BAVICHA yatangaza bingo kubuni nembo

BAVICHA yatangaza bingo kubuni nembo

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) linafanya mchakato wa kutafuta nembo yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya chama hicho.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi, ilieleza kuwa nembo hiyo itakuwa alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na mambo mbalimbali ya vijana ndani wa chama hicho.

Munishi aliwataka vijana wa CHADEMA na wapenda mabadiliko kubuni nembo kwa ajili ya alama ya baraza hilo.
"Ili kutoa fursa kwa vijana wabunifu kutumia vipaji vyao kutoa mchango wao kwa chama na baraza lao, tumeandaa shindano maalumu la ubunifu wa nembo na atakayeshinda atazawadiwa," alisema.

Munishi alisema wale wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano hilo, watapaswa kuzingatia vigezo muhimu ambavyo ni pamoja na rangi kuu za CHADEMA.
Alisema watakaokamilisha kazi zao, waziwasilishe makao makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kabla ya Machi 26.

Munishi alisema baada ya wadau mbalimbali kuwasilisha nembo walizozibuni, sekretaiati ya BAVICHA itazichambua na hatimaye kupata tatu bora ambazo zitawekewa utaratibu wa kushindanishwa kwa kuingizwa kwenye vyombo vya kimaamuzi, ili kupata nembo moja.
Alisema atakayeshinda atapatiwa sh 500,000 kama zawadi na cheti maalumu cha kutambua mchango wake kwa BAVICHA.

source:Tanzania Daima

Nimekuta tangazo hili pia kwenye Chadema Blog, na tangazo lenyewe liko hivi.

BAVICHA YAANZISHA SHINDANO LA KUPATA NEMBO YAKE​

Deogratias Munishi, Katibu Mkuu BAVICHA

Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) liko kwenye mchato wa kutafuta nembo yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya CHADEMA. Nembo hii itakuwa alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na mambo mbali mbali ya vijana ndani ya CHADEMA.

Katika kufanikisha upatikanaji wa nembo, BAVICHA inatambua uwepo wa vipaji mbalimbali vikiwemo vya ubunifu miongoni mwa vijana wa Tanzania ambao baadhi yao ni wanachama na wafuasi wapenda mabadiliko wa Chadema.

Ili kutoa fursa kwa vijana hawa kutumia vipaji vyao na kutoa mchango wao kwa Chama na Baraza lao, BAVICHA imeandaa shindano maalumu la ubunifu wa NEMBO YA BAVICHA na hivyo kukaribisha wale wote ambao wangependa kushiriki kwa kubuni nembo hii.

VIGEZO MUHIMU VYA KUZINGATIWA
Kwa wale wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano hili watapaswa kuzingaztia vigezo vifuatavyo katika ubunifu wao;
1. Rangi zitakazotumika ni lazima ziwe zinatokana na rangi kuu za CHADEMA
2. Nembo kuu ya Chama inaweza pia kutumika kubuni nembo ya BAVICHA
3. Mbunifu atoe maana halisi ya nembo atakayoibuni kwa mukhtadha wa vijana na maudhui mapana ya CHADEMA

MUDA WA SHINDANO
Muda wa shindano hili la kupata nembo ya BAVICHA utakuwa ni mwezi mmoja yaani kuanzia tarehe 26/02/2013 - 26/03/2013. Mbunifu anaweza kuwasilisha ubunifu wake moja kwa moja ofisi za BAVICHA zilizopo mtaa wa Togo Kinondoni – Manyanya, au kwa kutumia barua pepe: bavicha.chadema@gmail.com

MCHAKATO WA UCHAMBUZI
Baada ya wadau mbalimbali kuwasilisha nembo walizozibuni, Sekrataiati ya BAVICHA itazichmbua na hatimaye kupata nembo tatu bora ambazo zitawekewa utaratibu wa kushindanishwa na baadae kuingizwa kwenye vyombo vya kimaamuzi ili kupata nembo moja itakayotumiwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)

ZAWADI
Kwa kuwa shindano hili linalenga kuwapatia vijana wa CHADEMA na wasio wa CHADEMA lakini wenye mapenzi na CHADEMA fursa ya kutumia na kuvitangaza vipaji vyao na hivyo kutoa mchango wao katika ujenzi wa BAVICHA imara, mshindi wa shindano hili atapewa Shilingi 500,000/= kama zawadi na pia cheti maalumu cha kutambua mchango wake kwa BAVICHA.

WALENGWA
Walengwa wa shindano hili ni vijana wote wa CHADEMA pamoja na wanachama na wafuasi wa CHADEMA wenye ujuzi/kipaji cha ubunifu.

