Bavicha temeke watoa tamko

Bavicha temeke watoa tamko

Kumekucha.
Dr.W.Slaa uwezi kufunga mjadala na huna mamlaka ya kufunga mjadala.
Asanteni sana vijana kwa kuendelea kujadili na kupinga unyanyasaji wa kina mbowe,lissu na dr slaa.

Mbowe hana jinsi ni lazima akubali demokrasia ichukue nafasi.

Chadema na viongozi wake wanaongozwa na gadhabu,visasi.

Vijana msichoke kuongea na hata kama wakiwatisha kuwafukuza msichoke kabisa.

Mbowe anaogopa sana demokrasia sana.

Afu we pi*bi wacha mambo ya kidemu nani kakuambia ametishwa? Siku zinasogea hivoo zikiisha ndio hivyo. Aache kutumia vibaraka wake kutoa mishuzi ovyo
 
Last edited by a moderator:
Huyu ni Mwwenyekiti wa Mkoa ama Wilaya Bavicha Temeke? Au huku ni mjumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu? Haijuihata katiba ya chama chake ? Aseme kifungu gani kimekiukwa ? Sio porojo kama za MACCM ,,,,,,,

Eti naye Kiongozi dah! Hata uenyekiti w nyumba kumi ni Hatar.
 
Hahahahahahahahahhahahahaha

Yaani na wewe unajiweka humo!!!!!

Ama kweli dunia haiwezi kuisha vituko.
Ritz FaizaFoxy THE BIG SHOW mmeona kijana muashi? Huyu ni mlaghaika, umuhimu wake ni kuongeza idadi ya watu kwenye maandamano tu!!!

Haaa! ZeMarcopolo ww unajua ni kijana mcute sana sikutegemea kuwa bongo yako imejaa kamasi
Na wewe uwa unatumika kufanya nini kijana mcute?
 
Last edited by a moderator:
Mbona vijana mnatokwa povu si muache ZZK wenu ajibu barua ya tuhuma, kama hawezi mmsaidie kujibu ya nini kuonyesha upuuzi wenu hapa jamvini???
Au bado fedha za TISS zinafanya kazi??
 
Options for this story
PIGA NIKUPIGE CHADEMA.

TAMKO LA MJUMBE WA BARAZA KUU , MKUTANO MKUU CHADEMA, MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA BARAZA LA VIJANA TAIFA (BAVICHA), MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TEMEKE NA MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO/WILAYA YA TEMEKE KUHUSU MGOGORO NDANI YA CHAMA NA UAMUZI WA KAMATI KUU KUWAVUA NYADHIFA MJUMBE WA KAMATI KUU Dkt. Kitila Mkumbo na NAIBU KATIBU MKUU zitto kabwe .

UTANGULIZI.

Mimi Patrick Y.Joseph, ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ninayeshikilia nyadhifa mbali mbali kwa sasa kama inavyoonekana hapo juu kwenye kichwa cha Habari. Ninawashukuru kujitokeza kwenu hapa ili tushirikiane kuufikisha ujumbe kwa Watanzania kuhusiana na maswala yanayoendelea kwenye chama chetu hivi sasa.

MIGOGORO NDANI YA CHAMA

Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia chaguzi mbali mbali za ndani ya chama, migogoro hii hupelekea mpaka kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika lengo likiwa ni kuwadhoofisha mbele ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Tumeiona mifano mingi ya namna hii, wakati marehemu Chacha Zakayo Wangwe alipotangaza kugombea uenyekiti mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote mpaka anapoteza uhai wake hakuwa akisemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama. Alichafuliwa na viongozi wenzie waliotofautiana msimamo.

Alipotangaza zitto kabwe kugombea uenyekiti hali ikawa hiyo hiyo, akaitwa msaliti, anatumika na mengineyo mengi, alipotangaza kujitoa kugombea akaachwa kidogo apumzike.

Tunakumbuka yaliyotokea wakati wa chaguzi za ubunge wa viti maalum, tunakumbuka pia chaguzi za mabaraza ya chama, wakati nagombea nafasi ya umakamo mwenyekiti wa vijana nako pia waliogombea uenyekiti waliitwa kila aina ya majina.

Kwa kifupi migogoro hii ni ya kutengenezwa ili kudhoofishana kuelekea chaguzi za ndani ya chama.
Hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa chama tumeshuhudia tena Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo wakikutana na dhahama hiyo hiyo.

Hali hii si nzuri kuruhusu iendelee kushamiri ndani ya chama maana haikijengi chama zaidi ya yote inakibomoa tu.

KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU
Nikiwa kama mjumbe wa Baraza Kuu la chama ninayewakilisha wilaya ya Temeke, na nikiwa kama mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la vijana la Taifa (BAVICHA)

Nimefadhahishwa sana na uamuzi uliofikiwa na kamati kuu ya chama dhidi ya ndugu Zitto kabwe na Dkt. Kitila mkumbo.
Ukiachilia mbali kwamba kamati kuu haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kufikia maamuzi iliyoyafikia na kuyatangaza kwa umma.

Lakini imeonyesha ni jinsi gani wametawaliwa na Chuki, Ghadhabu, Unafiki na Ubaguzi uliopitiliza.

Ni uamuzi ambao hauwezi kuungwa mkono na mwanachama yeyote mwenye akili timamu,kwa kuwa haukisaidii chama badala yake unapandikiza chuki miongoni mwa wanachama.
Uamuzi huu uliojawa na hofu kubwa ya kiuchaguzi, hofu ya madaraka na hofu ya kupoteza umarufu unapaswa kukemewa na kusababisha watu wenye akili timamu wajiulize mara mbili mbili kama ni sawa ama la.

Kwa mantiki hiyo basi, nikiwa kama mjumbe wa baraza kuu, ninatoa masikitiko yangu kwa kamati kuu kufanya kazi isiyowahusu tena bila kufuata hata kanuni wala Taratibu zozote za kinidhamu baina ya viongozi.

Ningependa umma utambue kuwa sikubaliani na uamuzi huu kwa kuwa haukidhi misingi ya kidemokrasia wala kufuata utawala wa sheria.

Haiingii akilini hata kidogo kwa chama kinachopanga mikakati mbali mbli ya kuhinda dola, kuwafukuza na kuwaogopa watu wanaopanga mikakati ya wao kushinda uchaguzi ndani ya chama.

Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na usaliti, basi Operesheni zetu za chama ikiwemo M4C zenyewe zinapaswa kuwa uhaini uliopitiliza kwa kuwa nazo ni mikakati ya chama kushika dola.

MSIMAMO WANGU.

Ninamtaka mwenyekiti akishirikiana na watendaji wengine wa chama waitishe mkutano wa dharura wa baraza kuu ili tutolee maamuzi sahihi swala hili.

Ninataka pia pamoja na agenda zitakazojadiliwa,
(i). watueleze ni kwanini wameamua kusambaza waraka wanaozani unawadharirisha kina zitto na mkumbo badala yake waraka huo unakidharirisha chama kwa kuonyesha madhaifu ya mwenyekiti na katibu mkuu wa chama.

(ii). Ni kwanini tusiamini kwamba maamuzi haya yameathiriwa na hofu ya chaguzi za ndani ya chama .

(iii). Ni kitu gani kimeifanya sekretarieti ya kamati kuu itangaze ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama baada ya kuwachafua miongoni mwa watu waliotarajiwa kugombea nafasi mbali mbali mpaka kuwavua uanachama.

Ni vema sasa tu tukijenge chama chetu bila kufuata maswala ya ubaguzi wa kidini na kikabila ama kikanda.

Chama chetu kimekuwa kikishtakiwa sana kuhusiana na matatizo ya kidini na kikabila, lakini pia chama chetu kimekuwa kikiwatumia Zitto na Arfi kama ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama, sasa inawezekanaje kuwatimua na kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia.

Mwisho ninapenda kusema kuwa huu ni msimamo wangu na kwamba sipo tayari kuburuzwa wala kuruhusu kuona tunaendelea kuibomoa demokrasia tunayoitangaza kila kukicha.

Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu, na kukishauri namna bora ya kuendeleza demokrasia ndani ya vikao na sita ogopa kueleza maoni yangu kwa Watanzania.

Nawashukuru sana.

Imetolewa na ;-

Joseph Y. Patrick
+255713802226
Mwenyekiti wa chadema wilaya/jimbo Temeke
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Temeke
Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Taifa

Naomba ziongezwe siku kumi na nne nyingine tuwajue wengi zaidi... Njaa mbaya sana jamani hasa kwa vijana kama hawa wanaotaka shortcut... Tutawajua weng sana mlio kwenye mgao... Tunawasubilia na wengine.
 
Kwa hizi siasa endeleeni kufaidi ruzuku. Ruzuku ikifutwa hamna kitu chadema.

Watu wana recoup investments zao. Hamna kumkomboa mtanzania maskini. Hakuna demokrasia. Uhuni mtupu
 
Elsfu saba saba za kuwalipa kila mkiandika humu zitasita ruzuku ikikata. Tafuteni kazi ya kufanya
 
Hahahahahahahahahhahahahaha

Yaani na wewe unajiweka humo!!!!!

Ama kweli dunia haiwezi kuisha vituko.
Ritz FaizaFoxy THE BIG SHOW mmeona kijana muashi? Huyu ni mlaghaika, umuhimu wake ni kuongeza idadi ya watu kwenye maandamano tu!!!

mbona unadharau kwa baba yako au hujui ,au hayo mandevu yanakupa kibuli..
 
Last edited by a moderator:
Fundi muashi ndie mshauri mkuu wa intelejesia ya chadema. Jason
 
Unachosha wasomaji bana! Una quote lipage loote wala huna cha maana anachoandika,katumwa na nani unadhani watu woote ni misukule kama wewe, bila ZZK hakuna CDM, haya nasubiri hayo matusi yenu maana mkizidiwa hoja mnaishia kutukana tu.

Wewe ndiye haswa msukule maana kupewa hiyo b7 umejisahau na hata ndugu zako wa vijijini ambao ni maskini wa kutupwa umewasaliti!Unashindwa kulalamikia ongezeko la umeme unakaa kumtetea bwana wako zzk?Kama mnamuona ni mzuri ci mumchukue kwenye chama chenu?
 
Haina shida mkuu wewe umechukua chako , ingefurahi km ungeondoka moja kwa moja
na tutawasikia wengi tu ,maamuzi yako sahihi zito hana lolote , na kukumbusha tu uwe
umechua pesa yakutosha vinginevyo wambie wakuongeze,

pili njoo kwetu sisi wanachama utwambie huo uogoro wako ilitukuelewe vizuri'
kinachonitia imani bado wapenzi wa chadema tuko imara.

 
Mbona vijana mnatokwa povu si muache ZZK wenu ajibu barua ya tuhuma, kama hawezi mmsaidie kujibu ya nini kuonyesha upuuzi wenu hapa jamvini???
Au bado fedha za TISS zinafanya kazi??

kamanda, hata kuku ukimkata shingo halafu ukamwachia unajua nini kitatokea ndicho kinachotokea kwa pm7+uvccm+ team zitto...
 
Iwapo viongozi kama hawa watapewa fursa ya kuongoza Bavicha Taifa basi chama na nchi kwa ujumla itapiga hatua kubwa ya maendeleo...

kwa nini wasiongozd uvccm mkuu?
Hahahaaa! Haya bwana patrick umesikika.
 
Unachosha wasomaji bana! Una quote lipage loote wala huna cha maana anachoandika,katumwa na nani unadhani watu woote ni misukule kama wewe, bila ZZK hakuna CDM, haya nasubiri hayo matusi yenu maana mkizidiwa hoja mnaishia kutukana tu.

Hapa na wewe unatofautiana nini na MSUKULE? If ZITTO is your mentor then you are a BIG LOOSER!!
 
Mtapiga kelele sana, kisha mtatulia Kama Madiwani waliotimuliwa Arusha, halafu tutawasahau na kusonga mbele.
 
Mbowe hana Option yoyote zaid ya kukabiliana na Zitto Kabwe kwenye Sanduku la kura hapo June 2014, Lazima aelezwe kuwa Multiple ID za Vifaranga zinazomvimbisha kichwa hazina athari kwenye Jamii ya Wanachadema wenzie ambao ndi wapiga kura Pia Slaa aandaliwe kisaikolojia kuwa Mchakato wa kumpata Mgombea Urais 2015 utafuata Misingi ya Demokrasi na sio kauli mbiu za Mbowe na Mtei kuwa eti yeye ndo mgombea kisa anakubalika.


Msema kweli kipenzi cha mungu.
 
Huyu katumwa na anatumika,au ndo kazi ya zile mil 5 zilizosemwa ktk mawasiliano ya emma,lukuvi na nchemba wakiapizana kumsaidia zzk? mtahangaika sana kusafishana lakn maamuzi ya kamati kuu ni sahihi.asiyependa awafate masalia wenzake akina chonza mrembo na mwam-cotton.

acheni mawazo mgando nyie akili za panzi bavicha jibu hoja sio kila anaekosoa chadema katumwa au anatumika...
 
Yona Joseph ninamfahamu vizuri sana ni homeboy wangu. Nina shauku ya kujua sababu zilizomsukuma kutoa tamko hili na ningeweza "kubet" sababu za yeye kutoa tamko hili lakini kwa leo sitasema chochote hadi nitakapoongea naye.
 
Back
Top Bottom