Basi la Sauli lapata ajali Picha ya Ndege, Kibaha. Wanne wajeruhiwa, 40 wanusurika

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
46,924
122,195
Nimepita sasa hivi eneo hilo nimeona Sauli imegongana na Lori, Sauli imesukumizwa mtaroni hadi ikapanda kingo ya mtaro.

Sijajua kama kuna majeruhi na idadi yake.

Inaonekana walishindwa kupishana Sauli akaamua kupita upande wa kushoto mwa Lori likiwa linaelekea Mashariki hapo ndipo zikagongana(ila sio uso kwa uso), Sauli imekwaruzwa sana upande wa kushoto, vioo vyote vya upande huo vimeharibika, kuna uwezekano abiria waliokuwa wamekaa upande huo kujeruhiwa

=====

Basi la Sauli limepata ajali katika harakati za kukwepa kugongana uso kwa uso na Lori

Kibaha.

Watu wanne wamejeruhiwa na wengine 40 kunusurika baada ya ajali ya basi ya kampuni ya Sauli eneo la Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani .

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Agosti 23, 2021 saa 6:45 asubuhi baada ya dereva wa basi hilo ambaye jina lake halikupatikana mapema kulielekeza pembezoni za barabara ili kukwepa kugongana uso kwa uso wa uso na lori lillokuwa likitokea mbele yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema;

"Dereva alikuwa anaovateki gari lililokuwa mbele ya macho yake na baada ya kulitazama aliona lori linakuja mbele yake akalielekeza pembezoni mwa barabara basi hilo na likachegama," alisema.

Alisema kuwa majeruhi hao waliwahishwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi ambapo walipatiwa matibabu na kisha kuruhusiwa.

 

Attachments

  • twitter_20210823_163234.mp4
    886.8 KB
Ni kweli
IMG-20210823-WA0012.jpg
IMG-20210823-WA0013.jpg
IMG_20210823_063507_1.jpg


Sent from my M2006C3LI using JamiiForums mobile app

IMG-20210823-WA0011.jpg
 
Back
Top Bottom