Basi la Superfeo lapata ajali Songea

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000
SUPERFEO YAUA TENA SONGEA

KAMPUNI ya mabasi ya Superfeo inayosafirisha abiria toka jijini Mbeya hadi mjini Songea leo tena imepata ajali katika eneo la Hangagadinda wilayani Songea na kuua mtu mmoja ambaye alikuwa ni kondakta wa basi hilo .

Meneja huduma wa Kampuni hiyo Fransisi Sengo anasema ni siku moja tu imepita baada ya ajali nyingine ya superfeo kutoka Mbeya kuja Songea kupata ajali juzi katika kijiji cha Mbangamawe wilayani Songea na kuua dereva wa basi hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Songea ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ametembelea eneo la ajali ambapo Inadaiwa ajali hiyo ilisababishwa na dereva ambaye alikuwa anaongea na simu huku anaendesha gari.

Mgema ameagiza vyombo vya dola kufuatilia tabia za madereva ikiwa ni pamoja na kuwapima viwango vya ulevi ili kupunguza ajali zisizo za lazima.
3c9050a5252297d9e50daf8b4e826479.jpg
8f1bd51bc286d686ccadb2700712e7b1.jpg
 

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Ijumaa moja ya Basi la Kampuni ya Super Feo lilipata ' ajali ' na likaua ' Dereva ' tu na ni jana Jumamosi Basi la Kampuni hiyo hiyo ( Super Feo ) lilipata ' ajali ' na likaua ' Kondakta ' kitu ambacho kiukweli ' kimetutisha ' sisi Wasafiri wa ' Kutukuka '.

Je hili jambo linaashiria nini?

Nawasilisha.
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
42,666
2,000
Ijumaa moja ya Basi la Kampuni ya Super Feo lilipata ' ajali ' na likaua ' Dereva ' tu na ni jana Jumamosi Basi la Kampuni hiyo hiyo ( Super Feo ) lilipata ' ajali ' na likaua ' Kondakta ' kitu ambacho kiukweli ' kimetutisha ' sisi Wasafiri wa ' Kutukuka '.

Je hili jambo linaashiria nini?

Nawasilisha.
Yakiendelea kuua madereva na makondakta watakuwa makini kuzuia hizo ajali.(dereva na konda)
 

Vupu

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
1,775
2,000
Dalili za kupotea utajiri...

Gari imejigawa vipandevipande kitu kisichocha kawaida
 

Oxx

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
740
1,000
Asilimia kubwa ya Madereva wengi washirikina sana.... Uwez jua!
 

Prince Kunta

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
17,965
2,000
Huwa sinahusishwa na imani. nilisikia kitambo kipindi nipo Njombe. Kulikuwa hakuna ziendazo Dar
 

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
302
500
Kuna moja ya kaskazini huku nilisikia haiuwi abiria yenyewe ni kinda au dereva tu.

Yaani utasikia ajali lakini atakufa kati ya konda au dereva na baada ya muda itajirudia tena .

Ila ikitokea dereva au konda ambae ni Fundi kwenye Yale mambo amemzidi mmiliki au mcha Mungu basi utashangaa anafukuzwa Kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom