BASATA: Tunamtafuta Ben Pol atueleze kuhusu zile picha za nusu utupu

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,536
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA, Godfrey Mngereza amelaani picha za nusu za utupu za msanii wa muziki, Ben Pol ambazo imezua tafrani kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Mngereza amewataka wasanii kufanya kazi nzuri ambazo zinaweza kuwaweka sehemu nzuri na siyo kutengeneza mazingira ambayo yanautia dosari muziki wao.

“Sisi kama BASATA tumeona hizo picha mtandaoni, siyo kitu kizuri, kwanza hakiendani na tamaduni zetu. Kwahiyo sisi tunamtafuta Ben Pol halafu tumsikilize, atueleze zile picha ilikuwaje mpaka zikasambaa mitandaoni. Tukiongea naye tunaweza kutoa kauli yoyote na kulaani matukio ya namna hiyo,”

Aliongeza,” Pia naungana na wasanii waliolaani kitendo hiko ambacho ni cha ajabu sana na baraza kwa mamlaka yake kama mzazi haiwezi kukaa kimya lazima tujue kama ana tatizo la akili au maadili limemkumba Ben Pol.”

Pia Mngereza amewaomba wasanii wa Tanzania kwa upande wa muziki wafanye muziki mzuri wasitegemee kiki.

Chanzo: Bongo5
 
Sasa kama hujui lugha ya picha utaelewa nn?kweli ubashite umewaingia polen! Ben pol yuko vizur sana hata huyo anajamb hapo Basata nae ni zero brain! Shit!!!
 
Sasa kama hujui lugha ya picha utaelewa nn?kweli ubashite umewaingia polen! Ben pol yuko vizur sana hata huyo anajamb hapo Basata nae ni zero brain! Shit!!!
Tuambie basi sisi tusiojua hiyo lugha yako ya picha....
 
Awa ni mazuzu kuna wadada karbia mia wanakaa uch instagram wamemuona benpol tu.. Au kiki
 
Tamaduni zetu ????

Hawajui kuwa kuvaa nguo sio tamaduni zetu ??

I never heard such an irony before !!!
 
hiyo ni art tu, ukiangalia kwa umakini utagundua kitu kama cha utekaji yani watekaji wanavyowafanyia watekwa nyara. mfano kuna picha ibamwonesha amefungwa kitambaa usoni harafu kifuani imechorwa tatu (3)....moja kwa moja ujumbe unaenda kwa wale wasanii wetu waliotekwa majuma kadhaa yaliyopita
 
Nyie basata bosi wenu amewakataza kufatilia ya mtandaoni ni udaku... sasa mnamtafutaje mtu kwa udaku.. ???
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom