Basi la Happy Nation lapata ajali Mikese

Basi la Happy Nation lapata ajali Mikese

Kuna Taarifa za ajali ikihusisha Basi la Kampuni ya Happy Nation usiku huu maeneo ya Mikese

Kuhusu chanzo cha ajali na hali za Abiria Taarifa kamili itatolewa baadae na mamlaka husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna member humu alikuja na uzi kuwasihi mamlaka wasitishe safari za usiku.
Alitukanwa sana hapa.

Wacha tujionee sasa.

Hiyo picha jamaa kauvaa mti, that is fatigue...alikuwa kasinzia huyo.
Kabisa
 
Kuna member humu alikuja na uzi kuwasihi mamlaka wasitishe safari za usiku.
Alitukanwa sana hapa.

Wacha tujionee sasa.

Hiyo picha jamaa kauvaa mti, that is fatigue...alikuwa kasinzia huyo.
Unataka mabasi ya mikoani yawe kama kuku, saa moja jioni ndani! Hili tukio limetokea jioni jua linazama wewe unaleta zako tena hauko nyumbani kwako.
 
Ingekuwa ni dharura ya mara moja sawa (japo nayo kwa mtu anayejali wateja wake, lugha nzuri na hata kuomba msamaha ingefaa).

Kwa hawa ni malalamiko ya kawaida...unakatiwa basi namba E (nauli kubwa) unaletewa mkangafu. Siyo fair; na wanajiharibia biashara tu.

Hata kama unafanya kazi huko waambie hivyo!
Sifanyi kazi huko hiyo ndo biashara ninayo ijua zaidi
 
Utaratibi wa Gari kutembea Usiku na madereva wetu jinsi walivyo Aiseee VIFO VITAKUWA VINGI SANAAA...!
 
Madereva wanapitia mengi sana barabarani, Mungu awasimamie. Siku nilipopata ajali na nikaangalia mazingira ya ile ajali ndio nikajua kua hakuna dereva mzembe.

Acha ujinga madereva wazembe wapo ndo chanzo cha ajali nyingi za mabasi ya mikoani. Mwendo mkali bila tafadhari ndo chanzo kikuu cha ajali. Acha kupepesa macho.
 
Biashara ya mabasi ina changaamoto laiti kama na wewe ungekua unamiliki mabasi ungeona changamoto ya biashara hii na ungekua muelewa pindi zinapotokea dharura kama hizo,.
Ni bora uende na namba C nzima kuliko namba E ambayo imepata dharura na ina hitilafu.

Biashara ya magari siyo mchezo we endeleo tu kuona gari zinapita njiani na unatukana kuwa ni magari mabovu ila nyuma yake ujue kuna mwanaume anavuja jasho siyo mchezo

Hilo sisi hatujali, mpaka umeanza hiyo biashara ulikuwa tayari ku bear the coming risks, so what we need is maximum safety for the passengers. Hizo blah blah za maintenance and operation is none of our business.
 
Ilipangwa wafe hawa raia ..... Hakuna kusingizia bus wala madereva ni mipango ya Malaika mtoa roho amewakutia kwenye bus, nyakat mwingine tuzielewe alama za nyakat
Ni mipango ya Allah...na sio malaika.

Na ni kweli kila jambo lazima liwe na sababu....na hyo sababu ni vitendo vyetu mimi na wewe,usije ukathubutu unywe sumu ufe useme mipango ya mungu...kufa utakufa pia utahukumiwa kwa kujitoa uhai...

Hzo ajali zote ni uzembe wa madereva kuamini barabara zao....hizi Barabara za bongo hazina viwango vya kimataifa za kumruhusu dereva kuendesha vile anavyojisikia bila kujiongeza...

Alpha....uzembe wa lory la mafuta gbp kuover take bila kuchukua tahadhar....na dereva wa bus kuwa speed eneo la kona na maene ya miji ya watu..

Ally's....kutokuchukua tahadhari ya kupunguza mwendo au kusimama kabisa eneo la crossing kuangalia hali ya hewa labda kutokana na mazoea....pia dereva wa kichwa cha tren kutoa piga honi kupunguza mwendo wala kuwasha taa nahisi ni hali ya mazoea...

Baraka.....nasikia brake zilifeli..

Anyway.....mwisho wa siku wote sisi tutakufa
 
Back
Top Bottom