Nape KATIBU WA SIASA NA UENEZI CCM-TAIFA na Josephat Isango, MWENYEKITI WA BAVICHA-MKOA SINGIDA hawawezi kuwekwa kwenye ulingo mmoja na wakapambanishwa na watu wakalipia fedha zao kutazama tukio la kifo! Ni sawa na kutoa mtihani wa Chuo Kikuu kwa mtoto wa chekechea ukimshindanisha na mbobezi wa Chuo kikuu.
Wanachofanania watu hawa wawili ni UTANZANIA na kwamba wote ni WAAFRIKA. Wanachotofautiana kabisa miongoni mwao ni uwezo wa kujenga hoja, upeo, hadhi, elimu, uzoefu, fikara na kiwango cha uungwana. Nape kapata malezi ya kiuongozi kutoka kwa wazazi wake na uzoefu wa uongozi kupitia Chama chake.
Ukienda kilabuni, ikiwa wewe u-muungwana, bila shaka yoyote utakereka kwa makelele na nyimbo za walevi na mara nyingine waweza kukasirika sana. Ukiwakasirikia walevi, utakuwa unawakosea na kuwanyima haki yao. Ikiwa kama hoja za Isango ndizo bora kuliko za Nape, basi huyo Isango anao washabiki wa kufanana naye na hao wanayo haki ya kuwa hivyo, na kwakuwa yeye ni bora kuliko wao na wamfuate kwani hatutakuwa tumepoteza kitu
Ninawasiwasi sana na uwezo wako wa kufikiri hakika, samahani kama nitakua nimekutusi, kwako shida ni cheo au uwezo wa kujenga hoja? Kwa mtu yeyote makini, huwezi msifia Nape Nnauye kwa ujenzi wa hoja, hivi mtu makini unaweza kusema fulani ana kadi yetu hivyo ni mwananchama wetu wakati mtu huyo huyo anakitesa chama unachosema yeye ni mwanachama wake? Well tena mtu mwenyewe halipi hata michango na ada za chama? Anajua kweli hata katiba ya chama chake anacho kiongoza kweli huyu? Hivi sifa za mtu kuwa mwanachama huwa ni zipi? Mojawapo si ni hiyo ya mtu kuhamia chama kingine, wapi katika chama imeandikwa, once unapoondaka kwenye chama A kwenda B lazima urudishe kadi ya chama hicho ulicho kiasi? Hilo Moja, huyu huyu alisikika akisema eti, Elimu Bure ni sera ya ccm, kwa uwezo wako wa kutunza kumbukumbu za juzi tu, hilo hivi ni kweli? Mi nadhani hiyo ilikua sera ya Mwl. JK Nyerere (RIP) magamba hiyo wamekua wanaipigia kelele kwamba haiwezekani, tena hata huyo katibu mkuu mpya, nilimwona mwenyewe Star TV akifanya interiew, yeye alikua Dar na DR. Slaa akiwa Mwanza wakati ule wa kampeni, let just be serious, kuitetea ccm, nakubaliana na mtu 1 hapa alisema, kunahitaji akili ya mwendawazim au maiti, hiki chama hakiteteeki hiki, kipo tu ICU, mbona haya hata media zinazofanya utafiti wa kutosha zinakiri hivyo? Umeangalia CNN lakini mkuu!
Misango ni zaidi ya Nape, tofauti zao ni vyeo tu, huyu yupo Taifa na mwingine yupo ngazi ya mkoa, hilo naomba nalo usije ukaona kama ni sifa, si kila mwanafunzi anayeshika nafasi ya kwanza hua na akili kuliko wanfunzi wote, inawezekana akawa na akili kwenye hilo darasa lake na sio wanafunzi wote, unaweza kuwa wa kwanza kwenye darasa la wajinga, siku ukipelekwa darasa la werevu utajikuta uanshika nafasi ya mwisho, muulize Nape kwenye Kura za maoni za ubunge mwaka 2010, aligombea ccm akiwa hana pesa (hii inajulikana ndani ya ccm, no money no Vote, of course kumbuka alikua na bifu ma katibu mkuu wa chama wakati huo) alipotaka kuja CHADEMA aliwe hilo sharti la kua mgombea ubunge pale Ubungo, aliaambiwa, Mnyika ni zaidi yako wewe, ni kama Mto na Bahari, na wote tuanaona!