BAWACHA waliomuunga mkono Mbowe wasema walioondoka CHADEMA wana kiburi na ubinafsi

BAWACHA waliomuunga mkono Mbowe wasema walioondoka CHADEMA wana kiburi na ubinafsi

Wameongea vizuri. Lakini anaevaa kiatu ndie anajua kina mbana wapi. Kwa sababu wewe haujabaguliwa hauwezi kusema wengine hawajabaguliwa. Swali la Kigaila hawajalijibu. Wao waendelee kwenye vita dhidi ya chama tawala, waachane na wakina Ruge.

Amandla...
 
Watabaki wale nadhifu pekee Mungu ameamua kuitakasa CHADEMA na kuiondolea najisi iliyokuwa ikiwatesa.
 
Hawa wanawake wana akili kuliko kigaila na mashoga wenzake
😃 😀 😄 😁 🤣 😂 ingawa it depends, kina Kigaila, Mrema wao ni wanaume, wanatakiwa kupeleka pesa za chakula nyumbani, hawa kina mama either kapata pesa or hajapata, sio jukumu lao ku finance mambo ya nyumbani. Ndio maana wanaume wamekimbia kutafuta fursa sehemu nyingine ili familia ziendelee kuishi
 
Wameongea vizuri. Lakini anaevaa kiatu ndie anajua kina mbana wapi. Kwa sababu wewe haujabaguliwa hauwezi kusema wengine hawajabaguliwa. Swali la Kigaila hawajalijibu. Wao waendelee kwenye vita dhidi ya chama tawala, waachane na wakina Ruge.

Amandla...
Kama kuaguliwa pekee kunakufanya uondoke kwenye chama basi jk nyerere angeshaiacha TANU kipindi cha kudai uhuru mana alifukuzwa hata kazi.
Huwezi kujua kwamba unabaguliwa kama nawe siyo mbaguzi.
Watu wanaanzisha movement baadae wanaikana wenyewe ati walikuwa wanatikisa kiberiti?
 
Huwezi kujua kwamba unabaguliwa kama nawe siyo mbaguzi.
Tofauti na unavyosema. Anayebaguliwa ndie anae jua kuwa anabaguliwa pamoja na machungu yake. Mbaguzi anaona kila kitu kiko sawa.
Watu wanaanzisha movement baadae wanaikana wenyewe ati walikuwa wanatikisa kiberiti?
Nyerere aliwahi kusema kuwa ataondoka CCM kama akiona kuwa inaenda kusiko. Alisema CCM sio mama yake. Hicho ndicho G-55 walichofanya. Hawajatikisa kiberiti, wamefanya kweli. Ni kazi ya waliobaki kuwathibitishia kuwathibitishia kwa vitendo kuwa walikosea kuondoka Chadema.

Ni upotoshaji kusema kuwa kuenguliwa kwao katika nafasi za uongozi ndio sababu ya baadhi ya G-55 kuondoka Chadema. Sababu walitoa ni:
1. Maoni yao kuto sikilizwa. Ingawa wenye chama wanaaema waliitwa kwenye mkutano wa watia nia ili wakatoe duku duku zao lakini mwenye akili aliona kuwa mualiko huo ulikuwa na nia ya kuwazodoa na sio kuwasikiliza. Wakati wa mkutano waliohudhuria walitakiwa kunyoosha mikono kama hawaungi mkono NRNE. Bwana mmoja alinyoosha mikono lakini reception aliyopata ilibidi aseme hakuelewa swali. Haya sio mazingira ya mjadala wa haki na uwazi.
2. Hamna mkakati wa kutekeleza NE. Kila wakiiliza walikuwa wanapigwa chenga.
3. Waliona mkakati wa kususia uchaguzi hautafanikiwa pamoja na kuwa utawanyima wanachama wa Chadema haki yao ya kikatiba ya kupiga na kupigiwa kura.
4. Matusi na lugha za kejeli dhidi yao.
5. Kutengwa na wenzao.
Nadhani haujui historia ya Nyerere na TANU. Nyerere aliacha kazi ili ajilite zaidi kwenye shughuli za chama. Kama vile alivyojiuzuru kwenye nafasi ya uongozi wa serikali ili akijenge chama chake.

Amandla...
 
Sema tu CHADEMA ya Mbowe na yenyewe ilikuwa imejaa mamluki na wachumia tumbo wengi sana. Yaani watu walikuwa wapo kimaslahi sana ukilinganisha na hii CHADEMA ya Tundu Lissu na John Heche! Kuanzia Mbowe mwenyewe na jamaa zake akina John Mrema, walikuwa wakitoka nje wanajifanya ni Makamanda. Ila wakiwa kwenye ufujaji wa fedga za chama, walikuwa hawana tofauti na ccm.

Hii CHADEMA ya sasa ikienda tu kujifunza mbinu walizotumia wapinzani wenzao wa Ghana, Senegal, Ivory Coast, Nigeria, Zambia na Malawi; nina uhakika ccm itaondoka madarakani kwa wepesi sana.
 
Back
Top Bottom