GE2025 Bashungwa: Hakuna chama zaidi ya CCM chenye uzoefu wa kuongoza nchi yetu bila kuingia kwenye machafuko ya kivita

GE2025 Bashungwa: Hakuna chama zaidi ya CCM chenye uzoefu wa kuongoza nchi yetu bila kuingia kwenye machafuko ya kivita

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mgombea ubunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuendelea kuongoza Serikali bila nchi kuingia kwenye machafuko.

Bashungwa ameyasema hayo jana Oktoba 10, 2025 katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika Kijiji cha Nyakayanja, Kata ya Nyaishozi, ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu kwa kujitokeza kupiga kura za ndiyo kwa wagombea wa CCM ifikapo Oktoba 29.

“Zamu hii kina mama ni zamu yenu. Huyu ni mama mwenzenu (Samia Suluhu Hassan), naomba mumpende, tumpe ushirikiano na kura zote za kina mama ni mtaji namba moja,” amesema Bashungwa akimuombea kura mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan.

Mbali na hilo, Bashungwa pia ametumia nafasi hiyo kuomba kura kwa ajili yake kugombea ubunge wa Karagwe pamoja na mgombea udiwani wa Kata ya Nyaishozi, Wallace Mashanda.

Ameahidi kuendelea kuboresha huduma za kijamii, ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara zinazounganisha vijiji mbalimbali katika jimbo hilo ili kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi.


 
Hii nchi hata NLD wanaweza kuiongoza cha muhimu wasiziguse klabu mbili tu Simba na Yanga.
 
Huyo jamaa huwa ni mjinga mjinga fulani hivi ambae hana upeo kabisa wakuona mbali na hata kujieleza huwa ni shida.
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu. Machawa na mali zao tunaishi nao mitaani kwetu.

Ndugu watanzania, mafuta ya taa, petroli na viberiti havijawahi kuwa adimu.

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
 
Back
Top Bottom