema viongozi huo unalaani kitendo hicho na viongozi ndani ya jeshi la polisi wanatakiwa kujipima na kujitafakari kama kweli wanatosha au wajiuzulu.

Amesema kitendo cha jeshi hilo kumsababishia mwanamke huyo kujifungulia chini tena kwenye mchanga hakimdhalilishi yeye peke yake bali kinawadhalilisha akina mama wengi wa kitanzania na niukiukwaji wa haki za binadamu.

“Hapa unaweza kujiuliza mama anahusikaje na wizi wa mume wake,haya kama kweli waliona kuna vifaa vya wizi kwanini hawakuchukua vifaa hivyo kama ushahidi.

“Lakini inashangaza hao polisi hawakuona kama huyo mama ni mjamzito au hawajui mtu ambaye ni mjamzito,haya ni mambo ya ajabu sana kwa jeshi la polisi,” amesema Tendega.

Katika hatua nyingine Tendega amesema kama kweli jeshi la polisi lingekuwa na ueledi wa kazi yao ni kwanini wasingeweka matangazo kila kona kwa ajili ya kumsaka mharifu hadi wampate.

Katibu huyo mkuu wa BAWACHA amesema kitendo hicho ni kibaya na kuna kila sababu ya viongozi wa Jeshi la Polisi kuanzia ngazi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Kilombero, mkuu wa polisi Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania (IGP) pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi na Naibu wake wakajitafakari na kujipima kama kweli wanastahili kuendelea na kazi.

Amesema matukio ya aina hiyo yamekuwa yanajirudia mara kwa mara na jeshi la polisi limekuwa likikaa bila kuonesha juhudi yoyote ya kuwachukulia hatua wanaohusika na uharifu wa kuwatesa wananchi au kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

Tendega amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa vitisho mbalimbali lakini chama hicho na Baraza la Wanawake wa CHADEMA hawatanyamaza na badala yake kitapaza sauti kwa ajili ya kuwatetea wanyonge na kudai haki bila kuwa na woga.

Habari zaidi, soma=>Chenge asema kitendo cha mwanamke kujifungulia Polisi ni cha hovyo na kinyama
 
Hao Polisi kesi ni yao, halafu wao wenyewe wanajichunguza, wakati huo huo wanakuwa ndiyo waendeshaji wa kesi (prosecutors) na hapo hapo ndiyo wanakuwa majaji wa kuamua kesi
 
udhalilishaji wa haki za binadamu uongozi polisi kilombero wawajibishwe kwa tukio hili la makusudi..
 
Kile kitendo kimelaaniwa na watu wa kada zote bila ya kujari tofauti zao,sasa unaposema wamenunua kesi nashindwa kukuelewa halfu kwenye maelezo yako amna kitu kama hicho au ulitaka watu wafurahie ule udhalilishwaji wa yule mwanamke.
 
Kujifungua mtu aweza jifungulia bafuni akioga,daladala,ofisini,msibani,kwenye mwendo Kasi,kwenye boda boda,stendi,mkutano wa chadema etc inategemea uchumi umemkuta wapi that is not a big case you.Mwenyekiti wa bawacha halima Mdee anajijua mwenyewe Hana mume Wala mtoto Na hajui utungu wa kuzaa ni kitu gani? namshauri kama mbunge wa kawe kuna hospitalii kubwa jimboni kwake ya Dr Massawe asijifanye haijui anaijua sana tu Na imesheheni madaktari bingwa akawahoji utungu unakuwaje kwa mjazito mwehu mkubwa asiyejua hata utungu ni kitu Gani? Aulize hospital hiyo tu Na Nina maana yangu yeye nadhani kanielewa vizuri tena mno mjinga mkubwa.Bull shit.Halima Mdee behave yourself
 
Inashangaza kuna mijitu inafurahia kitendo hiki na wanaona ni sawa. Ni lini mtaacha kutetea matumbo yenu?
 
Polisi ya tanzania ni chaka la ma psychopaths, kuna wakati huwa wana enjoy kabisa kuona mtu akiteseka. Kuna umuhimu wa kuunda chombo kingine chenye mamlaka na uwezo wa kuchunguza na kuwafungulia mashtaka polisi, uhamiaji, magereza na takukuru.
 
Askari badala ya kupongezwa kwa kumsaidia kujifungua fasta ati wanashtakiwa.
 
Kujifungua mtu aweza jifungulia bafuni akioga,daladala,ofisini,msibani,kwenye mwendo Kasi,kwenye boda boda,stendi,mkutano wa chadema etc inategemea uchumi umemkuta wapi that is not a big case you.Mwenyekiti wa bawacha halima Mdee anajijua mwenyewe Hana mume Wala mtoto Na hajui utungu wa kuzaa ni kitu gani? namshauri kama mbunge wa kawe kuna hospitalii kubwa jimboni kwake ya Dr Massawe asijifanye haijui anaijua sana tu Na imesheheni madaktari bingwa akawahoji utungu unakuwaje kwa mjazito mwehu mkubwa asiyejua hata utungu ni kitu Gani? Aulize hospital hiyo tu Na Nina maana yangu yeye nadhani kanielewa vizuri tena mno mjinga mkubwa.Bull shit.Halima Mdee behave yourself
jifunze utu acha kashifa
 
