Basi la Batco lawaka moto maeneo ya Mto Kirumi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,846
2,000
BAD NEWS!

Basi la BATCO lenye namba za usajili T192DHW likiteketea kwa moto hii leo katika eneo la Kirumi kata ya Bukabwa Wilayani Butama Mkoani Mara. Gari hilo lilikuwa linafanya safari zake kutoka Tarime-Sirari na Mwanza.

Chanzo cha Moto huo bado hakijafahamika.

Taarifa za awali kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo pamoja na abiria wameeleza kuwa baadhi ya mali za abiria zimeteketea kwa moto na hakuna mtu aliyepoteza maisha.

batc.jpg
batco.jpg
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,595
2,000
, tuombe radhi. Hiyo ni ajari kama nyingine mkuu

Kuna Mdau mmoja wa Masuala ya Udereva na Usafirishaji wa Mizigo na Abiria aliwahi kuniambia kuwa siku zote ukiona ajali ya Gari au Basi ni ya Moto halafu hakuna hata Mtu mmoja ama aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha basi jua tu ya kwamba Kafara limekataa na kwamba kuna uwezekano mkubwa huyo Mlengwa ( mmiliki wa Gari / Basi hilo ) akapoteza maisha au kukatokea matatizo makubwa sana katika Familia yake ila akiwahi kufanya tambiko atajiokoa na dhahama.
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
15,368
2,000
Hizo gari nzuri sana alafu kondakta ni wanawake...aisee pole yao!!


Ni kweli viwango vya huduma za usafiri route ya Sirari - Mwanza vipo juu sana hakuna mahali pa kulinganisha napo kwa hapa nchini

Abiria wote kwenye seat (No extra passenger) na hakuna kusimama hovyohovyo
 

peter palla

JF-Expert Member
Sep 4, 2015
212
250
Sasa ndugu zangu tunasafirig na document za muhimu au pesa nyingi na kuweka kwenye bag kisha kuviweka kwenye buti,hapo tunakuwa hatuna chetu...fundisho /tahafhar kama una nyaraka za muhimu,au mzgo mdogo wa thamani tujitahid tuwe na rasket ndogo ya kuwekea ivyo vitu na kuwa nayo karibu iyo rasket kama vile cm yako unavyoihifadhi..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom