Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
OMAR BASHIR ASEMA MAANDAMANO HAYATAMTOA KWENYE UTAWALA
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amesema kuwa maandamano ambayo yanaendelea kuikumba Sudan kwa karibu mwezi mmoja hayatamuondoa kwenye utawala wake wa karibu miongo 3
Ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara wa wafuasi wake katika mji wa Darfur, Magharibi mwa Sudan
Alinukuliwa akisema, "Maandamano haya hayatasababisha mabadiliko ya utawala. Kuna njia moja tu ya utawala, na njia hiyo ni uchaguzi. Wananchi wa Sudan wanatarajia kupiga kura mnamo mwaka 2020 kuamua rais wao mpya," amesema Bashir
Maandamano ya sasa nchini Sudan yalianza tarehe 19 Desemba mwaka 2018 kufuatia uamuzi wa Serikali ya kuongeza mara tatu bei ya mkate.
Sw.rfi.fr