Uchaguzi wa Katibu Mkuu BAVICHA 2019: Upepo wamwendea vizuri CPA Kitalika Titho

THE FORBES

Member
Nov 25, 2019
7
45
Wanazengo salaam.

Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu kinachoendele katika uchaguzi ndani ya BAVICHA hasa kwa wagombe sita wanaofahamika yaani huyu CPA KITALIKA, Hemed ALLY, Simbeye Edward, Nusrate Hanje, Gwamaka Mbughi na Chacha Machera.

CPA Kitalika, Gwamaka na Chacha hawakabiliwi na kipingamizi cha umri kama wengine lakini kuna utofauti mkubwa baina ya wagombea hawa watatu katika nafasi hiyo nyeti ya ukatibu wa BAVICHA.

Gwamaka ameanza kukabiliwa na shutuma za kuhusishwa na Cecil Mwambe ambaye ni mgombea wa uenyekiti wa chama Taifa akimkabiri Freeman Mbowe. Kashfa hii haiwezi kuamcha salama hata kidogo hasa ukizingatia shaka anayotiliwa mh Mwambe kwamba anatumika na TISS. Kashfa ya kutumika na Mwambe haijamuacha salama pia mgombea mwingine kwa nafasi hii, huyu ni Edward Simbeye anatuhumiwa kufadhiliwa malazi na chakula wakati wa safari yake mkoani Dodoma hivi karibuni katika kikao cha KK ya chama.

Katika hali isiyo na afya, Katibu wa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Siame Gideon amemtuhumu Gwamaka kama mtu mbinafsi sana na asiyependa kujishusha mbele ya wengine. Wahenga wanasema ukitaka kuruka agana na nyonga, Gwamaka hajapata baraka za makamanda wengine wa Mbeya kitu ambacho kitamletea shida sana katika uchaguzi huu.

Chacha Machera mgombea ambaye amejipatia umaarufu kupitia mtandao wa twitter amechukua fomu jana, lakini wakosoaji wanamuona kama ni mtu asiye mtulivu na ambaye asingefaa katika nafasi hii nyeti. Wanamkosoa kwa tweet zake ambazo huwa zinamakosa mengi ya kimantiki na mpangilio na asiyependa kusikia ukosoaji juu yake.

Nusrate Hanje, ni Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya na mkoa wa kigamboni. Ni mwanamke pekee katika kinyanganyiro cha nafasi hiii nyeti. Ukiacha kuzungumzia jinsia yake ambayo nayo yaweza kuwa kikwazo katika mbio zake za kusaka ukuu wa BAVICHA haonekani kama ni mtu mwenye weredi na maarifa ya kukidhi matakwa ya wapigakura wengi.

Turufu kuu imebakia kwa mgombea huyu mwenye sifa za kipekee na asiye maarufu sana katika mitandao ya kijamii. CPA KITALIKA, TITHO.E anasifiwa sana kwa utulivu na umakini katika kila jambo alifanyalo. Katika mkoa wa Arusha anakumbukwa kwa jinsi alivyoshirikiana na wenzake kuanzisha CHASO na kuchaguliwa kuwa mratibu kwa awamu mbili mfululizo.

Ephata Nanyaro, Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Arusha mjini mjini na ambaye amefanya kazi kwa ukaribu na mgombea huyu anakumbuka jinsi CPA KITALIKA, TITHO.E alivyopambana kutaka kuanzisha CHASO TAIFA. Ni mtu mwenye ndoto na kudhubutu kutenda jambo litokee. Mwaka 2017 alishiriki kuandaa mswada wa kanuni za kuongoza CHASO TAIFA, mswada huu ulikabidhiwa kwa pro. Baregu mjumbe wa KK na mshauri wa masuala ya siasa katika chama.

Mwaka 2015 alishiriki katika kampeni za uchaguzi wa ubunge jimbo la Mafinga mjini kama mjumbe wa timu ya kampeni na mkufunzi, aliandaa mkakati wa namna sera za mgombea wa Urais na ubunge zitakavyofundishwa kwa viongozi wa chama katika matawi na misingi ili wawe waenezi wazuri na watetezi wa wagombea wa CHADEMA katika maeneo yao. Alizunguka na mgombea katika kata zote sita za jimbo la Mafinga Mjini.

Mwenyekiti mpya wa chadema mkoa wa Iringa bwana William Mungai na ambaye alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Mafinga katika uchaguzi huo ana muelezea CPA KITALIKA, TITHO.E kama mtu ambaye anafaa kupewa nafasi hiyo nyeti ndani ya baraza na chama.

Kwa tathmini ya mpaka sasa CPA Kitalika anaungwa mkono na wapigakura wengi zaidi kutoka kanda ya kaskazini, magharibi, kati, Zanzar na Nyasa. Naona jinsi ambavyo BAVICHA inaenda kuwa imara chini ya Katibu Mkuu imara.
 

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
2,707
2,000
Mwambe kwanza mengine baadae.

Mwambe ni dawa sahihi ya kuiondoa ccm madarakini, kwani hawezi kuuza chama kwa makapi ya ccm kama DJ alivyofanya .
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
27,001
2,000
Mwambe kwanza mengine baadae.

Mwambe ni dawa sahihi ya kuiondoa ccm madarakini, kwani hawezi kuuza chama kwa makapi ya ccm kama DJ alivyofanya .
Yaani ndiyo mnazidi kumharibia,yaa adui na mtesi wetu atuchagulie kiongozi!!!!!! Hapa mumebugi kinoma
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,510
2,000
Yaani ndiyo mnazidi kumharibia,yaa adui na mtesi wetu atuchagulie kiongozi!!!!!! Hapa mumebugi kinoma
Unajua hawa watu tokea wawe na huyu mwenyekiti wao msema hovyo matumizi ya akili yamekuwa madogo mno. Sasa kwa akili zao wanadhani huo ni ushawishi?
Ndio maana mzee meko anasimama huko njiani watu wenye shida ya maji hata visima hawana anawaambia tumenunua ndege nane! Ili iweje katika shida ya maji?
 

GFAZA

Member
Dec 17, 2017
24
45
CPA Titho kitalika E. Hakika anatosha pasina Shaka kwenye nafasi hiyo aliyoomba. Ni kijana machachari,muadilufu na mpenda chama kwa muda mrefu.

Nami naungana na Wote wenye mapenzi mema kumtakia ushindi katika nafasi hiyo ya utendaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom