NADHARIA Bata huendelea kuota manyoya mengine wakati akinyonyolewa

NADHARIA Bata huendelea kuota manyoya mengine wakati akinyonyolewa

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Wakuu naomba kufahamu ukweli kuhusu ili.

Ama ni imani tu tulionayo kutokana na kwamba bata huwa na manyoya mengi sana.
1753854541688.png
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwa na nadharia kwamba bata aliyechinjwa, manyoya yake huendelea kukua wakati wa kunyonyolewa. Wengine wamekuwa wakieleza kuwa wamekuwa wakiambiwa kuwa wasiongee wanapokuwa wanamnyonyoa ndege huyo.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa hiyo ni nadharia tu ambayo haina uthibitisho wowote wa kisayansi.

Tovuti ya Sussex wildlife trust kupitia makala yao yenye jina la How do feathers grow?, wameeleza kuwa;

"Manyoya hutengenezwa katika mizizi ya manyoya (follicles), sawa na nywele ambazo hutengenezwa katika mizizi ya nywele. Manyoya na nywele vyote huwa na sifa ya kufa, hivyo haviwezi kujirekebisha vinapoharibika au kuchakaa. Badala yake, ni lazima vianguke na nafasi yake kuchukuliwa na manyoya ama nywele mpya. Mchakato huu hujulikana kama moulting."

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la National libraray of medicine, yenye kichwa “The developmental biology of feather follicles” wanaeleza pia kuwa manyoya ya ndege hufa na kuja mapya lakini wanabainisha kuwa jambo holi hutokea kipindi ambacho ndege yupo hai.

“Kama ilivyo kwa mzunguko wa ukuaji wa nywele, mizizi ya manyoya yaani (follicles) pia hupitia mzunguko wa kumwaga manyoya kwa kujirudiarudia katika maisha yote ya ndege. Manyoya yanaweza kuota upya kwa njia ya asili (kupitia mchakato wa kumwaga manyoya) au kwa njia isiyo ya asili (kupulizwa au kung'olewa). Wakati unyoya unapong'olewa au kupotea kwa bahati mbaya, unyoya mpya kwa kawaida huanza kuota kutoka kwenye mzizi wa zamani ndani ya kipindi cha wiki mbili.”
Back
Top Bottom