jifunze utu acha kashifa
Ukiheshimu utu wa mwingine utaheshimiwa ukiudharau utadharauliwa vizuri utungu waweza mkuta mtu popote iwe rumande,polisi,jela,kituo cha daladala,sokoni au popote hili la Bawacha sidhani kama hawaheshimu utu wa huyo Mama kuwa aweza pata utungu popote niwaheshimu bawacha Na Mdee Kwa lipi? Mdee atamwanikaje mwanamke mwenzie hivyo kama vile hajui utungu kuwa waweza kutokea popote? narudia Halima Mdee Mwenyekiti Bawacha kaulize maswala ya utungu Hospital ya Dr Massawe.Unapajua sana tena sana sana sana sanaaaaaaaa!!!!!!!!!
 
Kujifungua mtu aweza jifungulia bafuni akioga,daladala,ofisini,msibani,kwenye mwendo Kasi,kwenye boda boda,stendi,mkutano wa chadema etc inategemea uchumi umemkuta wapi that is not a big case you.Mwenyekiti wa bawacha halima Mdee anajijua mwenyewe Hana mume Wala mtoto Na hajui utungu wa kuzaa ni kitu gani? namshauri kama mbunge wa kawe kuna hospitalii kubwa jimboni kwake ya Dr Massawe asijifanye haijui anaijua sana tu Na imesheheni madaktari bingwa akawahoji utungu unakuwaje kwa mjazito mwehu mkubwa asiyejua hata utungu ni kitu Gani? Aulize hospital hiyo tu Na Nina maana yangu yeye nadhani kanielewa vizuri tena mno mjinga mkubwa.Bull shit.Halima Mdee behave yourself
Halima mdee hajatajwa popote kwenye mada hii,cha ajabu umekurupuka huko na mapombe yako kuanza kumwagia matusi dada wa watu bila sababu! Ntashangaa usipokula ban ya muda mrefu!
 
Yeye ndie mkuu wa Bawacha huyo asingetamka Bila kibali chake Bawacha hawana protocol Kila mtu msemaji? Hilo zigo ni la Halima Mdee kamtuma aongee Kwa niaba ya Bawacha soma heading
 
DSC_0127-620x308.jpg

UONGOZI wa Baraza la wanawake CHADEMA (BAWACHA)limelaani vikali kitedendo cha udhalilishaji kilichofanywa na jeshi la polisi dhidi ya Amina Mapunda (26) mkazi wa Kiswanya kijiji cha Mgundeni, tarafa ya Mang’ula wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Uongozi huo ulisema kuwa kitendo cha mwanamke huyo kujifungulia nje ya kituo cha polisi bila msaada wowote ni kitendo cha kinyama na kinatoa picha ni kwa jinsi gani jeshi la polisi linafanya kazi yake bila ueledi wa kutosha.

Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa BAWACHA, Grace Tendega na mbunge wa Viti maalumu amesema viongozi huo unalaani kitendo hicho na viongozi ndani ya jeshi la polisi wanatakiwa kujipima na kujitafakari kama kweli wanatosha au wajiuzulu.

Amesema kitendo cha jeshi hilo kumsababishia mwanamke huyo kujifungulia chini tena kwenye mchanga hakimdhalilishi yeye peke yake bali kinawadhalilisha akina mama wengi wa kitanzania na niukiukwaji wa haki za binadamu.

“Hapa unaweza kujiuliza mama anahusikaje na wizi wa mume wake,haya kama kweli waliona kuna vifaa vya wizi kwanini hawakuchukua vifaa hivyo kama ushahidi.

“Lakini inashangaza hao polisi hawakuona kama huyo mama ni mjamzito au hawajui mtu ambaye ni mjamzito,haya ni mambo ya ajabu sana kwa jeshi la polisi,” amesema Tendega.

Katika hatua nyingine Tendega amesema kama kweli jeshi la polisi lingekuwa na ueledi wa kazi yao ni kwanini wasingeweka matangazo kila kona kwa ajili ya kumsaka mharifu hadi wampate.

Katibu huyo mkuu wa BAWACHA amesema kitendo hicho ni kibaya na kuna kila sababu ya viongozi wa Jeshi la Polisi kuanzia ngazi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Kilombero, mkuu wa polisi Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania (IGP) pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi na Naibu wake wakajitafakari na kujipima kama kweli wanastahili kuendelea na kazi.

Amesema matukio ya aina hiyo yamekuwa yanajirudia mara kwa mara na jeshi la polisi limekuwa likikaa bila kuonesha juhudi yoyote ya kuwachukulia hatua wanaohusika na uharifu wa kuwatesa wananchi au kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

Tendega amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa vitisho mbalimbali lakini chama hicho na Baraza la Wanawake wa CHADEMA hawatanyamaza na badala yake kitapaza sauti kwa ajili ya kuwatetea wanyonge na kudai haki bila kuwa na woga.
Ugoro tupu!
 
Back
Top Bottom