BAVICHA wamuasi Mbowe, waapa kwenda Dodoma

Waache waende ndipo watakapojifunza nidhamu ya democrasia kuwa kwenda kinyume cha seikali ni hasara
Serikali ya makaburu ilikuwa na maguvu mara elfu kuliko yetu. W ananchi wasio na silaha wakiwamo watoto wa shule ndio walorudisha democracy. Kuna wengi waliuwawa na kufungwa jela, matunda ndio hayo hata vijana watz wanakimbilia sauzi kutafuta maisha. Wangewasikiliza watu wa aina yako, wangekuwa bado wananyanyaswa na kubaguliwa kama wanyama.
 
Intelligensia zimeshanasa tishio la kuwepo fujo za Bavicha. Bila shaka wanaosimamia masuala ya usalama watatimiza wajibu wao. Mikutano mingi ya kisiasa ilishafutwa katika mazingira haya. Mifano ipo mingi tu
Inteligensia iliyoshindwa kumwona Mh Lugumi? Au ipi?
 
Siku hizi huwa hakunaga busara wala hekima bali ni mihemko! HATA MIMI NI BAVICHA LAKINI KI UHALISIA LAZIMA TUNGECHEMSHA!! najua kuwa baada ya mkutano huu next CDM NASISI tutaitisha wetu tu!!
 
Umesahau kuna mkuu wa nchi kwa jina Gadafi alikimbilia ndani ya culvert na akachomolewa huko kwa kichapo na kumrestisha, au huyi hakua mkuu wa nchi kwa akili yako mgando?! Ogopa resolve ya watu wanaojitambua na kudhamiria kutimiza malengo yao, hakuna cha chifaru au mtutu au washawasha! Ni mtiti kwa kwenda mbele, liwalo na liwe!
Mh hii sasa ni hatari ya danger. Hivi watu 5,000 wanaweza kumrestisha rais? Labda rais wa Manzese
 
Kwa kuwa sikio la kufa huwa halisikii dawa, mimi naomba hao vijana waende Dodoma wakakione kilichomnyoa kanga kichwani.
 
dom hiyo.


swissme
Simba mwenda kimya ndio mla nyama. Kwa kelele hivi hakuna wa kwenda Dom. Kama watu wenye nia ya kweli wangekaa kimya wangeibukia Dom. Kunguri anapiga kelele sana, akitishwa tu ......
Swissyou
 
Kama kweli hao vijana wakifanikiwa kwenda Dodoma bila idhini ya Mbowe basi itabidi Mbowe ajitazame upya maana yawezekana umaarufu wake umeshuka mpaka vijana hawamtii tena afikirie kujiuzulu

Hata mimi nitashangaa sana kama hao vijana bado wataendelea kumtii Mbowe. Mbowe ndiye aliyekiweka chama kwenye hali hii kiliyo nayo leo kwa kumleta Lowassa kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe. Lowassa sio mwanachadema na wala hajawahi kuipenda cdm zaidi ya kuitumia cdm ili kukidhi matakwa yake ya kuupata urais. Kwa hapa Mbowe alipofikia ni bora akakaa pembeni yeye na Lowassa wakawaachia wale wenye damu ya cdm wakaendeleza mapambano. Toka nimjue Mbowe na Lowassa sijawahi kuwaona hata siku moja kwenye midahalo zaidi ya kuwaona wakihutubia jukwaani. Akae pembeni kwani wamekipotezea chama mvuto na muelekeo.
 
CDM wasipokuwa makini siasa za CCM zitawasambatisha.
Kinachoendelea sasa ni sawa na kunywa mchuzi wa miguu ya kuku.
 
Haya mambo tulikuwa tunayasikia kule Rwanda, sasa yamepiga hodi hapa kwetu. R.I.P Benito Mussolin.
 
BARAZA la vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limeapa kwenda mkoani Dodoma kusaidia jeshi la polisi kuzuia mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaandika Josephat Isango

Kiongozi mmoja mwandamizi wa BAVICHA makao makuu aliyezungumza na MwanaHALISI Online kwa sharti la kutotajwa jina lake amesema, uamuzi wa wao kwenda Dodoma uko palepale.

