BAVICHA wamvaa Rais Magufuli na Jaji Mkuu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) limemtaka Rais John Magufuli kuacha kuingilia bunge na kuamuru nini kijadiliwe, anaandika Pendo Omary.

Limefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mussa Azzan Zungu, Mwenyekiti wa Bunge kuagiza kuondolewa baadhi ya vipengele katika Hotuba ya Godbless Lema ambaye ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Vipengele hivyo vilihusu; mauaji ya viongozi wa kisiasa, mkataba tata wa Lugumi, uuzwaji wa nyumba za serikali, Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, sakata la vitambulisho vya taifa (Nida), mwenendo wa rais, kashfa ya ununuzi wa rada na bunge kulinda walarushwa.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo kwenye Makao Makuu ya chama jijini Dar es Salaam, Julius Mwita, Katibu Mkuu BAVICHA amesema, “vipengele katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni – Wizara ya Mambo ya Ndani vililazimika kuondolewa bungeni kwa sababu ya Rais John Magufuli.

“Tunashuhudia Rais Magufuli ndio anaongoza bunge kutoka Ikulu. Baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapigiwa simu na kutishwa akiwemo Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtera.

“Hata spika na naibu spika wanapata maelekezo ya kuendesha bunge kutoka kwa rais. Hotuba hii tutaendelea kuisambaza hadi kila mtu aisome,” amesema Mwita.

Mwita amesema, kutajwa kwa Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani kudaiwa kuwa mbia wa Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited, iliyoingia mkataba tata na Jeshi la Polisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. 35 Bilioni, ni sababu tosha ya waziri huyo kuwajibika au Rais Magufuli kutengua uteuzi wake ili kuipa uhuru Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuchunguza mkataba huo.

“Tunajua wazi bunge lingekubali mkataba wa Lugumi ujadiliwe kungemuingiza Kitwanga kwenye mgogoro. Rais Magufuli ni swahiba wa Kitwanga. Jipu la Lugumi limeonekana kuwa mwiba. Tunamtaka Rais Magufuli achukue hatua,” amesema Mwita.

Aidha, Mwita amemtaka Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu kufuta kauli ya kusifia Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 aliyoitoa hivi karibuni nchini Uingereza alipokuwa akizungumza na Watanzania waishio huko kuhusu faida na hasara za sheria hiyo.

“Kazi ya jaji yoyote sio kusifu sheria. Anapaswa kutafsiri sheria kwa msingi wa Katiba. Tunamtaka Jaji Mkuu aondoe tamko hilo haraka. Litasababisha majaji wengine kushidwa kutafsiri sheria hiyo la sivyo tutaitisha “petition” nchi nzima kupinga suala hili. Sisi vijana ndio tunaoumia na sheria hii kuliko makundi mengine,” amesema Mwita.

Katika mkutano huo Mwita aliongozana na Emmanuel Masonga, Mwenyekiti BAVICHA Mkoa wa Njombe na Edward Simbeye, Mwenezi BAVICHA.
 
BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) limemtaka Rais John Magufuli kuacha kuingilia bunge na kuamuru nini kijadiliwe

Polisi wakiwabana na koleo kwenye makalio kuwataka watoe uthibitisho kuwa Raisi Magufuli kaingilia,Watatoa macho kama mjusi aliyebanwa kwenye mlango na kulia lia hovyo bila kutoa huo ushahidi.
 
Kampuni ya Lowassa inajiita bavicha ...wakanywe viroba vyao watuache watz na rais wetu
 
Boom limeisha wanatafuta kick kwa DJ na mauvi na vijistatement vyao sawa nakupiga miayo hata mijusi ya ufipa haishtuki.
 
Bavicha ilishakufa kitambo, tangu walipoondoka kina juliana shonza.

Waliopo wamemis viroba vya wakati uchaguzi. Haya mzee keshawasikia atawafanyie maarifa makoo yasikauke
 
kuendelea kuamini kuwa kuna baraza la vijana chadema ni kuugua uendawazimu.

taasisi gani haina njia mbadala za kujitanua zaidi ya kusubiria matukio ili yawape promo!! Taasisi safi na thabiti hubuni njia mbalimbali za kuwasaidia katika mapambano yao.

lakini hawa bavicha wa sasa ni bavicha wa kuchunga mifugo na kushinda vibalazini kusubiri kuonewa huruma. Kiongozi shupavu huonyesha uwezo wake katika kuisaidia jamii isiyoelewa.

wananchi wa vijijini wanakufa njaa lakini wabunge wao wanapigania BUNGE lionyeshwe LIVE huu ni Ujuha kupindukia. Na ndio maana Chama kinakosa watu makini kwa kuwa wanashindwa kuzalisha viongozi bora
 
Wanatoa nao maagizo

(1)rais amshughlikie waziri kingwanga

(2)Jaji mkuu afute kauli ya kusifia sheria makosa ya mtandao


Sikua najua ni chombo kikubwa hivyo mpaka kiwaelekeze viongozi hao kufanya hayo.ikumbukwe mihimili ni mitatu.Serekali , bunge ambalo ni kusimamia serekali na Mahakama.ila naona mihimili imeongezeka na Mhimili wa Bavicha umechipua kwaajili ya kutoa matamko hewa .

1463509027641.jpg
 
Jaji mkuu wa Tanzania akiwa Uingereza, ameisifu Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kuwa ni sheria inayolinda haki, faragha, usalama wa taifa, nk.

Jaji Mkuu ameysema hayo alipokuwa akizungumza na watanzania waishio Uingereza walipomuuliza kuhusu sheria hiyo na mapungufu yake, ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo iliyosababisha kwa pamoja na Uchaguzi wa Zanzibar kama taifa tukose fedha za wafadhili takribani Trilioni 1.4.
Sote tunajua kuwa Sheria hii imetupa akisi mbaya mbele ya jumuiya ya kimataifa, imetuwekea alama na doa baya kwa washirika wetu mbalimbali, na kwa msingi huo kuifanya nchi yetu kutazamwa kwa jicho baya na nchi wahisani na washirika wetu wa maendeleo.

Sisi vijana wa CHADEMA, na wengine wote ambao ndio wahanga wakubwa wa sheria hii kandamizi, tumeshtushwa na kusikitishwa na kauli hii ya Kiongozi huyu mkuu wa Mahakama katika nchi hii.
Kauli ya Jaji Mkuu inaonyesha wazi kuwa sheria hii kandamizi ilitungwa na serikali ya CCM kwa ajili ya kuwakandamiza vijana, na hii inaonyesha wazi kuwa ama Jaji Mkuu hajaisoma Sheria hii kwa ukamilifu wake au na yeye ameingia katika msitari wa kujirahisi kwa Serikali ya Magufuli ambayo imeonekana wazi kuingilia mihimili mingine ya Dola ikiwemo mahakama yenyewe na Bunge.

Akiwa ni kiongozi mkuu wa mhimili huo wa dola wenye jukumu la kutafsiri sheria, na sio kuisifia, anatupa ishara kwamba, hakuna haki inayoweza kutendekea kwa mtu8 yeyote atakayeshitakiwa chini ya sheria hii maana ameishaitafsiri kuwa ni nzuri.

Ni wazi Jaji Mkuu amevunja misingi ya sheria anayoisimamia na ni wazi kuwa hafahamu kwa undani uonezi unaofanywa kwa vijana wanaoeleza fikra zao kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa yanayoendelea nchini.
Hii inawezekana ni kutokana na ukweli kwamba yeye ameridhika mno, na kwamba anajua hakuna askari anayeweza kumsimamisha na kumuomba simu yake ili ikaguliwe na kudukuliwa nk na hivyo kuamini kuwa sheria hii kandamizi ni kwa ajili ya watanzania wanyonge tu.
Vijana wenzetu wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa, na polisi kwa kutambua abaya na ukandamizi wa sheria hii wamekuwa wakiwakamata na kuwafungulia mashitaka yasiyo na tija wala maslahi kwa taifa hili na kwa mfano wa hivi karibuni ni Kijana wetu Bob Chacha Wangwe.

Kaul hiyo ya Jaji Mkuu ni kiashiria kwamba vijana wanaelekea kuzibwa midomo na kushindwa kueleza hisia zao kwa wenzao,na hii ni ishara ya wazi kwamba tayari Rais Magufuli ameamua kuiingilia na kuidhibiti mihimili mingine ya dola.
BAVICHA tunalaani vikali kauli hii ya Jaji Mkuu wa Tanzania, na kumtaka aifute kauli yake, ili kurejeshaheshima yake kama kiongozi wa mhimili huo wa dola wenye dhamana kubwa ya kutoa haki kwa watanzania.



4.0 MAUAJI YA VIONGOZI WA KISIASA.
Viongozi wa kisiasa hasa wale wa Upinzani wamekuwa wakiishi kwa kubaguliwa na kwa mateso makubwa sana hata wengine kuuwawa kwa sababu ya kazi na wajibu wao katika siasa na jamii.
Rafiki na ndugu yetu mpendwa Alphonce Chemu Mawazo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita aliuawa kinyama kule Katoro- Busanda - Geita , mchana , hadharani , tena karibu na kituo cha Polisi.

Sisi tulilia sana na kuhudhunika sana hata mpaka leo, na tulipohitaji kumzika kwa heshima anayositahili kama rafiki na Kiongozi wetu hatukuruhusiwa na Polisi , tulipigwa sana mabomu na wengine kama Mwenyekiti wetu wa Vijana Taifa Patrobas Katambi walipewa kesi ya kushambulia jambo ambalo ni la kutunga na uzushi na mpaka leo anakesi mahakama , Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo ulizuiwa kuagwa kwa ubabe na Jeshi la Polisi bila sababu za msingi mpaka Mahakama ilipotoa haki ya mwili kuagwa kule jijini kwao Busanda Geita.

Wakati mioyo yetu ikilia ndani kwa huzuni, kwa dhuluma, uonevu, ukandamizwaji, vipigo hata vifo vya marafiki zetu na ndugu zetu katika kazi zetu za siasa tunazofanya, nyie mnaona mambo haya ni ya kawaida,hii ni hatari kwa usalama wa Taifa, kwani subira na uvumilivu
vitakapoishiwa nguvu, kuna dalili ya mauaji ya ulipizaji visasi kuanza na itakapofika hapo usalama na amani ya Taifa letu utakuwa mashakani sana sisi kama Viongozi wa BAVICHA tumeanza kuona dalili hizo.
5.1 Mkataba tata wa Lugumi na Jeshi la Polisi.
Baraza la vijana tunamtaka Raisi kujibu maswali yafuatayo kwa kuwa Msemaji wake pamoja na Bunge wameshindwa kuijbu maswali hayo yalioulizwa na Kambi rasmi ya upinzani Bungeni Tunataka Maswali yafuatayo yajibiwe.

1.Kwa kuwa mikataba ya serikali kwa mujibu wa sheria lazima ufuate sheria za manunuzi na kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Je, Utaratibu huu ulifuatwa?

2.Je Mkataba huu wa LUGUMI ENTERPRISES na JESHI LA POLISI umetekelezwa ama haukutelezwa, na kama ulitekelezwa ni kwa kiwango gani, na ikiwa kulikua na tatizo la utekelezaji, Je, Jeshi la Polisi lilichukua hatua zipi?

3.Je, ni kampuni ngapi ambazo zinahusika na hatua za utekelezaji wa Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, kwa kuwa kampuni ya INFOSYS ambayo mmoja wa wamiliki wake ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga inatajwa kufunga vifaa hivyo (AFIS).

4.Ni kwanini C.A.G katika ukaguzi wake hakuhoji kuhusu uhalali na ulinganishi wa thamani ya pesa ya manunuzi na faida ya vifaa hivyo? Kampuni ya INFOSYS (inayomilikiwa na Mhe. Kitwanga) imedai kulipwa na Jeshi la Polisi, takribani Dolla za Marekani 74,000, Je fedha hizi Kampuni ya Mhe. Kitwanga ililipwa kwa kazi ipi iliyofanya na Jeshi la Polisi?

5.Ni kwanini mpaka sasa , Rais Magufili hajachukua hatua dhidi Said Lugumi, na aliyekuwa IGP Said Mwema / Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na kuwasimamisha kazi wale wote ambao bado wako kazini juu ya mkataba tata wa Lugumi
6.Tunamtaka Rais , kutengua mara moja uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe na kumrudisha nchini mara moja , kwani alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na ni imani ya Kambi rasmi kuwa alijua mambo yote yanayoendelea ya mkataba wa Lugumi

Idara ya habari

BAVICHA Taifa
 
Back
Top Bottom