Bavicha temeke watoa tamko

Bavicha temeke watoa tamko

Kumekucha.
Dr.W.Slaa uwezi kufunga mjadala na huna mamlaka ya kufunga mjadala.
Asanteni sana vijana kwa kuendelea kujadili na kupinga unyanyasaji wa kina mbowe,lissu na dr slaa.

Mbowe hana jinsi ni lazima akubali demokrasia ichukue nafasi.

Chadema na viongozi wake wanaongozwa na gadhabu,visasi.

Vijana msichoke kuongea na hata kama wakiwatisha kuwafukuza msichoke kabisa.

Mbowe anaogopa sana demokrasia sana.
wewe Mjinga Nenda kanunue used computer Kama kawaida yako
 
nasubiri tamko la mkoa wa kilimanjaro au arusha wanaopinga ni wafuatao .ruvuma. mtwara.geita.vyuo vikuu,baregu. kigoma tuendelee
 
Ya NCCR & CUF yanatimizwa Chadema, hakika demokrasia ni ngumu ktk siasa za Tanzania.

Hakuna kitu hapo Mwana. Kwa Chadema wamegonga ukuta. Msaliti lazima aondoke. Na wanasema ukitaka kumfukuza kichaa, mtupie na makopo yake. Na hayo ndiyo makopo ya zito.
 
Kuzuia mazishi ya chadema ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mikono
 
Uongozi wa cdm hii ni fursa pekee ya kuwa tambua watu wa aina hii wako wengi na watazidi kujidhihirisha siku zinavyozidi kusonga mbele.
 
Kumekucha.
Dr.W.Slaa uwezi kufunga mjadala na huna mamlaka ya kufunga mjadala.
Asanteni sana vijana kwa kuendelea kujadili na kupinga unyanyasaji wa kina mbowe,lissu na dr slaa.

Mbowe hana jinsi ni lazima akubali demokrasia ichukue nafasi.

Chadema na viongozi wake wanaongozwa na gadhabu,visasi.

Vijana msichoke kuongea na hata kama wakiwatisha kuwafukuza msichoke kabisa.

Mbowe anaogopa sana demokrasia sana.

We malaya wa siasa
 
Last edited by a moderator:
Kuzuia mazishi ya chadema ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mikono

Nyie makenge mmekomaa na CDM wakati wanaichi mmewapandishia umeme kwa 68% hii ndo tutatoka nayo.
 
Mtalia sana lakini chama tayari tushasafisha mamluki,

Na wewe jiandae ama jiwajibishe mwenyewe kabla ya kuwajibishwa.
 
Options for this story
PIGA NIKUPIGE CHADEMA.

TAMKO LA MJUMBE WA BARAZA KUU , MKUTANO MKUU CHADEMA, MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA BARAZA LA VIJANA TAIFA (BAVICHA), MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TEMEKE NA MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO/WILAYA YA TEMEKE KUHUSU MGOGORO NDANI YA CHAMA NA UAMUZI WA KAMATI KUU KUWAVUA NYADHIFA MJUMBE WA KAMATI KUU Dkt. Kitila Mkumbo na NAIBU KATIBU MKUU zitto kabwe .

UTANGULIZI.

Mimi Patrick Y.Joseph, ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ninayeshikilia nyadhifa mbali mbali kwa sasa kama inavyoonekana hapo juu kwenye kichwa cha Habari. Ninawashukuru kujitokeza kwenu hapa ili tushirikiane kuufikisha ujumbe kwa Watanzania kuhusiana na maswala yanayoendelea kwenye chama chetu hivi sasa.

MIGOGORO NDANI YA CHAMA

Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia chaguzi mbali mbali za ndani ya chama, migogoro hii hupelekea mpaka kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika lengo likiwa ni kuwadhoofisha mbele ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Tumeiona mifano mingi ya namna hii, wakati marehemu Chacha Zakayo Wangwe alipotangaza kugombea uenyekiti mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote mpaka anapoteza uhai wake hakuwa akisemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama. Alichafuliwa na viongozi wenzie waliotofautiana msimamo.

Alipotangaza zitto kabwe kugombea uenyekiti hali ikawa hiyo hiyo, akaitwa msaliti, anatumika na mengineyo mengi, alipotangaza kujitoa kugombea akaachwa kidogo apumzike.

Tunakumbuka yaliyotokea wakati wa chaguzi za ubunge wa viti maalum, tunakumbuka pia chaguzi za mabaraza ya chama, wakati nagombea nafasi ya umakamo mwenyekiti wa vijana nako pia waliogombea uenyekiti waliitwa kila aina ya majina.

Kwa kifupi migogoro hii ni ya kutengenezwa ili kudhoofishana kuelekea chaguzi za ndani ya chama.
Hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa chama tumeshuhudia tena Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo wakikutana na dhahama hiyo hiyo.

Hali hii si nzuri kuruhusu iendelee kushamiri ndani ya chama maana haikijengi chama zaidi ya yote inakibomoa tu.

KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU
Nikiwa kama mjumbe wa Baraza Kuu la chama ninayewakilisha wilaya ya Temeke, na nikiwa kama mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la vijana la Taifa (BAVICHA)

Nimefadhahishwa sana na uamuzi uliofikiwa na kamati kuu ya chama dhidi ya ndugu Zitto kabwe na Dkt. Kitila mkumbo.
Ukiachilia mbali kwamba kamati kuu haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kufikia maamuzi iliyoyafikia na kuyatangaza kwa umma.

Lakini imeonyesha ni jinsi gani wametawaliwa na Chuki, Ghadhabu, Unafiki na Ubaguzi uliopitiliza.

Ni uamuzi ambao hauwezi kuungwa mkono na mwanachama yeyote mwenye akili timamu,kwa kuwa haukisaidii chama badala yake unapandikiza chuki miongoni mwa wanachama.
Uamuzi huu uliojawa na hofu kubwa ya kiuchaguzi, hofu ya madaraka na hofu ya kupoteza umarufu unapaswa kukemewa na kusababisha watu wenye akili timamu wajiulize mara mbili mbili kama ni sawa ama la.

Kwa mantiki hiyo basi, nikiwa kama mjumbe wa baraza kuu, ninatoa masikitiko yangu kwa kamati kuu kufanya kazi isiyowahusu tena bila kufuata hata kanuni wala Taratibu zozote za kinidhamu baina ya viongozi.

Ningependa umma utambue kuwa sikubaliani na uamuzi huu kwa kuwa haukidhi misingi ya kidemokrasia wala kufuata utawala wa sheria.

Haiingii akilini hata kidogo kwa chama kinachopanga mikakati mbali mbli ya kuhinda dola, kuwafukuza na kuwaogopa watu wanaopanga mikakati ya wao kushinda uchaguzi ndani ya chama.

Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na usaliti, basi Operesheni zetu za chama ikiwemo M4C zenyewe zinapaswa kuwa uhaini uliopitiliza kwa kuwa nazo ni mikakati ya chama kushika dola.

MSIMAMO WANGU.

Ninamtaka mwenyekiti akishirikiana na watendaji wengine wa chama waitishe mkutano wa dharura wa baraza kuu ili tutolee maamuzi sahihi swala hili.

Ninataka pia pamoja na agenda zitakazojadiliwa,
(i). watueleze ni kwanini wameamua kusambaza waraka wanaozani unawadharirisha kina zitto na mkumbo badala yake waraka huo unakidharirisha chama kwa kuonyesha madhaifu ya mwenyekiti na katibu mkuu wa chama.

(ii). Ni kwanini tusiamini kwamba maamuzi haya yameathiriwa na hofu ya chaguzi za ndani ya chama .

(iii). Ni kitu gani kimeifanya sekretarieti ya kamati kuu itangaze ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama baada ya kuwachafua miongoni mwa watu waliotarajiwa kugombea nafasi mbali mbali mpaka kuwavua uanachama.

Ni vema sasa tu tukijenge chama chetu bila kufuata maswala ya ubaguzi wa kidini na kikabila ama kikanda.

Chama chetu kimekuwa kikishtakiwa sana kuhusiana na matatizo ya kidini na kikabila, lakini pia chama chetu kimekuwa kikiwatumia Zitto na Arfi kama ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama, sasa inawezekanaje kuwatimua na kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia.

Mwisho ninapenda kusema kuwa huu ni msimamo wangu na kwamba sipo tayari kuburuzwa wala kuruhusu kuona tunaendelea kuibomoa demokrasia tunayoitangaza kila kukicha.

Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu, na kukishauri namna bora ya kuendeleza demokrasia ndani ya vikao na sita ogopa kueleza maoni yangu kwa Watanzania.

Nawashukuru sana.

Imetolewa na ;-

Joseph Y. Patrick
+255713802226
Mwenyekiti wa chadema wilaya/jimbo Temeke
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Temeke
Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Taifa

M-PESA nenda katowe
 
Naomba ni kusahihishe na nikuongoze.
Kwa usahihi wa jambo hili ni bora ungeweka wazi juu ya baraza kuu la january 28.2013 lililofanyika dsm moja ya maamuzi yake yalikuwa ni nini? Tuache kuwadanganya wanachama ambao hawanafursa ya kuingia kwenye vikao vikubwa kama hivyo.

Ndugu zangu napenda kuweka wazi ya kwamba mimi mwenyewe ni mjumbe wa baraza kuu, katika baraza kuu lililopita tuliagiza kamati kuu kushughulikia tuhuma za zitto na tulitaka kufanya maamuzi siku ile ile ya baraza kuu juu ya zitto ndipo mkt mbowe kwa busara zake akasimama na kuwaambia wanachama kuwa siyo vizuri kumuwajibisha zitto kwenye mahakama hii ya rufaa ambayo ndiyo kimbilio la kila mwanachama wa ngazi fulani anapokuja kukataa rufaa badala yake kamati kuu iende kukaa na ifanya maamuzi yake ndipo jambo hili liletwe kwenu viongozi na wajumbe wa baraza hili.

Nakumbuka wewe mleta uzi ama muandika habari ulikwepo na maamuzi ya kawa kamati kuu ikamahughulikie zitto kisha tuletewe taarifa za utekelezaji wa maazimio ya baraza kuu, ungesema kuwa kwanini kamati kuu imechelewa kumchukulia hatua wakati hayo yalikuwa ni maazimio ya baraza kuu la chama ningekuelewa na siyo kupotosha watu humu na hata zitto anajua ukweli huu maana alilia na kwenda chooni kufuta aibu baada ya wajumbe kuwa mbogo..zitto yumo humu aje abishe kuwa baraza kuu halikuagiza haya niliyoyasema ama mjumbe mwingine yoyote yule bila kupotosha.

Acheni kuwadanganya watu maamuzi yaliyochukuliwa ni sahihi kabisa wewe kama ni mjumbe wa baraza kuu tusubiri kikao hicho cha baraza kuu kwani ni lazima tutaletewa taaerifa ya maamuzi ya kamati kuu na sisi baraza kuu tutatoa ya kwetu.
 
Mtalia sana lakini chama tayari tushasafisha mamluki,

Na wewe jiandae ama jiwajibishe mwenyewe kabla ya kuwajibishwa.

Hahahahahahahahahhahahahaha

Yaani na wewe unajiweka humo!!!!!

Ama kweli dunia haiwezi kuisha vituko.
Ritz FaizaFoxy THE BIG SHOW mmeona kijana muashi? Huyu ni mlaghaika, umuhimu wake ni kuongeza idadi ya watu kwenye maandamano tu!!!
 
Last edited by a moderator:
Buku 7 team+ Team Zitto + PM7 mmeisha kazi.
 
Last edited by a moderator:
Naomba ni kusahihishe na nikuongoze.
Kwa usahihi wa jambo hili ni bora ungeweka wazi juu ya baraza kuu la january 28.2013 lililofanyika dsm moja ya maamuzi yake yalikuwa ni nini? Tuache kuwadanganya wanachama ambao hawanafursa ya kuingia kwenye vikao vikubwa kama hivyo.

Ndugu zangu napenda kuweka wazi ya kwamba mimi mwenyewe ni mjumbe wa baraza kuu, katika baraza kuu lililopita tuliagiza kamati kuu kushughulikia tuhuma za zitto na tulitaka kufanya maamuzi siku ile ile ya baraza kuu juu ya zitto ndipo mkt mbowe kwa busara zake akasimama na kuwaambia wanachama kuwa siyo vizuri kumuwajibisha zitto kwenye mahakama hii ya rufaa ambayo ndiyo kimbilio la kila mwanachama wa ngazi fulani anapokuja kukataa rufaa badala yake kamati kuu iende kukaa na ifanya maamuzi yake ndipo jambo hili liletwe kwenu viongozi na wajumbe wa baraza hili.

Nakumbuka wewe mleta uzi ama muandika habari ulikwepo na maamuzi ya kawa kamati kuu ikamahughulikie zitto kisha tuletewe taarifa za utekelezaji wa maazimio ya baraza kuu, ungesema kuwa kwanini kamati kuu imechelewa kumchukulia hatua wakati hayo yalikuwa ni maazimio ya baraza kuu la chama ningekuelewa na siyo kupotosha watu humu na hata zitto anajua ukweli huu maana alilia na kwenda chooni kufuta aibu baada ya wajumbe kuwa mbogo..zitto yumo humu aje abishe kuwa baraza kuu halikuagiza haya niliyoyasema ama mjumbe mwingine yoyote yule bila kupotosha.

Acheni kuwadanganya watu maamuzi yaliyochukuliwa ni sahihi kabisa wewe kama ni mjumbe wa baraza kuu tusubiri kikao hicho cha baraza kuu kwani ni lazima tutaletewa taaerifa ya maamuzi ya kamati kuu na sisi baraza kuu tutatoa ya kwetu.
Kilimanjaro moja mjumbe wa baraza kuu chadema.

No wonder...
 
Last edited by a moderator:
Mtalia sana lakini chama tayari tushasafisha mamluki,

Na wewe jiandae ama jiwajibishe mwenyewe kabla ya kuwajibishwa.

ni bora jeshi la watu kumi kuliko la watu mia ndani yake wasaliti kibao tutimue wakafie mbali tuanze na huyo zitto kitilla, mwigamba..
 
Strategy za masalia za kitoto mno. Yaani watoa tamko lako, walifanya letu sote!!! Kama mwampenda Zitto si mumpe wake zenu.
 
Back
Top Bottom