Bashe anusurika kutekwa

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu, alisema Bashe na kuongeza:

Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa, alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013, alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu
 
Ni kweli? Nchi gani hii?
 
Hii Tz sasa inaendelea kuwa nchi yenye kuleta hofu nyingi juu ya usalama wa raia. Maana kwa sasa kila raia ana taharuki kubwa na usalama wa maisha yake. Nchi imejaa rushwa, watu masikini, udini, ukabila na sasa linaongezeka ugaidi. Maana hata ukiripoti polisi hakuna reaction yoyote hasa kwa mipango ambayo inaratibiwa na serikali au watu wenye nguvu kubwa ya kifedha na ushawishi mkubwa serikalini.
 

Hapo kwenye blue, labda uniambie kwamba umetoka shimoni leo hii lakini kama wewe unaishi hapa duniani utakuwa unaelewa kwamba hiki kitu kipo dunia nzima. Mimi nadhani badala ya kulalamika ungeutumia muda huu kufikiria namna ya wewe pia kuwa mtu mwenye nguvu kubwa ya kifedha na ushawishi mkubwa serikalini.
 
Hayo ndiyo MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA aliyotuahid kikwete na ccm yake.
 
hii stori mbona ipo kama imechonwa vile. muda wote ufuatiliwe halafu ushindwe kutoa taarifa polisi. ina maana Bashe hana contact za watu ambao wangeweza kujua hiyo noah wakati anaelekea kwake. maanake isije ikawa ni alibi ya kutaka huruma ya watu. lazima hii taarifa tuipokee kwa tahadhari kubwa. la mwisho kwani Bashe yeye mbaya wake si mmoja tuu na anamfahamu na alikwishamtaja kule Dodoma labda angempigia simu na kumuuliza vipi mzee.
 
Polisi hawa hawa wanaong'oa watu meno bila ganzi na kunyofoa kucha kwa koleo ndo hawa hawa wanatoa RB na ni hawa hawa wanakuja kujichunguza baadae. We are finished!!!!!!!!!!!!!!
 
Operesheni ng'oa kucha, meno na macho bila ganzi inaendelea. Je ni nani yuko nyuma ya matukio haya?
Sidhani kama bwana mdogo Kigwangala ana maujuzi haya.
Uraia wa Bashe nao uko mashakani licha ya kuwa Uhamiaji ilisha tusadikisha kuwa Bashe ni raia halali wa Tz
 
Sasa wanamshikilia Lwakatare wanini ikiwa wanamuachia akafanye ugaidi mtaani!!!??

Yaani hapa Polisi onyesheni umahili wenu sasa tuwaone, KAMATA MWIGURU TIA NG'OA MENO NA KUCHA AWAAMBIE ANAOWATUMA!!!!
 

Sina uhakika kama hoja yako ina mantiki yoyote!
 
Au ile Vita na Mzee wa ndoto bado wanawindana na kulipana visasi?urais 2015 tutakimbiana hapa nchini na kuuaana!
 
Magamba wanawindana wenyewe
 
Unamaanisha Joka la mdimu ndio atakua kapanga hii kitu??
Tena Nasikia yule Mzee ni Shushushu hatari!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…