Basi la Moro Best limepata ajali

Basi la Moro Best limepata ajali

Kuna mtu kaandika humu anasema wawili wamekufa na ajali imetokea Kibaigwa, hebu tujuzeni ipi ni habari sahihi zaidi maana nijuavyo kibaigwa ipo baada ya njiapanda ya mpwapwa kama waenda Dodoma kama sijakosea
 
ha ha ha as Idimi says natumia outdated NOKIA

Kimbweka kwani uongo?
Sisi akina team 'WEKA PICHA' a.k.a TOMASO hatuamini habari hadi picha iwekwe. Na kwa jinsi mchina alivyoteka soko la simu, almost kila simu ina kamera, UNLESS iwe Nokia tochi kama yako (sina uhakika kama ina internet, huenda uko cafe)
 
Basi la Moro best likitokea Dodoma kwenda Dar limepata ajali mbaya sana muda huu eneo la Kibaigwa, ni mwendo kasi na imekoswa koswa na maroli na basi kabla ya kutumbukia kwenye mtaro, maiti wawili tayari wametolewa, majeruhi ni wengi mno na huenda idadi ya waliokufa ikawa kubwa zaidi, tuko katika jitihada za kunasua watu walionasa.
Picha baadae.

ni morobest iliyotokea mpwapwa kwenda dar. na ikumbukwe 30 july kampuni hii hii iliua zaid ya watu 20 waliokuwa wakitokea mpwapwa kwenda dar, na pia mwezi huo uliopita huko kilosa ilipata ajali. morobest ni majanga kwa huu mfululizo wa ajali
 
Moro best again! Na sababu ni ile ile mwendo kasi. Haya mabasi sasa yatazamwe kwa upana.
Poleni sana wafiwa na majeruhi
Mabasi sio tatizo. Tatizo ni watu na system. Polisi wanauza leseni class c kama njugu. Hawafikirii maafa yanayoweza tokea baadaye. Ni lazima kuwepo na control ya utoaji leseni za magari kama mabasi na malori. Tatizo lingine ni barabara. Bado highway zetu ni njia mbili kama ilivyokuwa kabla ya uhuru. Tunaambiwa pesa hakuna lakini za kuendesha bunge la katiba Feki zipo. Elimu duni nayo ni tatizo. Madereva wengine hata hizo Alama zA barabarani hawawezi soma. Mwisho njaa ya polisi wetu ni tatizo kubwa kuliko Ebola. KwA hali ilivyo sasa hivi hakuna aliye salama. Upande basi, utembee kwA miguu, uendeshe gari binafsi hiyo haitazuia kupata Ajali hapa bongo. Mungu tusaidie!
 
Duh... umenichekesha.

Yaani hatuna pesa za kujenga barabara za lami nzuri, lakini tunazo pesa za kuendesha bunge la 'kimagumashi' la mzee wa 'viwango vilivyoporomoka' Samuel Sitta?!

Hebu nikuulize swali la kizushi, hivi jumla ya posho zote ambazo wabunge wa magamba, wa bunge maalum la katiba 'weshalamba' so far, tokea ukawa wasusie bunge hilo mwezi wa 4, inaweza kuwa equivalent na kujenga kilomita ngapi vile za barabara ya lami?
 
Basi la Moro best likitokea Dodoma kwenda Dar limepata ajali mbaya sana muda huu eneo la Kibaigwa, ni mwendo kasi na imekoswa koswa na maroli na basi kabla ya kutumbukia kwenye mtaro, maiti wawili tayari wametolewa, majeruhi ni wengi mno na huenda idadi ya waliokufa ikawa kubwa zaidi, tuko katika jitihada za kunasua watu walionasa.
Picha baadae.
Mdau hii ajali ilitokea maeneo ya Kiegea,ukishapita Gairo kama unakuja Dumila,binafsi niliikuta pale,na baadhi ya maejruh tulirudi nao mpaka Njia Panda ya Kongwa,wenyewe walisema hakufa mtu, simu yangu ilipiga picha hafifu nikaona hakuna haja ya kuziweka hapa
 
Back
Top Bottom