Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,408
- 10,601
Leo katika mahojiano ya mtuhumiwa mmoja kwenye kesi ya ugaidi inayovuma limetumika neno "Battle Confusion". Mtuhumiwa ambae alikuwa Komandoo alisema alipotoka Congo kwenye misheni aliambiwa ana " Battle Confusion" na kuondolewa kwenye kazi yake ya uanajeshi. Hili neno sijawahi kusikia ila nadhani linatokana na literal translation ya " kuchanganyikiwa vitani".
Ninachojua ni kuwa watu wengi ambao wamepitia katika matukio yenye taharuki kubwa kama vita huwa wanaugua kitu kinaitwa " Post Traumatic Stress Disorder ( PTSD)". Hali hii imewatokea sana askari waliopigana Afghanistan, Iraq na sehemu nyingine. Ni hali inatakiwa matunzo bora na tiba, sio kufukuzwa kazi. Kwa vile inaelekea tuna askari wengi wanaorudi kutoka kwenye misheni inabidi jeshi letu liupe uzito suala hili.
Amandla..