BAVICHA Singida wamshukia Nape

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
0
CHAMA CHADEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA.

MKOA WASINGIDA.

TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI:

Watanzania wengi wanatambua mapambano ambayo chamachetu (CHADEMA) kinayaendesha kiasi cha kutishia CCM kuendelea kuwepomadarakani mwaka 2014 na 2015, ni mapambano ya haki dhidi ya udhalimu, ni mapambano ya matumaini dhidi ya kukata tamaa, ni mapambano ya uadilifu dhidi yaufisadi.

Kwa kuelewa hilo, sisi vijana wa CHADEMA, Mkoa wa Singida tunamwonya Katibu wa Itikadina Uenzi wa CCM Taifa, Bw. Nape Nauye kwa kuwatumia vibaya vijana wa kitanzania wasio na ajira, na ambao ‘wamefika bei' kulingana na matarajio ya mafisadi.Vijana wanaonunulika na mafisadi, hawawezi kamwe kuwa viongozi kwanihawatashindwa ‘kufika bei' siku nyingine na kuuza nchi. Hivyo hawafai kuwaviongozi wa nchi.

Tumepokea kwa masikitiko makubwa kuwa Nape na baadhi ya viongozi Mafisadi wanatumia pesa zao kuwatumia vijana wa kitanzania wasio naajira, na kupandikiza migogoro ndani ya CHADEMA, chama pekee cha kutumainiwa nawatanzania ili kuleta maisha bora. Tunamwonya Nape aachane na siasa za majitakazisizo na tija kwa shida za watanzania.

Badala yake, Nape kama anataka kuwa Mwanasiasa Mzuri, awaeleze watanzania jinsi alivyoshindwa kusimamia mkakati wa kujivua gamba,ulioasisiwa na Chama chake. Alizunguka nchi nzima kuelezea dhana ya kujivuagamba lakini siku hizi anafanya kazi na wale aliowatukana usiku na mchana kuwani magamba.

Nape awaeleze watanzania, jinsi Meli za Katibu Mkuu waChama chake, Abdulrahman Kinana, anavyosafirisha meno ya tembo nje ya nchi wakati serikali inalalamika kila siku kuna ujangili katika mbuga zetu, na itakuwa vema zaidi Nape akijitokeza kuwaambia watanzania kwanini hadi sasa tangu kuibuka kwa taarifa kuwa meli zilikuwa ni za Abdulrahmani Kinana Serikaliya CCM haijazitaifisha meli hizo. Sheria za nchi yetu zipo wazi kuhusu chombo chochote kitakacho kamatwa na maliasili zetu ni lazima kitaifishwe. Je, hivi vyombo vya usafiri vya Katibu Mkuu wa CCM vinangoja nini kutotaifishwa hayo ndo mambo ambayo Nape anaweza kuwaambiawatanzania, na yana manufaa kwao.

Bavicha Mkoa wa Singida, tunawapongeza vijana wenzetu wa Mkoa wa Mwanza kwa kutoa tamko zuri, na sisi vijana wa CHADEMA Mkoa wa Singida hatupo tayari kutumiwa na CCM wala kutumikia mafisadi. Tutakilinda Chama chetu na viongozi wake na hatutakubali propaganda ambazo hazina tija kwawatanzania.

Tunakiomba Chama chetu kiwachukulie hatua vijana wote waliosimamishwa uongozi sehemu mbalimbali nchini lakini wameendelea kujipachika vyeo bandia ili kuhalalisha utoaji wa matamko yasiyo rasmi. Nami kama msemaji wa BAVICHA Mkoa wa Singida, Nasisitiza kuwa hatuna mpango wowote wa kuandamana kusaidia propaganda za CCM. Dhumuni la dirisha kwenye nyumba nikupitisha hewa,cha kushangaza ukilifungua wataingia inzi, mbu na vingine ambavyo havikusudiwa.

Tunachotaka kusema sisi BAVICHA Singida ni
kuwa mbu, nzi na kunguni wameshaingia kwenye chama, kilichobaki kunatakiwa kufanyike usafi kwa umakini wasijewakachafua zaidi.

Lakini vijana waliosimamishwa uongozi ndani ya CHADEMAni vema wakajiunga na CCM wazi ili wakasaidie mafisadi waliosababisha maisha magumu kwa watanzania. Watanzania wanajua hali yao ya maisha, na ndio waamuzi sahihi wa Tanzania wanayoitaka, tusiwalishe maneno ya uongo kurutubisha Ufisadi nchini.

Josephat Isango,
MWENYEKITI WA BAVICHA-MKOASINGIDA.
 

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
2,000
Yes! Nakukubali sana mpiganaji wangu Josephat Isango.
Ahsante BAVICHA-SINGIDA kwani Chama kinahitaji vijana wenzangu kama nyie na sio wale waasi.

Peoples power.
 

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,085
2,000
Nimeambulia kitu humu.. Mbona watu wa CHADEMA wakiandika vitu ukavisoma Yaani vinaeleweka kabisa.. Tofauti Na M-CCM , akiweka bandiko ukalisoma Yaani hadi kichwa kinakuuma, post Za William, Nape Na mask zao zote, ukisoma hadi unajiuliza hivi huyu Mtu kweli ana akili au karogwa..

Siongelei kishabiki lakini wewe soma tu lazima wakukere, hakuna mwenye uwezo Wa kujenga hata robo ya Hoja.. Naamini sasa wenye akili wote wameshahama ccm.. True
 

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,122
2,000
CCM, iko wapi Mali emper? Uko wapi utawala wa RUMI ulio kuwa na nhuvu za ajabu? Uko wapi utawala wa Shaka zuzu? Iko wapi Soviet Union? Iko wapi KANU?

Jamaa watakuja kuvuna aibu ya Kipee siku moja, na TBCCCM yao na Star TVCCM watakuja vuna aibu, wajifunze yaliyo tokea kule Zambia
 

Malolella

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
366
195
Asante Bavicha Singida. Wanaanza kuvuliwa nguo taratibu. TUNTEMEKE na kujiapiza kwake sijui ataficha wapi uso wake. Sheme on u TUNTEMEKE na kundi lako.
 

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,122
2,000
Nimeambulia kitu humu.. Mbona watu wa CHADEMA wakiandika vitu ukavisoma Yaani vinaeleweka kabisa.. Tofauti Na M-CCM , akiweka bandiko ukalisoma Yaani hadi kichwa kinakuuma, post Za William, Nape Na mask zao zote, ukisoma hadi unajiuliza hivi huyu Mtu kweli ana akili au karogwa..

Siongelei kishabiki lakini wewe soma tu lazima wakukere, hakuna mwenye uwezo Wa kujenga hata robo ya Hoja.. Naamini sasa wenye akili wote wameshahama ccm.. True

Kule CCM wamebakia na akili za kuwaibia Watanzania, wanawaibia hadi wagonjwa wa Ukimwi, na hawa jamaa wanayo laana kubwa sana na ndo inawatafuna kwa sasa,
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,225
Hili ndio jukumu la viongozi wa vijana , kwani sisi wengine tunashangaa sana kuona hayo yanayoendelea kwenye baraza lenu na matamko husika
 

Magwangala

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,141
2,000
Huyu mwanafalsafa Josephat Isango ndiye Mkiti wa Bavicha Singida?kusema ukweli cdm ina hazina ya watu wanaojua kwa usahihi matumizi ya kichwa!
 

LUCAS KISIMIR

Member
Sep 11, 2012
29
0
Nape KATIBU WA SIASA NA UENEZI CCM-TAIFA na Josephat Isango, MWENYEKITI WA BAVICHA-MKOA SINGIDA hawawezi kuwekwa kwenye ulingo mmoja na wakapambanishwa na watu wakalipia fedha zao kutazama tukio la kifo! Ni sawa na kutoa mtihani wa Chuo Kikuu kwa mtoto wa chekechea ukimshindanisha na mbobezi wa Chuo kikuu.

Wanachofanania watu hawa wawili ni UTANZANIA na kwamba wote ni WAAFRIKA. Wanachotofautiana kabisa miongoni mwao ni uwezo wa kujenga hoja, upeo, hadhi, elimu, uzoefu, fikara na kiwango cha uungwana. Nape kapata malezi ya kiuongozi kutoka kwa wazazi wake na uzoefu wa uongozi kupitia Chama chake.

Ukienda kilabuni, ikiwa wewe u-muungwana, bila shaka yoyote utakereka kwa makelele na nyimbo za walevi na mara nyingine waweza kukasirika sana. Ukiwakasirikia walevi, utakuwa unawakosea na kuwanyima haki yao. Ikiwa kama hoja za Isango ndizo bora kuliko za Nape, basi huyo Isango anao washabiki wa kufanana naye na hao wanayo haki ya kuwa hivyo, na kwakuwa yeye ni bora kuliko wao na wamfuate kwani hatutakuwa tumepoteza kitu
 

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
0
Safi sana Kijana, Kumbe wenye akili mpo mnaacha Vilaza wanasumbua kutoa mtamko. Mlikuwa wapi?.
 

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,211
0
Tunawashukuru Bavicha singida kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa letu na cdm kiujumla kwa ajili ya ukombozi wa awamu ya pili. God bless u!
 

Manyi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
3,253
1,195
Wale waliokuja na tuhuma za kumuunganisha Zitto na hii saga leo sijaona comments zao!
 

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
195
Wanachotofautiana kabisa miongoni mwao ni uwezo wa kujenga hoja, upeo, hadhi, elimu, uzoefu, fikara na kiwango cha uungwana. Nape kapata malezi ya kiuongozi kutoka kwa wazazi wake na uzoefu wa uongozi kupitia Chama chake.

LUKAS KISMIRI, Asante kwa hoja yako, bahati nzuri ndo naingia JF nimeikuta, nimefurahi kumbe unafikiri sisi ambao Baba zetu hawajawahi kuwa viongozi CCM ndo hatuna HADHI, Sisi sio WAUNGWANA, Sisi ambao hatujapata malezi ya Kiuongozi toka kwa walezi wenye Uzoefu toka Chama cha Mapinduzi ndio hatuna Uwezo wa Kujenga Hoja, wala Upeo wala fikra za kuuliza rasilimali za watanzania zinavyoibiwa, na kuwaomba watanzania wasifuate propaganda ili tushirikiane kudai mali zilizoibwa na tabaka la watu wenye 'HADHI'.

Kumbe Nyie mlio tabaka tofauti na sisi ndo mnajua mna hadhi sana kuliko sisi.............. Watanzania wanasoma hapa, wanajua tulivyoibiwa na bado wanaona. Wanaona baada ya kuiba pesa zao mnakuja na dharau kujiita wenye hadhi tofauti, Wenye Elimu tofauti, Wenye Malezi ya Waliowahi kuwa Vigogo wa CCM.

Asante kwa kuunga Mkono tamko langu kwa namna ambayo wewe hukujua. Rashidi alisema Yana Mwisho haya akapanda karandinga kwenda gerezani-KULI-By Shafi Adam Shafi
 

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,244
1,500
CCM, iko wapi Mali emper? Uko wapi utawala wa RUMI ulio kuwa na nhuvu za ajabu? Uko wapi utawala wa Shaka zuzu? Iko wapi Soviet Union? Iko wapi KANU?

Jamaa watakuja kuvuna aibu ya Kipee siku moja, na TBCCCM yao na Star TVCCM watakuja vuna aibu, wajifunze yaliyo tokea kule Zambia

MKUU SI UKO TU, WAKO WAPI GHADAF PIA SAADAM? HAWA WALIKUWA NA MAJESHI VERY STRONG BANA .
VIJANA WENZETU WA SINGINA SAFI SANA TMEWAKUBALI, MMETUPA UJUMBE MARIDHAWA NA TUKO PAMOJA, CHADEMA NI NYUMBA YETU SOTE SI BUSARA KUGOMBEA FITO, ELA ZA MAFISADI NI HARAMu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom