iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Naona Startv wameamua kutakatisha habari/taarifa na kupitia kufanya hayo,wanaitumia studio yao kama "washroom" kwa ajenda wanayoijua wenyewe.
Wameamua kutumia waandishi wao kujitahidi kubadili na kudhibiti maoni ya umma ambao muda mfupi uliopita umeshudia watu karibu elfu kumi wakifutwa kazi na wao wameamua kusimama na mtu mmoja mwenye tuhuma za vyeti feki,wanajaribu kutengeneza shujaa na kuuaminisha umma kwamba japo naye ana feki lakini yeye ni shujaa zaidi kuliko waliofutwa kazi,hivyo aaminike japo ana feki,wanamtakatisha!
Tunajua propaganda si jambo baya,bali limekuwa likitumika vibaya tu,tangu enzi na enzi propaganda zipo! Hata Hittler naye alikuwa na Joseph Goebbels kama waziri aliyehusika na habari pamoja na propaganda,Al Sahhaf naye alikuwa mpiga propaganda wa Saddam Hussein na kimsingi kila mahali kuna propaganda
Mwandishi wa habari anapofanya propaganda huwa anafanya "news management"," spinning" akiwa na lengo la kutoa habari chanya tu kuhusu mtu au kitu alichokilenga na kuondoa habari zile mbayambaya,hata yule mgeni aliyemfikia ROMA ofisi za pale habari Maelezo baada ya kutekwa,ilikuwa ni mkakati wa kudhibiti habari na taarifa,STARTV wameamua kufanya news management kwa MTEJA wao na hawataongelea yale anayotuhumiwa.
Propaganda ili ifanikiwe lazima iwe imekusudiwa,iwe kimpangilio na yenye lengo maalum kwa mtoa propaganda .....hapa star TV wanaonekana kufanya makusudi na tayari walishafanya mpangilio na mkakati kwa kusambaza vipeperushi kila mahali wanakoweza na inawezekana hata wameshafanya vikao vya awali na anayetarajiwa kuhojiwa kujua anataka "atakatishwe" wapi has a.
Propaganda ni mchezo wa kuchezea akili za watu (kwa tafsiri mbaya kutokana na inavyotumika....)ndio maana wengi huifananisha na ulaghai,uongo,upotoshaji,brainwashing,na mengineyo.
Propaganda ni stage ya juu sana ya uongo inayoandaliwa kwa umakini mkubwa,hongereni STARTV kwq maandilizi makubwa ya uongo,uzandiki,upotoshaji na ulaghai na utakatishaji habari na taarifa