WITO
BAVICHA inawahamasisha vijana wa CHADEMA na wote wanaopenda mabadiliko kushiriki shindano hili ikiwa ni sehemu ya kuijenga taasisi hii ya vijana ndani ya CHADEMA

Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Katibu Mkuu - BAVICHA​
 
good move although the reward is not that much attractive .... they need to add more motivation e.g award of computer and or automatic qualification to a winner to do all BAVICHA designing contracts
 
Hapo sasa! Bora viwavi waliondolewa wapishe watu waijenge BAVICHA. Naomba kama vipi MOD waunganishe hiyo real tangazo na hiyo habari ya gazeti ili watu waeze kuona vigezo halisi na tunaoweza kushiriki tushiriki tukiwa na taarifa kamili.
 
MUNISHI mbona dau dogo sana, walau fanyeni milioni moja:tape2:

Kwa mtizamo wangu mimi sioni kama ishu ni dau hapo kwa kuwa walengwa ni wanachama , wafuasi na hata yeyote mwenye mapenzi mema na BAVICHA.

Naona ndio kitu cha msingi ambacho wakina Munishi wamezingatia kama ukisoma between the lines kwenye tangazo lao.

We kama una moyo shiriki wala usiangalie dau .
 
utekelezaji wa mipango ndio muhimu zaidi
 
good move although the reward is not that much atractive .... they need to add more motivation e.g award of computer and or automatic qualification to a winner to do all BAVICHA designing contracts
Dah! Mkuu umeenda mbali mno.
Mbona wasanii wanafanya kazi nyingi na kubwa kuliko hiyo ya kubuni logo ya bavicha, na sidhani kama wanapata zaidi ya 100,000/- kwa kila kazi.

Mfano mzuri angalia wale wachoraji kwa mfano; muda, nguvu na rasilimali wanazotumia kukamilisha kazi moja ya picha ya kubuni na kuchora. Halafu ulizia hiyo picha inauzwa shilingi ngapi. Utagundua zawadi iliyowekwa na Bavicha is beyond and above na kazi itakayofanywa.
 
Kwa mtizamo wangu mimi sioni kama ishu ni dau hapo kwa kuwa walengwa ni wanachama , wafuasi na hata yeyote mwenye mapenzi mema na BAVICHA.

Naona ndio kitu cha msingi ambacho wakina Munishi wamezingatia kama ukisoma between the lines kwenye tangazo lao.

We kama una moyo shiriki wala usiangalie dau .

Hii siyo nembo ya kibiashara. Kwa hiyo dau la laki tano(500,000/=) linatosha kabisa!
Kama ilivyowekwa wazi watakaoshiriki wengi ni wanachama wa CHADEMA, kwa hiyo basi watakuwa wanakisaidia chama chao kwa kuchangia kupitia ubunifu wa nembo hiyo!
 
Dah! Mkuu umeenda mbali mno.
Mbona wasanii wanafanya kazi nyingi na kubwa kuliko hiyo ya kubuni logo ya bavicha, na sidhani kama wanapata zaidi ya 100,000/- kwa kila kazi.

Mfano mzuri angalia wale wachoraji kwa mfano; muda, nguvu na rasilimali wanazotumia kukamilisha kazi moja ya picha ya kubuni na kuchora. Halafu ulizia hiyo picha inauzwa shilingi ngapi. Utagundua zawadi iliyowekwa na Bavicha is beyond and above na kazi itakayofanywa.

Mkuu .... kumbuka haya ni mashindano na huu ubunifu utatumika katika institution .... hii ni zaidi ya trade mark .... ubunifu wa uchoraji mwingine is just for fun and leisure uses .....
 
Kwa mtizamo wangu mimi sioni kama ishu ni dau hapo kwa kuwa walengwa ni wanachama , wafuasi na hata yeyote mwenye mapenzi mema na BAVICHA.

Naona ndio kitu cha msingi ambacho wakina Munishi wamezingatia kama ukisoma between the lines kwenye tangazo lao.

We kama una moyo shiriki wala usiangalie dau .

Nakubaliana na mawazo yako mia kwa mia.
 
Dah! Mkuu umeenda mbali mno.
Mbona wasanii wanafanya kazi nyingi na kubwa kuliko hiyo ya kubuni logo ya bavicha, na sidhani kama wanapata zaidi ya 100,000/- kwa kila kazi.

Mfano mzuri angalia wale wachoraji kwa mfano; muda, nguvu na rasilimali wanazotumia kukamilisha kazi moja ya picha ya kubuni na kuchora. Halafu ulizia hiyo picha inauzwa shilingi ngapi. Utagundua zawadi iliyowekwa na Bavicha is beyond and above na kazi itakayofanywa.

Correctly
 
Hivi Masalia na wale virus wakiona hivi wanahisikiaje?

Afadahali mmeondoka muwaache vijana wenye moyo wafanye kazi ya ujenzi wa baraza.
 
Wakisikia hivi wanatamani ardhi ipasuke wajifiche huko
 
Back
Top Bottom