BASATA lawashukia wavaa nusu uchi wa bongo movies na wacheza shoo za bend!

valid statement

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
2,851
868
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limewaagiza viongozi wa mashirikisho ya sanaa hapa nchini kufuatilia kwa karibu matukio ya ukiukwaji wa maadili yanayoendelea katika sekta hiyo hivi sasa na kuchukua hatua kwa wanaobainika kufanya hivyo. Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, mbali na kuwakemea vikali wasanii wanaotumia majukwaa kwa kuidhalilisha sanaa, wao wenyewe na watazamaji, pia limeyataka mshirikisho kushirikiana na vyama vyao, kuwaita wale wote watakaohusika na uvunjwaji wa maadili ili kuwakanya katika hatua ya kwanza na kama wasipoacha tabia hizo, Baraza litawafungia kujishughulisha na kazi ya sanaa hapa nchini. “Shirikisho la Muziki tumeliagiza kuangalia tungo za wanamuziki zenye maneno yenye lugha isiyofaa, Shirikisho la Sanaa za Ufundi limeagizwa kuwachukulia hatua wasanii wachoraji na wachongaji wanaotengeneza sanaa zinazokiuka maadili. “Aidha Shirikisho la Sanaa za Maonyesho waliagizwa kufuatilia wasanii wote wanaocheza bila staha majukwaani. Na mwisho Shirikisho la Filamu tumeliagiza kuwaita, kuwaonya na kuwachukulia hatua wasanii wote katika fani hiyo wanaovaa nusu utupu bila kuzingatia uhusika katika kazi za sanaa,” alisema Ghonche. Aidha, alisema Baraza limewaagiza wamiliki wa kumbi zote za burudani, kuzingatia maadili pale ambapo sanaa zitakuwepo jukwaani na kwamba, hawatasita kuufungia ukumbi wowote utakaokiuka agizo hilo. “Pia tunaviomba vyombo vya usalama, kuhakiki muda wa vibali vya maonyesho na bila kuchelewa kuwachukulia hatua stahiki wasiozingatia muda wa maonyesho. Na tunawakumbusha wamiliki wa vyombo vya habari na wahariri, kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wasimamizi wa sanaa kwa kutokurusha wala kutangaza maonyesho ambayo kwa njia yoyote yanachangia mmomonyoko wa maadili ya taifa letu. “Kwa suala hili, Baraza linaziomba mamlaka zinazohusika na usimamizi wa uendeshaji wa vyombo vya habari nchini, kuingilia kati na kuvichukulia hatua vyombo vya habari ambavyo kila siku vimekuwa mstari wa mbele kueneza wimbi la mmomonyoko wa maadili hapa nchini na kushusha hadhi ya tasnia/sekta ya sanaa nchini,” alisema Ghonche. Hivi karibuni, kumekuwepo na malalamiko kuhusiana na tamasha moja linaloendelea hivi sasa hapa nchini, ambako wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie wamekuwa wakipanda jukwaani wakinengua huku sehemu kubwa za miili yao ikiwa utupu, huku BASATA ikiwa kimya. SOURCE: GAZETI TANZANIA DAIMA Hivi ukishakuwa supastaa wa kike hapa Tanzania ni lazima uwe unavaa nusu uchi kila wakati? Wakicheza izo filamu zao wanavaa vimini hata kama wanaigiza maisha ya kijijini, wakiwa kwenye intavyuu kwenye luninga, wanagonga vimini, wakiwa jukwaani kwenye disko/tamasha ndo kabisaa wanakufuru na vimini vyao. Hebu BASATA na waanze na wacheza shoo katika mabendi hawa wanaovaa boxa na kucheza jukwaani! Leo ni ijumaa tunajua kabisa watapanda nusu uchi kama kawaida yao, BASATA wawajibishe hizo kumbi za starehe tuone kuwa wako makini.
 
uroho tu huo acheni watu waonyeshe mambo. tanzania haina maadili, maisha magumu anzeni kwanza na vibosile wenu waliowaweka waache wizi kwanza.
 
Acheni kutuaribia burudani,kwani maadili ni kwenye sanaa tu? Mbona wanaotuibia rasilimali zetu hawafanywi chochote? BASATA Acha hizo watu tuendelee kujinea masaburi.
 
Nakubalianan naewe Valid Statement. Hawa dad zetu wamezidi kufanya vituko. Heko BASATA fuatilieni kwa karibu. isiwe maneno tu.
 
Utawajua watu wenye roho za uzinzi na uasherati kwa matendo yao, hata kama hujawakuta wakizini. Kushabikia wanawake kuvaa nusu uchi hadharani kwa kisingizio chochote ni ishara ya wazi kuwa huo ni uzinzi.
 
Wanastuka leo...waachen watu na uhuru wao nyie BASATA mmchelewa vya kutosha aisee
 
hakuna kitu hapo ni politik tu hiyo vimin vitaendelea kuvaliwa kama kawa kwakuwa kwa sasa hakuna mkono wenye kuamua au kuagiza jambo litekelezwe likafanyika kama inavyotakiwa
 
Utawajua watu wenye roho za uzinzi na uasherati kwa matendo yao, hata kama hujawakuta wakizini. Kushabikia wanawake kuvaa nusu uchi hadharani kwa kisingizio chochote ni ishara ya wazi kuwa huo ni uzinzi.

