Bashe unahujumiwa CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bashe unahujumiwa CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Sep 27, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Harakati za Bashe kisiasa ndani ya CCM zinakabiliana na vikwazo vingi.

  Baadhi ya vichache na vilivyoathiri maisha yake kisiasa ni kama vifuatavyo:

  1. Ndani ya UVCCM anakabiliwa na upinzani kila kona na hivyo kuhatarisha nafasi yake kiuongozi!
  2. Madai ya kutokuwa raia wa Tanzania ambayo hadi sasa ufumbuzi wake unatia shaka. Hii ilipelekea kuenguliwa katika kugombea ubunge kupitia CCM pamoja na kushika nafasi ya kwanza katika kura za maoni na badala yake akateuliwa hasimu wake mkubwa kisiasa Bw. Kingwangwalla ambaye alishika nafasi ya tatu katika kura za maoni!
  3. Kuzuiliwa na hasimu wake mkubwa Bw. Kingwangwalla kurudisha fomu ya kugombea ujumbe wa NEC (CCM) kwa madai kuwa muda wa kurudisha fomu ulikwisha!
  4. Kutishiwa bastola na hasimu wake mkubwa Bw. Kingwangwalla, kitu ambacho si cha kawaida kwa watu walio chama kimoja!

  Maswali ya kujiuliza hapa ni:

  1. Je Kingwangwalla anatumwa kumhujumu Bashe na wakubwa wake kichama?
  2. Je Kingwangwalla anatumiwa na vigogo na kwa lengo na manufaa gani ?
  3. Je Kingwangwalla alikuwa time keeper wakati wa kurudisha fomu?
  4. Je Kingwangwalla hastahili kuchukuliwa hatua kichama kwa kumtishia Bashe kwa bastola?
   
 2. m

  malaka JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ngumi za walevi. Mmoja anarusha ngumi anadondoka mwingine anakwepa anadondoka. Hahaha raha sana.
   
 3. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwani chama kiko kimoja? Bashe naye atumie akili kidogo, alipoanzisha vita na mtoto wa Raisi haya ndiyo matunda yake.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ileje, mimi nilidhani hii ni thread kimhusu Bashe kuhujumiwa CCM!. Kwa taarifa yako, hakuna hujuma yoyote, hayo uliyotaja ni "zengwe" tuu!.

  Kumbe hata la kumtisha mtu bastola ni kosa la kuchukuliwa hatua kichama?. Kumbe bado tuna watu humu ambao bado wanaamini CCM ni chama dola!.

  Safari ya ukombozi wa kifikra ni ngumu kuliko inavyo dhaniwa!.

  P.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Pasco

  CCM inapaswa kuchukua hatua ili kuonyesha kutopendezwa na kitendo hicho! CCM kuendelea kukaa kimya bila kuchukua hatua na ukizingatia kuwa ni chama tawala kunaweza kuvifanya vyombo vya dola kutofanya kazi zao kwa uhuru!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. piper

  piper JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naona ni mambo ya mbwa kala mbwa
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mbona kwa maelezo yako hapa unaongelea vyama viwili vyenye jina moja.
   
 8. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mawazo yako yapelekwe kwa TENDWA ili afute hicho chama ambacho viongozi wake wanahatarisha maisha ya wenzao, au hilo hajaliona ili awaite wanahabari atangaze nia ya kuifuta CCM? Kama ushahidi hautoshi kuna ile sakata ya ADEN RAGE pale Igunga na Mguu wa kuku kiunoni.
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  I love SSM!! Long live!!! Watatupiana makonde weeee!!! Ila kwa Bashe kwa ushauri mdogo tu ni hivi kwa kuwa alikuwa na tifu na mtoto wa mfalme hakuna namna yoyote ile atapata cheo SSM kama kambi ya mtoto wa mfalme itakuwa inashika hatamu!!! Apumzike tu hadi ile kambi nyingine itakaposhika hatamu if at all hakuna kuwa chama cha upinzani 2015. Again viva SSM!!
   
 10. m

  multmandalin JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 8, 2012
  Messages: 1,951
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Unajuwa Mwalimu alipokemea ukaburu ndani ya Tanzania hakumaanisha kuwakubali watu kama Bashe!
  Mabarabara yako mengi aende huko akafanye uhuni wake! Unapokuwa kiongozi lazima ujiheshimu sio unaishi kihunihuni.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi ni lazima Bashe awe kiongozi ndio aweze kutoa mchango wake kwa maendeleo ya taifa?
   
 12. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  huyu awe mtu wa kusubili ufalme mwingine kama anafaa, au aende CUF
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Hussein Bashe kayataka mwenyewe, anakuwa king'ang'anizi kama kupe bana!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. i

  iseesa JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si inasemekana kuwa wote (Bashe na Kigangala) si WABONGO? Sa' kwa nini wanakuja kugombania huku kwetu?!!
   
 15. m

  multmandalin JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 8, 2012
  Messages: 1,951
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Aende akaendeshe shamba lake huko!
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hivi what is so special about uraia wa Tanzania?

  Mbona mtu yeyote akizaliwa USA au UK swala la uraia linakuwa halina utata kabisa.
   
 17. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,536
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Dah maswali yako ya msingi sana mkuu,nilitegemea Bashe kama hatendewi haki angefaili malalamiko yake katika kamati husika ili haki itendeke,aidha kama wakati wa vetting kwenye chama sijui kama huwaga wanatoa maelezo kama sababu za kuenguliwa,kama yapo basi anajua tatizo liko wapi na afanye nini ili wakati mwingine afanikiwe.Na zaidi maisha siyo lazima uwe mwanasiasa akiona siasa chafu awezi anakaa pembeni au apigane kuyapata mabadiliko anayoyataka ndani ya chama.
   
 18. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Bashe arudi kwao Mogadishu watanzania hawamtaki
   
 19. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,536
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Mkuu acha kumdanganya,siku akitangaza kuhama ccm wiki haiishi utasikia uhamiaji wanawashikilia familia kadhaa kwa kosa la kuishi nchini kinyume cha sheria,achana na siasa zetu hizi tunaziweza wenyewe mtu unalishwa sumu afu unapewa uwaziri ili usubirishie kifo!
   
 20. k

  kilaboy Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 25
  Makundi ndicho kikubwa kinachoiangamiza CCM
   
Loading...