Bashungwa CUP 2024 Kuanza Kurindima Mwezi Julai, 2024

Bashungwa CUP 2024 Kuanza Kurindima Mwezi Julai, 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,429

BASHUNGWA CUP 2024 KUANZA KURINDIMA MWEZI JULAI, 2024

Mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la "BASHUNGWA CUP 2024" yataanza kurindima mwanzoni mwa mwezi Julai 2024 katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika kwa miezi miwili yatazinduliwa kata ya Iguruwa yakihusisha timu 77 kutoka vijiji 77 vya Halmashauri hiyo ambavyo vitaunda timu 23 kutoka kata 23 za jimbo hilo.

Akitoa maelezo ya awali wakati akikabidhi mipira 77 kwa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo kwa niaba ya mbunge wa Jimbo la Karagwe, katibu wa Mbunge wa Jimbo la Karagwe Ndg Ivo Ndisanye amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa na lengo mahususi ambalo ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 inayobainisha umuhimu wa michezo.

Ameyataja malengo mengine katika mashindano hayo kuwa ni kuimarisha afya kwa vijana, Kusaka vipaji na kuviendeleza kwa kuunda timu ya Halmashauri itakayoshiriki katika ligi mbalimbali ndani na nje ya wilaya ya Karagwe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mashindano hayo Anastazia Amani ambaye pia ni Katibu wa Wazazi Wilaya ya Karagwe, amesema kuwa jambo hilo ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo kwani mashindano hayo yatatoa fursa ya serikali kueleza mafanikio ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa serikali inafanya kazi kubwa ikiwemo uimarishaji wa miradi ya maji, miundombinu, elimu, afya na uwekezaji hivyo michezo ni sehemu ya fursa muhimu kuwakutanisha pamoja wananchi na kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM.

MWISHO
 

Attachments

  • 1718386320233063-0.jpg
    1718386320233063-0.jpg
    1.8 MB · Views: 7
  • 1718386312437588-1.jpg
    1718386312437588-1.jpg
    2.2 MB · Views: 7
  • 1718386304944822-2.jpg
    1718386304944822-2.jpg
    1.7 MB · Views: 7
  • 1718386295855773-3.jpg
    1718386295855773-3.jpg
    2.1 MB · Views: 8
  • 1718386287254408-4.jpg
    1718386287254408-4.jpg
    2.5 MB · Views: 7
  • 1718386275638489-5.jpg
    1718386275638489-5.jpg
    2.4 MB · Views: 8
Sasa nimeanza kuelewa kwa nini deni la taifa linakimbilia haraka trilioni 100 (100,000,000,000,000!!!) huku thamani ya shilingi na hali ya maisha ya Watanzania vinaporomoka kwa kasi, licha ya mikopo lukuki, makusanyo mengi ya tozo na kodi na bajeti kubwa.
 
Hayo mashindano jamaa huyafanya kila mwaka nadhani hata mwakani atafanya ni utaratibu wake!

Nimewahi kuona clip fulani huko nyuma akikabidhi kombe Kwa washindi!
 
Back
Top Bottom