Basi la BATCO lenye namba za usajili T192DHW likiteketea kwa moto hii leo katika eneo la Kirumi kata ya Bukabwa Wilayani Butama Mkoani Mara. Gari hilo lilikuwa linafanya safari zake kutoka Tarime-Sirari na Mwanza.
Chanzo cha Moto huo bado hakijafahamika.
Taarifa za awali kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo pamoja na abiria wameeleza kuwa baadhi ya mali za abiria zimeteketea kwa moto na hakuna mtu aliyepoteza maisha.
Kuna Mdau mmoja wa Masuala ya Udereva na Usafirishaji wa Mizigo na Abiria aliwahi kuniambia kuwa siku zote ukiona ajali ya Gari au Basi ni ya Moto halafu hakuna hata Mtu mmoja ama aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha basi jua tu ya kwamba Kafara limekataa na kwamba kuna uwezekano mkubwa huyo Mlengwa ( mmiliki wa Gari / Basi hilo ) akapoteza maisha au kukatokea matatizo makubwa sana katika Familia yake ila akiwahi kufanya tambiko atajiokoa na dhahama.
Sasa ndugu zangu tunasafirig na document za muhimu au pesa nyingi na kuweka kwenye bag kisha kuviweka kwenye buti,hapo tunakuwa hatuna chetu...fundisho /tahafhar kama una nyaraka za muhimu,au mzgo mdogo wa thamani tujitahid tuwe na rasket ndogo ya kuwekea ivyo vitu na kuwa nayo karibu iyo rasket kama vile cm yako unavyoihifadhi..