hekimatele
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 9,889
- 2,805
wadau wa graphic design changamkeni sasa ndo muda huu wa kuonesha utofauti kati ya magamba na magwanda
BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) linafanya mchakato wa kutafuta nembo yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya chama hicho.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi, ilieleza kuwa nembo hiyo itakuwa alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na mambo mbalimbali ya vijana ndani wa chama hicho.
Munishi aliwataka vijana wa CHADEMA na wapenda mabadiliko kubuni nembo kwa ajili ya alama ya baraza hilo.
Ili kutoa fursa kwa vijana wabunifu kutumia vipaji vyao kutoa mchango wao kwa chama na baraza lao, tumeandaa shindano maalumu la ubunifu wa nembo na atakayeshinda atazawadiwa, alisema.
Munishi alisema wale wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano hilo, watapaswa kuzingatia vigezo muhimu ambavyo ni pamoja na rangi kuu za CHADEMA.
Alisema watakaokamilisha kazi zao, waziwasilishe makao makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kabla ya Machi 26.
Munishi alisema baada ya wadau mbalimbali kuwasilisha nembo walizozibuni, sekretaiati ya BAVICHA itazichambua na hatimaye kupata tatu bora ambazo zitawekewa utaratibu wa kushindanishwa kwa kuingizwa kwenye vyombo vya kimaamuzi, ili kupata nembo moja.
Alisema atakayeshinda atapatiwa sh 500,000 kama zawadi na cheti maalumu cha kutambua mchango wake kwa BAVICHA.
source:Tanzania Daima