Bashe: Afrika haihitaji kusaidiwa bali ipewe Haki yake

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Afrika haihitaji kusaidiwa. Afrika inahitaji kupewa haki yake kwenye keki ya dunia ili tuweze kutumia rasilimali pamoja na kuleta maendeleo ya nchi yetu. Muda mwingi kumekuwa na lugha ‘jinsi gani tutawasaidia wakulima wadogo.' Wakulima wadogo wa Afrika hawahitaji msaada, wanahitaji kupata mgao wao sahihi wa rasilimali za kimataifa.

--

My Take
Baada ya Rais Samia 2030 Bashe ndio Anafaa Awe Rais wa Tanzania,tutafika mbali.
 
kuwa na Rais with below 60yrs itakua disaster hakuna kazi ya Maendeleo itafanyika bali ni siasa tu....
 
Yeye anataka mgao wa keki ya dunia! Mbona mgao wa keki ya Taifa miaka nenda wanafaidi wachache? Au ndiyo mtu ukishiba na kuvimbiwa, na akili nazo zinadumaa!!
Kuna waziri wa kilimo au Rais anegawa keki ya Tanzania kwa makusudio kabisa ya kutajirisha vijana na wakulima wa Tanzania zaidi ya Bashe na mama Samia? Sijawahi kuona mfano kabla, hapa Tanzania.

Unaelewa anachokifanya Bashe kwenye kilimo Tanzania kwa sasa hivi?
 
Tanzania inahitaji Mapinduzi ya Kilimo ili hicho kilimo kilete tija kwa wananchi walio wengi, na pia Taifa kwa ujumla.

Kuwakusanya vijana 200 pekee, kati ya vijana let us say milioni 30 na kuwapa mafunzo ya kilimo ya miezi 3! Sidhani kama hayo ndiyo mafanikio.

Serikali ikigeuze kilimo kuwa rahisi kwa wananchi! Ihamasishe ugunduzi wa mashine mbalimbali, iwatafutie wakulima masoko ya uhakika ya kuuzia bidhaa zao(ndani na nje ya nchi), kilimo kiwe ni cha kisasa kabisa! Na siyo hiki cha kupinda mgongo, nk
 
Usiseme uongo. BBT ni zaidi ya kuchukuwa vijana, ni mpango unaogusa kila sehemu ya kilimo Tanzania kwa vitendo na watu kuwezeshwa.

Hao vijana unaosema siyo 200, ni 1,200 ni batch ya kwanza tu tena wameshamaliza mafunzo ya awali sasa hivi wanafanyiwa "monitoring and evaluation"ya walichofundishwa kwenyemkilimo.

Hapo bado hujasema wale wa ufugaji na wa uvuvi. Jionee combination hiyo:

1694178915583.png
 
View attachment 2743257
Monitoring and evaluation wanafanyiwa wakiwa wapi?
 
Sasa mtu kama Bashe atakuwa na muktadha gani kwa mfano!! Kwanza mipango na mikakati yake mingi imekaa ki utopia!!

Anachotakiwa ni kufanya mapinduzi ya kilimo ili kilete tija kwa wananchi walio wengi. Mambo ya kuanza kulia lia na kutafuta visingizio, ni dalili mojawapo ya kushindwa.
Wivu
 
Usiseme uongo. BBT ni zaidi ya kuchukuwa vijana, ni mpango unaogusa kila sehemu ya kilimo Tanzania kwa vitendo na watu kuwezeshwa.

Hao vijana unaosema siyo 200, ni 1,200 ni batch ya kwanza tu tena wameshamaliza mafunzo ya awali sasa hivi wanafanyiwa "monitoring and evaluation"ya walichofundishwa kwenyemkilimo.

Hapo bado hujasema wale wa ufugaji na wa uvuvi. Jionee combination hiyo:

View attachment 2743257
Bado hiyo idadi ya vijana 1200 pekee, ni ndogo ukilinganisha idadi ya Watanzania wote nchini ambao hawana ajira/wamejiajiri kwenye kilimo.
Na bado hujanishawishi huo mpango kuwagusa vijana pekee, na wakati sekta ya kilimo ni uti wa mgongo wa Watanzania zaidi ya 70%+

Ushauri wangu kwake; aje na mpango mkakati wa muda mrefu, na ambao utaleta mapinduzi ya kilimo nchini. Mapinduzi hayo ya kilimo, ndiyo yatakayo tutoa kwenye hiki kilimo chetu cha mazoea cha sasa! Na ambacho kinachukiwa na Watanzania walio wengi! Nikiwemo mimi hapa Tate Mkuu!

Maana ni kilimo kinacho tegemea mvua pekee, gharama zake za uendeshaji ni kubwa ukilinganisha na mavuno, njia zinazotumika kwenye uzalishaji ni duni! Hakuna ruzuku ya kueleweka kutoka serikalini, nk.
 
Hao ilikuwa batch ya mwanzo tu.

Wanaofuzu hapo na wao kufundisha idadi kubwa zaidi.

Hii kazi endelevu, siyo ya betting hii kijana.
 
Afrika haihitaji kusaidiwa. Afrika inahitaji kupewa haki yake kwenye keki ya dunia ili tuweze kutumia rasilimali pamoja na kuleta maendeleo ya nchi yetu. Muda mwingi kumekuwa na lugha ‘jinsi gani tutawasaidia wakulima wadogo.' Wakulima wadogo wa Afrika hawahitaji msaada, wanahitaji kupata mgao wao sahihi wa rasilimali za kimataifa.
Kabla hajaongelea mataifa ya mbali kuhujumu Africa aongelee yeye na genge lake kuhujumu wakulima (mazao yakiwa mengi uzeni mnapotaka wala bila kuwasaidia kuwatafutia soko - hence mengi kuozea mashambani; yakiwa machache hakuna kuuza sijui mpaka vibali n.k.)

Awamu hii imejikita kwenye ngonjera kuliko vitendo; Just talking the talk rather than walking the walk...
 
Wewe mwenyewe umeelewa ulichokiandika?
 
Wewe mwenyewe umeelewa ulichokiandika?
Ungekuwa umetumia vema rasilimali muda kama huo muda wa kuandika ulichoandika ungeuliza ambacho haujaelewa.... Anyway labda wewe una muda wa kupoteza....
 
Imebidi nicheke Kwanza
Tanzania ilishakuwa na slogan nyingi Sana Kwa kila Rais anaeingia madarakani kupitia chama cha mapinduzi
Ila slogan ilonikosha ni moja tuu

"KILIMO KWANZA ;

Mtoto wa mkulima akiwa namba tatu wa nchi nilikiona sasa kwenye kilimo tunatoboa kumbe ni danganya toto
Leo kila uchao ni matamko so sishangai wananchi kulima kilimo Kwa ajili ya chakula cha watoto tuu

Jambo dogo tuu angalia machinga na bodaboda ambao wamekuwa ni sehemu ya wapiga Kura wa chama tawala na wamekuwa mitaji yao yote haya ni kidharau au kuwa na Sera mbovu za kilimo

Halafu mtu anakuja kukuambia kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa kweli ? Inangia akilini

Pamoja na majirani zetu kututegemea bado watanzania tunalima chakula Kwa ajili ya familia zetu pekee na hilo halina ubishi

Hao wachache wana export Kwa Tz hawafiki hata 2%ya watz
Wizara kuna jambo zaidi ya kufufua kilimo

NB mwenyewe mm ni mkulima naelewa
 
Back
Top Bottom