BAWACHA mnaiangusha CHADEMA!

Jamani BAWACHA amkeni, hutuwachukii, tunawapa changamoto.

Mkuu mimi siamini kuwa wanachukiwa ila BAWACHA wanajichukia wenyewe,kwa kukubali kuwa
kwenye uongozi halafu hawafanyi yale wanayopaswa kuyafanya.Kwa nini wanawafanya Mwenyekiti
na katibu wafanye kazi kwa kuugua kuwa hata BAWACHA wawasimamie wao!!!! Mimi nionavyo BAWACHA
walitakiwa kuwa kuwa Sweaper kule ambako viongozi wa kitaifa wanatakiwa kwenda kwa ajili ya M4C, wao
wanatakiwa wawe wameshapita na kuweka uongozi wao upande wa wanawake utaona hamasa kwa wanawake
kwenye mikutano ya M4C itakuwa kubwa zaidi hata ya vijana."Mama ndie msimamizi wa nyumba".
 
ni promo au?
Kujenga hoja tu ndo kumpe mtu uongozi?

ndiyo. ile jana alikua kwenye interview. Mi nilikua nasikia Dr.Slaa anamsifia lakini nilikua sijajua ni kwanini. sasa nimejua. dakika moja inafaa kumtambua mtu ni wa aina gani. mia
 
hamna mjadala hapa kwa manufaa ya cdm uongoz bawacha ni lazima uondolewe.bila kuwaunganisha wanawake cdm 2tajuta
 
Mkuu umesema vizur M4C BILA UHAMASISHAJ NA KUSIMIKA UONGOZI WA MABARAZA 2TAKUA 2NAPOTEZA MAANA YAKE DR.SLAA TAZAMA HILI KWA MAKINI
 
Nakubaliana na mleta hoja ila twende step kwa step!
Tukiwa tunakurupuka tutakurupikiwa tena vibaya sana! si kila anae ingia DCM lazima apewe uongozi!
Dada Ester namkubali sana tuu! ila bado tuna mda mwingi tuu wa 'kumthamanisha' kabla ya kumpa uongozi ndani ya chama
 
Kumthaminisha kungekua na maana nzuri zaid na faida kwa CDM kama akipewa nafas ndan ya BAWACHA ILIYOPWAYA HIZO NI CHANGAMOTO TU
 
Si lazima awe kiongozi anaweza akafanya kazi na kamanda mawazo kwenye M4C, mbona ye hajachaguliwa kitengo na anafanya kazi nzuri? Kama mtu mwenye hoja nzuri akiingia kwenye chama na moja kwa moja akapewa uongozi tutegemee makundi ya hatari sana kwenye chama, nimempenda esther kwa hoja zake lakini kupewa uongozi wa chombo nyeti kama BAWACHA nadhani ni mapema, apewe muda kama atataka aje agombee baadae wakati ameaminika tayari..
hivi shibuda na kupayuka kwake tungempa umakamu cdm ingekuwaje!??
 
Namuunga mkono aliyesema hatuwezi kumpatia uongozi kabla ya kujua anaweza nini.kujua kujieleza na kupanga mikakati,kuratibu mipango na kusimamia utekelezaji (uongozi) ni vitu viwili vinavyotofautiana kabisa.kufanya hamasa na kujua kuelezea jambo kama huyu dada Esta kunaendana.katika baraza la mawaziri wa Jk waziri anayejua kujieleza ni Wasira.kwa kigezo hiki alitakiwa awe rais wa nchi kwa kuwa anamzidi Jk kujieleza.lakin Wasira hafanyi vizuri hata jimböni kwake.
 
That's a stupid topic,am men but I know women are more in numbers u can't compare to men,hivyo succes ya chadema inatokana na nguvu kubwa ya kina mama,so stop demoralize women wing of chadema,then chadema hawakurupuki Kama vipi aingie kwa kinyang!anyiro
Msiwe mnashabikia ushenzi nyie mpunga nini?
 
ni promo au?
Kujenga hoja tu ndo kumpe mtu uongozi?
kujenga hoja ndio njia pekee ya kujua na ya uwazi ya kujua uwezo na mtazamo wako. Hata ukiwa na na madegree 200 lakini bubu, kama walivyo mabubu viongozi wa BAWACHA tutakutambuaje.

If youno something but you can’t tell people that you know is a good as you knownothing. BAWACHA mpoozi?
Waambieni CDM mnajua ninikilichowafanya mkagombea na kushinda hizi nafasi mlizo nazo.
 
watu aina yako ndio watafanya cdm ichelewe kuchukua dola.nguvu ya wanawake katika uchaguz n kubwa ndio maana kipindi cha uchaguz ccm kontena nyingi zinazoletwa ni za kanga
 
Mkuu ESTER WASSIRA NA SHIBUDA NI WATU WAWILI TOFAUT KABISA KIMTAZAMO
 
Kweli mkuu ni mabubu wamelala pono wanasubiri viti maalumu
 
Bavicha, sasa kumekucha amkeni. Mmeona Esta Wasira? Tafuteni hawa, sio lazima wawe viongozi, watumieni kujenga BAWACHA.
 

Bahati mbaya jana sikuhudhuria kongamano wal akuliangalia kwenye Luninga. Lakini jioni nilipita kwenye kijiwe changu cha kahawa na kama kawaida nikawakuta vijana ambao huwa nakunywa nao kahawa. Hawa vijana wengi ni wapenzi wa CDM na wachache wa CCM. Huwa nikifika pale kabla sijapata kikombe cha kahawa huwa tunaanza kuongelea yaliyojiri kwenye mambo ya siasa kwa siku husika. Basi jana nilipofika tu vijana wakaniuliza kama nilihudhuria kwenye kongamano, nikawaambia sikupata wasaa nikaombe wanipe yaliyojiri. Kwa kuwa wao waliangalia kupitia Luninga basi wakanipa meengi yaliyojiri. Lakini wote kwa pamoja walitoa sifa nyingi sana kwa Ester Wassira wakisema ni jembe jipya na muhimu kwa CDM na kwa hakika wakaniambia ni vyema huyu mdada akapewa nafasi ndani ya CDM.

Huenda CDM wamelamba dume.
 
Estar Wassira ndio hbr ya mjini
 

Bila shaka wewe ni mmoja wa viongozi wa BAWACHA ambao mmeshindwa kwendana na kasi ya M4C
kaeni pembeni muone watu wanavyopiga kazi ,mnawaza viti maalum tu!!!!
 
Bavicha, sasa kumekucha amkeni. Mmeona Esta Wasira? Tafuteni hawa, sio lazima wawe viongozi, watumieni kujenga BAWACHA.

Mkuu kwa nini naumia nilikwenda kijijini kwetu sehemu za Singida,kiukweli CDM inakubalika sana pale
na vuguvugu la mageuzi kwelikweli,ila tatizo nililoliona ni wanawake kutwa na vilemba vya CCM vichwani
nikaamua kufanya utafiti mdogo kwa nini akina mama wako nyuma kwenye mageuzi ,majibu yao ni karibu
yalifanana kuwa wao wanatembelewa na kujaliwa na akina mama wa CCM hawajaona mama wa CDM hivyo
wanadhani CDM inatakiwa kuwa kwa vijana na wanaume.Nilichogundua ni kuwa UWT wanajitahidi kuwabana
wanawake hasa vijijini wakijua ndio angalau wanaweza kupata kura zao.Viongozi Bawacha kama hamna wito
wa uongozi kaeni pembeni.
 
Bila shaka wewe ni mmoja wa viongozi wa BAWACHA ambao mmeshindwa kwendana na kasi ya M4C
kaeni pembeni muone watu wanavyopiga kazi ,mnawaza viti maalum tu!!!!
Inawezekana mkuu anajua kitumbu chake kitaingia mchanga
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…