Dont judge a book by its cover. Uzinzi uko akilini na sio kwenye mavazi. Kama mtu ni mzinzi hata akivaa HEMA bado ataendelea na mambo yake. Na kwa upande wa mwanaume, kama naye ni mzinzi hakuna aina ya vazi litakalobadilisha tabia yake. Uwanja wa fisi wako wamama wamevaa nguo ndefu na wengine na hijabu lakini wapo kazini mchana kweupe! Afghanistan wamama are wearing 'tents,- literally! lakini bado cases za rape zipo, na hata ukahaba upo!

Lakini ukiangalia statement ya BASATA utaona wanaongelea upande mmoja - wanawake. Kama ni uzinzi hao wanawake wanafanya na nani? It takes two to tangle.

Pili, hakuna mtu analazimishwa kuangalia wavaa vimini. Lakini kama unatoka nyumbani kwako kwenda kwenye ukumbi wa wavaa vimini - tena unalipa kiingilio, kwanini BASATA wanaondoa sehemu ya huduma uliyolipia (vimini)? Kinawahusu nini BASATA hadi waamue watu wazima na hela zao wanaruhusiwa kuona au kutoona nini?

Tanzania tuna tatizo kubwa sana la unafiki. Watu ni mahodari wa kusimama mbele ya camera na kusema mambo ambayo kwanza hayahusu (a free nation/democracy?) lakini pia kujidai tunajali maadili. Utasikia wakubwa wanalia maadili akitoka hapo stop ya kwanza ni nyumba ndogo! Maadili?
 
wasisahau kuwashughulikia kina 'khanga moko laki si pesa' wanadhalilisha utu wa mwanamke
 
hakuna kitu hapo ni politik tu hiyo vimin vitaendelea kuvaliwa kama kawa kwakuwa kwa sasa hakuna mkono wenye kuamua au kuagiza jambo litekelezwe likafanyika kama inavyotakiwa

afu ni upuuzi pia maana ukataze bongo mavi sijui muvi then kwa miss tanzania ndo vazi rasmi
 
Hizo hadithi zilikuepo tokea zamani ni kama zile za Sungura na fisi maana haziishi utaskia leo sungura kaiba kwa fisi kesho kampiga mtoto wa kobe yaani ni mauza uza
 
Hao BASATA ni kama mbwa koko, hawana uwezo wa kuuma. Joulize, je hao wasanii wameanza kuwa uchi juzi kwenye Fiesta? Kwa nini wanaongea baada ya jamii nzima ya Watanzania kulalama? Je BASATA hawajui nini kinaendelea mpaka Taifa lilie?
BASATA INAHUSIKA NA HUU 'UKAHABA' UANAOFANYWA...
 
Dont judge a book by its cover. Uzinzi uko akilini na sio kwenye mavazi. Kama mtu ni mzinzi hata akivaa HEMA bado ataendelea na mambo yake. Na kwa upande wa mwanaume, kama naye ni mzinzi hakuna aina ya vazi litakalobadilisha tabia yake. Uwanja wa fisi wako wamama wamevaa nguo ndefu na wengine na hijabu lakini wapo kazini mchana kweupe! Afghanistan wamama are wearing 'tents,- literally! lakini bado cases za rape zipo, na hata ukahaba upo!

Lakini ukiangalia statement ya BASATA utaona wanaongelea upande mmoja - wanawake. Kama ni uzinzi hao wanawake wanafanya na nani? It takes two to tangle.

Pili, hakuna mtu analazimishwa kuangalia wavaa vimini. Lakini kama unatoka nyumbani kwako kwenda kwenye ukumbi wa wavaa vimini - tena unalipa kiingilio, kwanini BASATA wanaondoa sehemu ya huduma uliyolipia (vimini)? Kinawahusu nini BASATA hadi waamue watu wazima na hela zao wanaruhusiwa kuona au kutoona nini?

Tanzania tuna tatizo kubwa sana la unafiki. Watu ni mahodari wa kusimama mbele ya camera na kusema mambo ambayo kwanza hayahusu (a free nation/democracy?) lakini pia kujidai tunajali maadili. Utasikia wakubwa wanalia maadili akitoka hapo stop ya kwanza ni nyumba ndogo! Maadili?

i like your comment
 
  • Thanks
Reactions: FJM
nao mkuu wamezidi tangu walipoambiwa wazuri basi imekuwa tatizo,sasa wanatamani hat kwenda kanisani waende uchi,kwani kuwa superstar ni lzm uonyeshe nyeti zako?na hiyo concept wanayo sana basata ya kwamba superstar wa kike bila kuwa uchi bd hakijaeleweka sasa wanaloloma nini
 
uroho tu huo acheni watu waonyeshe mambo. tanzania haina maadili, maisha magumu anzeni kwanza na vibosile wenu waliowaweka waache wizi kwanza.

Si ndo hapo eti maadili kwani nchi hii ina maadili ya watu kuiba na kupokea rushwa? Kuvaa nguo fupi ni part of entertainment mizee yenyewe inayopiga makelele ni mafuska watupu wasituzingue
 
Back
Top Bottom