Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 54,555
- 43,960
Watanzania bana kwa misaada ya kujionyesha kulikuwa kuna haja gani kupiga picha na mfuko wa unga, mpeni misaada endelevu sio kumpelekea mfuko wa mahindi na sukari.
Watanzania bana kwa misaada ya kujionyesha kulikuwa kuna haja gani kupiga picha na mfuko wa unga, mpeni misaada endelevu sio kumpelekea mfuko wa mahindi na sukari.
Ritz aka tume ya Katiba htakuja tena labda kama analaana.
wapenda sifa , wauza sura hao, acheni siasa misibani.
Nawapongeza Bavicha Arusha kwa jambo hili.Hizi ndizo siasa zinazofaa.siasa zinazojali utu na kuthamini mchango wa mashujaa wetu katika harakati hizi
Comrade Nanyaro Ephata na makamanda wengine kwa ujumla hongereni sana kwa jambo hili.Tushirikiane tuone njia ya kuisadia familia hii
Wakati huu pia tuendelee kushinikiza Jeshi la polisi kuhakikisha kila aliyehusika katika tukio lile haki inatendeka.Katika harakati hizi tunapoteza wenzetu wengi njiani,wengine wanajeruhiwa.Tuonyeshe mshikamano kwa vitendo katika kukabiliana na casualities zitokonazo na mapambano haya.
Wapenda mabadiliko wote Jf tuangalie namna ya kusaidia familia hii kwa kushirikiana na BAVICHA na hata chama
Nitawasiliana na kamanda Ephata(mwenyekiti BAVICHA-Arusha) tuone namna bora ya kufanya hili
Napendekeza BAVICHA waandae mkakati wa muda mrefu wa kuisaidia familia hii, japo bado sijajua uwezo wao wa kiuchumi. Ni kweli mahitaji kama mchele, unga na sabuni tuupeleke, lakini tutapeleka hadi lini? hebu kaeni chini, angalieni namna ya kuikwamua familia hiyo ambayo imeondokewa na bread winner kwa namna ya uwekezaji ambao utawasaidia maisha yao yote. Angalieni, kuna watoto wanaosoma? kama ndiyo tuweke mkakati wa kusaidia hata ada. Pia huyu mama anaweza kupatiwa mtaji gani ili afanye kazi itakayomwingizia kipato cha kudumu bila kutegemea kuletewa ready made food.
Ni hayo tuu wadau