Basil Mramba kupanda kizimbani leo

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Messages
1,408
Points
2,000

Informer

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2006
1,408 2,000
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba anatarajia kuhojiwa leo na mawakili wa Serikali, baada ya kumaliza utetezi wake kuhusu tuhuma za kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Mramba, atahojiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, mbele ya jopo la mahakimu, John Mtemwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika.

Mramba, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Grey Mgonja wanadaiwa kutumia madaraka vibaya kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart.

”Si kweli kwamba kuna fedha zilipotea Serikali ilipoingia mkataba na Alex Stewart ...kiasi kinachodaiwa kuwa ni hasara ni kodi iliyosamehewa.

"Huwezi kusema samehe kodi kisha urudi ukidai nilisamehe alafu nimepoteza, unadai hasara.

"Serikali imepata faida kubwa, faida ya kuingia mkataba na

Kampuni ya Alex Stewart si ya kifedha, ni faida ya kiuchumi na kisiasa," alidai Mramba kwa kuongozwa na wakili wake Peter Swai.

Mramba alidai katika utetezi wake kuwa, utaratibu waziri anashauriwa na Katibu Mkuu pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na katika suala hilo wote walimshauri.

Alidai baada ya taratibu zote kufanywa na watendaji, mkataba ulipelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo, Andrew Chenge ambaye alielekeza apelekewe Waziri wa Fedha, Mramba asaini.

Mshitakiwa huyo, alidai mkataba huo uliokuwa na sharti la kusamehe kodi aliusaini na kwa utaratibu wa kawaida, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikuwa haihusiki katika kutoa ushauri.

Alidai baada ya Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa kukubali fedha zitafutwe kwa ajili ya kuilipa kampuni hiyo, aliomba kibali Baraza la Mawaziri cha kumruhusu kupeleka suala hilo bungeni.

"Nilipata kibali, nikaupeleka kwa ajili ya utaratibu wa kuombea fedha katika bajeti ya mwaka 2003/2004, Bunge liliidhinisha fedha zote zipatikane kwa kazi ya ukaguzi wa madini, zilipwe kwa Kampuni ya Alex Stewart," alidai Mramba.

Chanzo: Mtanzania | Novemba 28, 2012
 

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
6,299
Points
2,000

R.B

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
6,299 2,000
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba anatarajia kuhojiwa leo na mawakili wa Serikali, baada ya kumaliza utetezi wake kuhusu tuhuma za kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7......
 

Forum statistics

Threads 1,392,869
Members 528,740
Posts 34,120,589
Top