“Tumeshaamua kwenda Dodoma na hakuna yeyote anayeweza wa kutuzuia. Uamuzi wetu uko palepale na tutatekeleza kila ambacho tumepanga,” ameeleza.

Mkutano mkuu wa CCM umepangwa kufanyika mkoani Dodoma wiki mbili zijazo. Unatarajiwa kumchagua John Pombe Magufuli, kuwa mwenyekiti wa taifa wa chama hicho.

Msimamo mkali wa kiongozi huyo wa BAVICHA umefuatia uamuzi wa mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuzuia vijana wa Chadema kwenda Dodoma kukabiliana na CCM.

Mbowe alitoa kauli hiyo jana Jumapili, kufuatia kuwapo kwa taarifa kuwa jeshi la polisi nchini, limeapa kupambana na viongozi na wafuasi wa Chadema, ikiwa watafika mkoani humo kuzuia mkutano wa CCM.

Chadema kimeamua kuchukua hatua ya kukabiliana na CCM baada ya jeshi la polisi kuzuia mikutano ya ndani ya chama hicho; mikutano ya hadhara na mahafali yaliyopangwa kufanywa na Umoja wa Wanavyuo wa Chadema (CHASO), katika baadhi ya mikoa.

Kauli ya Mbowe imepingwa na baadhi ya vijana katika maeneo mbalimbali, ikiwamo mkoani Arusha, ambako uongozi wa mkoa umekabidhi kwa BAVICHA kiasi cha Sh. 5 milioni kwa ajili ya kwenda Dodoma.

Miongoni mwa mahafali ya Chadema yaliyovurumishwa na polisi, ni pamoja na yale yaliyofanyika mkoani Dodoma ambako mgeni rasmi alikuwa waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Mahafali ya Dodoma yalitarajiwa kufanyika katika hoteli ya African Dreems, yaliporomoshwa na polisi kwa kutumia mabomu ya machozi, silaha za moto na gari moja la maji ya kuwasha.

“Upole wa Mbowe na Edward Lowassa, ndiyo uliosababisha tukaibiwa kura na kushindwa kuandamana. Katika hili, hatuko tayari kumsikiliza yeyote,” ameeleza kiongozi huyo.
Anasema, “…kama Mbowe ameshindwa kuongoza chama basi ni vema akaamua kukaa pembeni na kuwacha wenye uwezo na ujasiri wa kutenda.

“Kama anaogopa kuwekwa ndani basi aache kabisa siasa hadi watakapopatikana polisi wapole atarudi kuwa mwenyekiti.”

Akiongea kwa uchungu kiongozi huyo mwandamizi wa Chadema anasema, “tunataka kwenda Dodoma ili azima yetu itimie. Ni lazima polisi na CCM wafahamu kuwa nchi hii siyo mali ya genge la watu wachache. Nasi ni umma ambao unapaswa kutendewa haki.”

Katika mitandao ya kijamii kumesheheni mijadala inayopinga kauli na msimamo wa Mbowe wa kuwazuia BAVICHA kwenda Dodoma na wengine kufikia hatua ya kumshambulia.

Baadhi ya waliojitokeza kupinga uamuzi huo wa Mbowe, ni viongozi wenzake wa Kamati Kuu (CC), Baraza Kuu la taifa (BKT), wabunge, madiwani na viongozi wa mikoa.

Hatua ya polisi kuzuia mikutano ya hadhara ilifuatia kauli ya Magufuli, aliyotangaza zuio la jumla la kufanyika mikutano ya kisiasa ya hadhara na ya ndani na kusema, “wanaotaka kufanya siasa wasubiri hadi mwaka 2020.”
Waende wakione cha moto.
 
Viroba vimeshawaharibu maini, siku zao zinahesabika, sasa wanatafuta sababu tu. Hatari sana kujihusisha na organization isiyo na nidhamu, uhuni mtupu
 
Simba mwenda kimya ndio mla nyama. Kwa kelele hivi hakuna wa kwenda Dom. Kama watu wenye nia ya kweli wangekaa kimya wangeibukia Dom. Kunguri anapiga kelele sana, akitishwa tu ......
Swissyou
lazima wajue kuwa tunakuja kuwasaidia police kwa shuruti


swissme
 
Back
Top Bottom