Bashe aonya: Ya Zambia yanaweza kutokea Tanzania 2015!

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,080
MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe, ameonya kuwa iwapo CCM hakitajadili matatizo ya wananchi sasa, kitarajie kupoteza dola mwaka 2015, kama ilivyotokea kwa chama tawala Zambia.

Akizungumza katika Kata ya Kasamwa wilayani Geita katika maadhimisho ya miaka 33 ya kuanzishwa kwa UVCCM, Bashe alisema kuwa uchaguzi wa Zambia umemalizika na chama kilichoongoza kwa zaidi ya miaka 20 kimeondolewa madarakani, tukio linalopaswa kuwa funzo kwa CCM.

Alisema katika mazingira ya sasa ambayo wapiga kura wengi ni vijana, CCM kinapaswa kuwasikiliza, kujadili matatizo yao na kuyapatia ufumbuzi, vinginevyo kitang'oka madarakani muda mfupi ujao.

“CCM kianze kujiandaa leo kwa kutoa majibu ya matatizo ya vijana kinaowaongoza ikiwa ni pamoja na viongozi wake kuepuka kukaa ofisini na umangimeza kwani bila hivyo, mwaka 2015 wataanza kutafuta mchawi,” alisema Bashe na kuendelea:

“Kiache kutafuta mchawi mmoja mmoja, kiache kujadili watu kijadili matatizo ya watu tujadili watu wanapata wapi maji, watu wanapata wapi ajira, wanapata wapi zahanati na fedha zinazotengwa katika halmashauri ya wilaya kwenda kwa wananchi zinawafikia... haya ndiyo mambo ya msingi kabisa kama yakifanyiwa kazi CCM kitaendelea kushika dola.”

Alisema wakati UVCCM leo ukisherehekea miaka 33 tangu kuanzishwa kwake, viongozi wanatakiwa kujiuliza ni kwa nini watu wengi hawajaichagua CCM na ni vipi vijana wengi ndiyo wanaoonekana hawataki kuiunga mkono CCM. Alisema hii ndiyo changamoto kubwa inayokikabili chama hicho tawala kwa sasa.

Bashe alisema vijana wa Tanzania leo watapenda CCM kama tu kitawahakikisha elimu bora, afya bora, fursa ya kufanya kazi na kujiajiri na uchumi ulio imara.

“Taifa linakwenda kwenye uchaguzi mwaka 2015, kipindi hicho kitakuwa na wapiga kura wapya zaidi ya milioni sita ambao wengi watakuwa ni wale wenye umri wa miaka 30. Vijana hawajui habari za uhuru na amani wala nini, wanataka kusikia wamepata zahanati, elimu bora na wamepata fursa za kufanya kazi basi, hapo ndipo chama kitakuwa kimejibu matatizo yao.”

Alisema CCM ya leo siyo ile ya miaka 10 iliyopita na kwamba ndani yake kumejaa migawanyiko mingi aliyoieleza kuwa haina maslahi kwa watu wanaowaongoza huku, akisema kumejaa mizengwe mingi na matokeo yake watu wamekuwa wakikimbilia upinzani.

“Lazima tujiulize maswali kulikoni hali hii? Lakini majibu tunayo ni kwa sababu UVCCM imeshindwa kufikia mahitaji ya vijana wengi na sasa wanakichukia chama hiki.”

Alisema vijana wengi wamezaliwa na kukua na kuukuta uhuru ambao leo, unasherehekewa na taifa kutimiza miaka 50. Wakati huo vijana wa CCM nao wakisherehekea miaka 33 ya kuzaliwa umoja wao, uhuru huo umetokana jitihada binafsi za wazee na vijana wa wakati ule, vijana wa sasa hawana habari na uhuru.

“Nimeambiwa CCM tulishindwa uchaguzi katika Kata ya Kasamwa tuliyopo ambayo tunaadhimisha miaka 33 ya umoja wetu. Kata ipo chini ya Chadema na nimeambiwa hapa kumewahi kutokea vurugu. Labda niseme jambo moja kuwaambia Kasamwa uamuzi mlioyafanya wa kuchagua kutoka Chadema ni wenu na ndiyo demokrasia. Mmempa udiwani mbaye hatokani na CCM, lakini niwaombe tofauti za kisiasa zisiwagawe kufikia hatua ya kushambuliana.”

“Nilipata taarifa kwamba mlifikia hatua ya kuchomeana nyumba hapa Kasamwa. Niwaombe vijana wenzangu haya maslahi ya kisiasa yasitugawe vijana wenzangu, tutofautiane kwa sera na itikadi, lakini tusivurugane, haisaidii mtu yeyote ikitokea vurugu hapa na vijana ndiyo watakuwa wa kwanza kuathirika.”

Alisema viongozi wa UVCCM wanapaswa kuepuka ‘Ndiyo mzee’ bali kuhakikisha wanazibana halmashauri za wilaya zifanye kazi ambayo itasaidia kuleta maendeleo kwa wananchi na vijana kwa ujumla na alionya kuwa CCM kinapaswa kuhakikisha kuwa maeneo yaliyochukuliwa na upinzani hayaachwi kwa kuhakikisha kinafikisha maendeleo.
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,636
116,789
Bashe ana hasira sana baadhi ya viongozi wa CCM.

Kila analolisema kuhusu CCM anawalenga maadui wake na maadui bosi wake walioko ndani ya CCM.
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,531
5,357
Nadhani it is late. CCM kimeshaamua kutumikia matajiri na wawekezaji. Waache walalie kitanda walichojitandikia.
 

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,224
3,085
nimefuatilia kwa karibu jamaa namna anavyotoa hoja zake hua anazungum zia uhalisia walengwa hawapaswi kubeza anachosema!
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Huyu nae si ana kundi lake ndani ya ccm?. Ila ametoa pointi.
 

Baiskeli

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
336
61
ccm inautaratibu wa matundu mawili, ya moja linapokea jingine linatoa hawashauriki hawa. jamaa kaongea fact kwa faida ya chama yao bt sikia mabosi wake watakavyo react.
 

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,335
5,509
Kimsingi jamaa ametoa ushauri mzuri kwa chama chake. Ila ninamambo mawili ninayoweza kuzungumzia kutokana na ushauri wake.

1. Ana historia ya kusukumwa na siasa za makundi kwenye chama chake pa1 na hasira ya kupokwa nafasi ya kugombea ubunge. Hii inatupa mashaka ya kujiuliza kama anamaanisha anachokinena au ni mashambulizi kwa makundi wanayohasimiana. Hapo mashaka yanazidi matumaini!

2. Ushauri wake kwenye chama umechelewa sana hasa ukizingatia kwamba ccm ni kama mgonjwa aliyerudishwa nyumbani! Hakuna tiba tena. Inasubiri kifo tu. Ameshapewa kila dawa (ushauri?) lakini haiponi. Kwa kifupi tunajipanga na maisha yetu baada ya ccm kuanguka! Nadhani ushauri ungeifaa zaidi chama kinachotarajia ku"succeed" ccm ili nchi istawi. Kuishauri au kuisaidia ccm ni sawa kabisa na kwenda kucheza bao au draft kwa maana ya kupoteza muda!
 

Bakeza

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
348
191
Pamoja na makundi alionayo lakin katoa point za msingi. My take mbona malaria sugu, rejao, mwita25, na wenzao hawachangii kulikoni?
 

Bei Mbaya

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
2,262
837
zambia's rupiah banda farewell letter:

i have called this press conference to say a few words. The election campaign of 2011 is over. The people of zambia have spoken and we must all listen. Some will be happy with what they have heard, others will not.

the time now is for maturity, for composure and for compassion. To the victors, i say this: You have the right to celebrate but do so with a magnanimous heart. enjoy the hour but remember that a term of government is for years.

Remember that the next election will judge you also.


treat those who you have vanquished with the respect and humility that you would expect in your own hour of defeat.

I know that all zambians will expect such behaviour and i hope it will be delivered. speaking for myself and my party, we will accept the results. We are a democratic party and we know no other way.

It is not for us to deny the zambian people. We never rigged, we never cheated, we never knowingly abused state funds. We simply did what we thought was best for zambia. I hope the next government will act likewise in years to come.

Zambia deserves a decent democratic process. Indeed, zambia must build on her past victories. Our independence was hard won, our democracy secured with blood.

Zambia must not go backwards, we must all face the future and go forward as one nation. Not to do so would dishonour our history.

To my party, to the mmd candidates who did not win, the lesson is simple. Next time we must try harder.

We fought a good campaign. It was disciplined. I still believe we had a good message and we reached every part of the country.

We travelled to all nine provinces and we spoke to all zambians. To those who worked every hour of the day, i say ‘thank you'. You have done your best. But, sadly, sometimes our best is not good enough.

Do not be disheartened. The mmd will be back. we must all face the reality that sometimes it is time for change. Since 1991, the mmd has been in power. I believe we have done a good job on behalf of all zambians.

Frederick chiluba led us to a genuine multi-party state and introduced the private sector to our key industries. Zambia was liberated by an mmd ideal but maybe we became complacent with our ideals. maybe we did not listen, maybe we did not hear.

did we become grey and lacking in ideas? Did we lose momentum? our duty now is to go away and reflect on any mistakes we may have made and learn from them. If we do not, we do not deserve to contest power again.

the zambia we know today was built by an mmd government. We know our place in history and we know that we can come back to lead again in the future. A new leadership will be chosen, and that leadership will be from the younger generation.

My generation -- the generation of the independence struggle -- must now give way to new ideas; ideas for the 21stcentury. from this defeat, a new, younger mmd will be re-born. if i can serve that re-building, then i will.

I must thank my cabinet for delivering on our promises. We did a lot of good for zambia. Many of our projects will blossom into bright flowers. Some of you will be back to serve zambia again – i know you will do your best for your party and for your country.

To the civil servants and government officials, it has been a privilege to serve with you. We have worked many long hours together. We did it not for ourselves but for zambia. serve your next masters as you did me, and zambia will be in good hands.

