Battery yangu ya solar inaisha nguvu haraka

Wanu

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
353
223
Habari wana JF?
Battery yangu ya solar imekuwa ikipoteza nguvu ndani ya masaa mawili baada ya kuwa full charged, ni battery ya maji (acid) na pia nimeshawahi kuiongezea maji(acid) mara mbili kwa kipindi tofauti ila hakuna improvement. Je kuna utalaamu wowote naweza kufanya ikarudia hali yake hata kwa 50 -70%?. Nawasilisha hoja
 
Habari wana jf?
Battery yangu ya solar imekuwa ikipoteza nguvu ndani ya masaa mawili baada ya kuwa full charged, ni battery ya maji (acid) na pia nimeshawahi kuiongezea maji(acid) mara mbili kwa kipindi tofauti ila hakuna improvement. Je kunautalam wowote naweza kufanya ikarudia hali yake hata kwa 50 -70%?. Nawasilisha hoja
Battery ya Solar au nyingine yoyote haiongezwi acid kamwe. Battery ikipungua nguvu ongeza distilled water sio Acid mkuu. Kwa maelezo yako inaonekana battery imekufa japokuwa ili kujiridhisha inabidi kujua umekaa nayo muda gani na kama inaweza kuwa recharged
 
Mwanzo ilikuwa na acid nikajuwa acid ndio suluhisho, au nimwage niweke distilled water? Battery nimekaa nayo miaka miwili.
 
Habari wana jf?
Battery yangu ya solar imekuwa ikipoteza nguvu ndani ya masaa mawili baada ya kuwa full charged, ni battery ya maji (acid) na pia nimeshawahi kuiongezea maji(acid) mara mbili kwa kipindi tofauti ila hakuna improvement. Je kunautalam wowote naweza kufanya ikarudia hali yake hata kwa 50 -70%?. Nawasilisha hoja
Kabla ya kununua ingine jaribu kusugua terminal zake kwa msasa kwani nina wasiwasi haiwi full charged mchana. Pia angalia wire wa kutoka kwenye panel. Unaweza kujaribu charging system kwa kuweka balbu kweny waya zitokazo kwenye sola kabla ya kufika kwenye betri (kawaida huwa zinatoa mwanga)
 
Mwanzo ilikuwa na acid nikajuwa acid ndo suruhisho, au nimwage niweke distilled water? Battery nimekaa nayo miaka miwili.
Panel yako ni watts ngapi? Ili nikushauri zaidi. Pia bei ya battery sio hiyo kaka, kwa sasa zimeshuka bei
 
Daah boss langu ni N100 dukani wanauza 350,000 tsh na hali yangu kiuchumi si nzuri kabisa, ngoja tusubili wajuzi waje huwezi juwa twaweza pata solution.
Tatizo, watu wengi wenye solar system, huwa hamzichaji hizo batteries to full charge.... na huwa mnazitumia mpaka baatery ya 12V inafika 8V... Ukiifikisha battery hapo, una-destroy cells. Zikishaharibika hutaweza kuzichaji tena to full capacity

Halafu anayekushauri ununue battery ya Ampare Hour kubwa (N100), je solar panels zako zina uwezo wa kuichaji hiyo battery?

Kumbuka, wakati wa mchana, jua linapokuwepo, solar panels, zinapeleka umeme sehemu mbili, mzigo wako (Taa, na vifaa vyote vinavyotumia umeme wa hiyo solar) na kuchaji battery. Sasa kama hesabu haijapigwa vizuri, hutakuja kuijaza hiyo battery, na utakuwa unaitumia kabla haijajaa kila siku, HENCE WITH TIME, ITAKUFA...
 
Kabla ya kununua ingine jaribu kusugua terminal zake kwa msasa kwani nina wasiwasi haiwi full charged mchana.Pia angalia wire wa kutoka kwenye panel.Unaweza kujaribu charging sysstm kwa kuweka balbu kweny waya zitokazo kwenye sola kabla ya kufika kwenye betri (kawaida huwa zinatoa mwanga)
OK sawa nitajaribu hilo kesho wakati Jua likiwaka.
 
Habari wana jf?
Battery yangu ya solar imekuwa ikipoteza nguvu ndani ya masaa mawili baada ya kuwa full charged, ni battery ya maji (acid) na pia nimeshawahi kuiongezea maji(acid) mara mbili kwa kipindi tofauti ila hakuna improvement. Je kunautalam wowote naweza kufanya ikarudia hali yake hata kwa 50 -70%?. Nawasilisha hoja
Polesana, nakushauri nunua betry ya dry. Zinakaa sana na chaji na ni imara
 
Tatizo, watu wengi wenye solar system, huwa hamzichaji hizo batteries to full charge.... na huwa mnazitumia mpaka baatery ya 12V inavika 8V... Ukiifikisha battery hapo, una-destroy cells. Zikishaharibika hutaweza kuzichaji tena to full capacity

Halafu anayekushauri ununue battery ya Ampare Hour kubwa (N100), je solar panels zako zina uwezo wa kuichaji hiyo battery?

Kumbuka, wakati wa mchana, jua linapokuwepo, solar panels, zinapeleka umeme sehemu mbili, mzigo wako (Taa, na vifaa vyote vinavyotumia umeme wa hiyo solar) na kuchaji battery. Sasa kama hesabu haijapigwa vizuri, hutakuja kuijaza hiyo battery, na utakuwa unaitumia kabla haijajaa kila siku, HENCE WITH TIME, ITAKUFA...
Panel yangu ni watt 90, nawashia taa 5 pekee. Au ninunue N50 ya gari inaweza kufaa?
 
Sikushauri ununue dry cell hata kidogo, kwani battery hizi si nzuri licha ya kusema kwamba haihitaji matengenezo. Huwa batery dry hufa mapema kabla ya acid na huweza kupasuka kwani ziko sealed hivyo hewa hushindwa kutoka hasa kunapokuwa na overcharging.
 
Mimi natumia N100 na 200W panels na ninafurahia mno solar system yangu kwani battery hii hujaa kabisa kila siku hata ningeweka battery 2 pia zingejaa licha ya kutumia laptop asubuhi hadi jioni. Angalia charger yako. Ni vizuri ukawa na charger yenye digital display kwani utajua mwenendo wa chaji na hata kama kuna excess voltage hivyo kupanga matumizi kuna kuwa rahisi.

ProSolar charger controller ni nzuri natumia kwa mwaka sasa na nimefurahi mno. System yangu ina taa 4 za watts 5, taa 2 za watts 2 ambazo huwaka usiku mzima. Bado taa nyingine 4 za vyumba huwashwa saa 1 jioni hadi saa 4 usiku. Pia tv panasonic kubwa kuwashwa kuanzia saa 2 hadi saa 4 usiku na siishiwi chaji hata siku 1.
 
Mkuu betri yako imekaa miaka miwili imejitahidi sana ukizingatia ulikuwa huijazi vya kutosha.
Kwa hiyo panel kama hujakaa sawa chukua n50 itakusaidia sana.
Chunguza njia zako kama kuna loose wire au zilizoungua uzitoe
 
Fazili umenena, charger control nunua digital hiyo ndio utakuwa na uhakika na matumizi ya solar, inauzwa 60,000
 
Back
Top Bottom