blogger
JF-Expert Member
- Mar 13, 2012
- 13,416
- 16,789
Katoka Mwanza saa ngapi ili awe mikese mchana!??Hio sio safari ya usiku ni mchana huu, hapo mtu katoka Mwanza ndo anaingia mjini sasa
Katoka Mwanza saa ngapi ili awe mikese mchana!??Hio sio safari ya usiku ni mchana huu, hapo mtu katoka Mwanza ndo anaingia mjini sasa
Mkuu wewe ni dereva, ngoja madereva wa jf na notes zao za NIT wajeMadereva wanapitia mengi sana barabarani, Mungu awasimamie. Siku nilipopata ajali na nikaangalia mazingira ya ile ajali ndio nikajua kua hakuna dereva mzembe.
Wasitishe kwa sababu zipi? Wengine kusafiri mchana hatuweziKuna member humu alikuja na uzi kuwasihi mamlaka wasitishe safari za usiku.
Alitukanwa sana hapa.
Wacha tujionee sasa.
Hiyo picha jamaa kauvaa mti, that is fatigue...alikuwa kasinzia huyo.
Sadaka kwa bwana waoMwisho wa mwaka, ajali ni nyingi.
Biashara ya mabasi ina changaamoto laiti kama na wewe ungekua unamiliki mabasi ungeona changamoto ya biashara hii na ungekua muelewa pindi zinapotokea dharura kama hizo,.Happy Nation ni mabasi ya hovyo yanayoendeshwa hovyo hovyo tu. Ajali kwa hawa jamaa ni suala la muda tu!
Halafu wadanganyifu. Unamkatia mtu tiketi inasema basi E (jipya) linalokuja ni mkangafu namba C mpaka seat zimechakaa. Na lazima liharibike njiani.
Nadhani kampuni imekua kwa kasi na sasa wameanza kujaa kiburi na kutojali. Wataanguka wasipojiangalia! 🚮🚮🖐
Mimi sioni sababu ya haya magari kusafiri usiku. Kwa mfano mtu unaenda Moshi , masaa 8 hadi tisa umeshafika, dereva analala vizuri tu saa 12 yuko barabarani. Kiherehere tuKweli mkuu. Mtu ana safari usiki ya zaidi ya km 500, mchana kutwa anashinda anazurura, saa 2 usiku anakunywa kahawa/energy drink anaanza safari.
Ilipangwa wafe hawa raia ..... Hakuna kusingizia bus wala madereva ni mipango ya Malaika mtoa roho amewakutia kwenye bus, nyakat mwingine tuzielewe alama za nyakatDuuh....
1...Alpha-nzega
2...Baraka-uko kusini
3...Ally's-manyoni
Na hizi zote zmeondoka na watu zaidi ya 10
4..Leo tena Happy nation
Innalillah wainnailayh rajiuun
KWani akitoka mwanza ndio anatakiwa kusafiri usiku?Hio sio safari ya usiku ni mchana huu, hapo mtu katoka Mwanza ndo anaingia mjini sasa
Utetezi wako ni wa hovyo!Biashara ya mabasi ina changaamoto laiti kama na wewe ungekua unamiliki mabasi ungeona changamoto ya biashara hii na ungekua muelewa pindi zinapotokea dharura kama hizo,.
Ni bora uende na namba C nzima kuliko namba E ambayo imepata dharura na ina hitilafu.
Biashara ya magari siyo mchezo we endeleo tu kuona gari zinapita njiani na unatukana kuwa ni magari mabovu ila nyuma yake ujue kuna mwanaume anavuja jasho siyo mchezo
Hata ndege huwa zina hairisha safari, unaweza kukatiwa ticket gari namba E na asubuhi ikakataa kuwaka au ikapata hitilafu alafu gari nyingine aliyobaki nayo ni namba C lazima atakuletea hiyo hiyo upande ili ufike safari yako, sasa ulitaka afanyaje akurudishie nauli au akufaullishe kwenye gari zingine?Utetezi wako ni wa hovyo!
Hii ni biashara. Na hakuna aliyemlazimisha kuifanya. Kama ikimshinda anaacha watakuja wengine. Na kuna biashara ambayo siyo mchezo? Kwa hiyo watu wavumilie huduma mbovu na udanganyifu kisa biashara fulani "siyo mchezo?". Come on man!
Na katika biashara jaribu kila uwezalo kumridhisha mteja wako. Hata ukikosea au ukapatwa na dharula basi toa maelezo ya kueleweka na ikibidi muombe mteja wako msamaha. Jamaa wana kiburi utafikiri mmepanda bure. Siyo mtu anakuuliza kabisa wakati anakata tiketi kuwa hili basi ni jipya namba E unamjibu ndiyo na tiketi yake inaonyesha hivyo halafu unamletea basi limechoka kweli kweli. Huo sio udanganyifu katika biashara? Kwa nini tu usiseme ukweli?
Haya hilo basi C likashindwa kupanda Mlima Sekenke kidogo lirudi kinyume nyume likazimika hapo mbele tu. Abiria wakakaa hapo zaidi ya masaa matatu. Hakuna cha maelezo wala nini. Kumbe tatizo dogo tu filter mbovu. Akaja mwenzao akawapa filter mpya. Piga moto huku karibia na Dodoma basi likazima tena...
Aaaaaargh! 🚮🚮🚮
Uko sahihi mkuu, tatizo ni madereva na wasimamizi wa makampuni yao. Mf. haya basi ya saa 1 jioni Dar to Mwanza, madereva wanaamkia gereji, wakitoka hapo wanaanza misele mtaani, jioni wanakamata ndinga kuana safari.Gari inayotembea zaidi ya masaa 12, taratibu za kupewa leseni LATRA zinataka awe na dereva wawili. Madereva akili zao fyatu tu, hasahasa hawa wa ma bus.
Ingekuwa ni dharura ya mara moja sawa (japo nayo kwa mtu anayejali wateja wake, lugha nzuri na hata kuomba msamaha ingefaa).Hata ndege huwa zina hairisha safari, unaweza kukatiwa ticket gari namba E na asubuhi ikakataa kuwaka au ikapata hitilafu alafu gari nyingine aliyobaki nayo ni namba C lazima atakuletea hiyo hiyo upande ili ufike safari yako, sasa ulitaka afanyaje akurudishie nauli au akufaullishe kwenye gari zingine?