I must thank my family and my wife. They have stood by me and i cannot ask for more loyalty than that which they have displayed. I love you all dearly and i will always be in your debt.

Being president is hard work, it takes long hours of work. And because of it, i have not always been there for you. Yet, still you were there for me.

Words cannot express the depth of my love for you all. All i ask is that my family continues to serve zambia as i have sought to do.

But my greatest thanks must go to the zambian people. We may be a small country on the middle of africa but we are a great nation. Serving you has been a pleasure and an honour. I wish i could have done more, i wish i had more time to give.

Our potential is great. Our resources are impressive.

I urge you all now to rally behind your new president.

Yes, we may have different ideas but we both want the same thing – a better zambia.

Now is not the time for violence and retribution.

Now is the time to unite and build tomorrow's zambia together. Only by working together can we achieve a more prosperous zambia.

In my years of retirement, i hope to watch zambia grow. I genuinely want zambia to flourish. We should all want zambia to flourish. So, i congratulate michael sata on his victory.

i have no ill feeling in my heart, there is no malice in my words. I wish him well in his years as president.

i pray his policies will bear fruit.

but now it is time for me to step aside. Now is the time for a new leader. My time is done. It is time for me to say ‘good bye'.

May god watch over the zambian people and may he bless our beautiful nation.

I thank you.


 

Said Bagaile

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
686
255
Bashe is running very fast but it is so unfortunate that he is running at a wrong track. All he has said are but Time barred.
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Ni vigumu sana kuamini maneno ya mwana-ccm. Nasema hivi kwa sababu historically wapo watu (ccm) ambao wamekuwa wanaongea maneno ya maana kabisa na kueleza mikakati ya kupambana na maisha magumu kwa watanzania lakini mara wanapoingia kwenye safu ya uongozi ndani ya ccm wanakuwa kama wamenywesha dawa ya kuwatoa fahamu.

Hivi nani asiyekumkumbuka Nape Nnauye kabla hajawa kwenye hii safu ya NEC? Na kwa wale wasiojua, Mama Magreth Sitta kabla ya 2005 aliuiwa Rais wa chama cha waalim na alikuwa mpiga debe mzuri mno wa kutetea haki za waalim, leo hii yuko wapi? au alipopewa wizara ya elimu soon after 2005 elections aliondoa kero ngapi za waalim?

Sina shaka hata kidogo kwamba leo hii Bashe akipata cheo kikubwa huko ccm atakuwa excatly like the rest of them! Kama kweli Bashe na wenziwe wa aina yake wanaona CCM inapelea nchi siko basi wangijiengua na kuungana na wale wanaoona wanaipeleka nchi kwenye mstari ulio sahihi. Haya makelele anayopiga kila siku ni kutusumbua sisi wananchi.

Tunajuwa matatizo yetu, na tunajuwa ccm ndio wametusababishia haya matatizo, Bashe hana historia ya historia ya upambanaji zaidi ya hizi ngonjera za kila siku. No one owns this country, ccm hawana haki ya kuendelea kutawala maana hawana jipya, they have expired kabisa and if I had my way neno ccm lingepigwa marufuku kabisa kwenye katiba ya nchi hii. Marufuku kuwa na chama (hata cha wauza vitunguu) kinachoitwa ccm - Nightmares!
 

makwimoge

JF-Expert Member
Apr 14, 2011
298
41
Bashe huyo hana lolote, anachokisema hakihitaji elimu yeyote kukichambua,CCM si lolote kwa sasa naye analijua.anachofanya ni kama kurudia kusema mambo yaliyopo kwa ajili ya kutafuta umaarufu.si chochote huyo asijifanye anatoa unabii wakati alama za nyakati zimekwisha onekana
 

Mzee Madoshi

Senior Member
Feb 16, 2011
134
41
Kusema tunasema sana, lakini je matendo yetu yanaendana na yale tusemayo? Je Chama cha ndugu Bashe kinaweza kukidhi mahitaji ya wananchi iwapo hakitakuwa na ujasiri wa kuwasema na kuwafukuzilia mbali viongozi wabovu wanaoangalia zaidi matumbo yao na ya wale wanaowapigia filimbi? Hapa kuna kazi kweli kweli
 

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
729
Huyu jamaa ana point lakini anasukumwa zaidi na hasira alivyofanyiziwa na magamba wenzake.
 

Typical Tz

Member
Sep 13, 2011
45
4
Hivi watanzania watawaliwa tufanye nini? Kwa nini matatizo ya watanzania yanageuka-dili kwa kuyazungumza tu bila utekelezaji? maana kila kukicha viongozi wa chama na serikali wanayazungumza lakini hakuna dalili ya matumaini ya unafuu wa maisha kwa mtz wa kawaida.

Watu wanajitahidi kufanya kazi, wanalipa kodi lakini inawanufaisha wachache! Hivi Nchi hii ni ya watu wachache, kama ni hivyo tuigawe basi!.....
Tunakosea wapi watanzania?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom