BASATA: Tuliufungia "WAPO" wa Ney wa Mitego kwa sababu za kipolisi

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.

FB_IMG_1490612178363.jpg

Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.

Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kama kazi yake ikibainika kuwa na kosa la jinai.

“Tulifanya mazungumzo na wenzetu jeshi la polisi waliokua wanamhoji msanii Nay wa Mitego na kuchunguza jinai katika wimbo wake wa Wapo,” Basata walitweet.

Aliongeza, “Baada ya ushauri kutoka kwa Waziri Mwakyembe na baadaye taarifa ya jeshi la polisi na mazungumzo na msanii Nay kituo cha kati cha polisi.

Tunaruhusu wimbo wa ‘Wapo’ wa msanii Nay kuchezwa katika vyombo vya habari.
Kama taarifa yetu ilivyoeleza, ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi,”

Rapa huyo aliachiwa jana jioni na jeshi la polisi kwa kauli ya Rais Magufuli baada ya kushikiliwa kwa siku mbili.

Chanzo: bongo5
 
Hivi hii nayo ipo kwenye sheria na kanuni za uendeshaji wa BASATA. Inavyoonekana huyu Muingereza bada hajafikishwa mahakamani na kulipa fidia. Sasa ni wakati wa Nikki Mbishi kumfikisha mahakamani. Ameuzuia wimbo wa Samahani JK. Vijana hebu isomeni vizuri sheria ya BASATA kisha ashikishwe adabu huyu jamaa. Anafanya kazi kimazoea wakati jamii imeshapevuka!!
http://www.basata.go.tz/downloads/Kanuni_za_Baraza_la_Sanaa_la_Taifa.pdf
 
Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.

View attachment 487823
Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.

Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kama kazi yake ikibainika kuwa na kosa la jinai.

“Tulifanya mazungumzo na wenzetu jeshi la polisi waliokua wanamhoji msanii Nay wa Mitego na kuchunguza jinai katika wimbo wake wa Wapo,” Basata walitweet.

Aliongeza, “Baada ya ushauri kutoka kwa Waziri Mwakyembe na baadaye taarifa ya jeshi la polisi na mazungumzo na msanii Nay kituo cha kati cha polisi.

Tunaruhusu wimbo wa ‘Wapo’ wa msanii Nay kuchezwa katika vyombo vya habari.
Kama taarifa yetu ilivyoeleza, ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi,”

Rapa huyo aliachiwa jana jioni na jeshi la polisi kwa kauli ya Rais Magufuli baada ya kushikiliwa kwa siku mbili.

Chanzo: bongo5

Nadhani ni wakati muafaka sasa BASATA kuanza kujitafakari hasa Utendaji wao kwani tokea niwafahamu kila kukicha tu nazidi kugundua kuongezeka Kiwango chao cha Upumbavu wa Kiutendaji. Wizara husika kama inaweza ifanye mabadiliko makubwa sana na ya Tija hapo BASATA. Halafu hata hii sababu walioitoa ni ya ' Kipuuzi ' mno na niwashauri tu kuwa siku nyingine hata kukaa Kimya kunasaidia angalau kuficha Upumbavu ulionao na kupunguza hasira ya hadhira. Personally ' nimewadharau ' sana BASATA.
 
Usahihi ni kwamba waliofungia wimbo wa Nay ni Basata na aliyeufungulia wimbo huohuo 6ni Rais.

Tuache blabla.

Nilitalajia huyo Muingereza atangaze kujiuzuru kupinga maamuzi ya Rais kuwaingilia kazi, tatizo njaa.

Ushauri kwa mamlaka husika hii Basata ni jipu ambalo sasa libataka kugeuka kuwa Tambaza, tumbuwa mara moja.
 
Hahahahahahaha, hii kweli awamu ya vituko. Yani wajitekenya halafu wanacheka wenyewe. Mwakyembe aliamua siku moja kusema bila ya cheti cha kuzaliwa hakuna ndoa, mtukufu akaamua kupinga. BASATA wamefungia nyimbo chaguo la mungu kasema fungua. Sasa ni dhahiri uhalali wa jambo lolote nchi hii ni kwa mujibu wa mkulu tu. Guilty until proven innocent by the president. Illegal until stated otherwise by the president. Long live TZ.
 
Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.

View attachment 487823
Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.

Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kama kazi yake ikibainika kuwa na kosa la jinai.

“Tulifanya mazungumzo na wenzetu jeshi la polisi waliokua wanamhoji msanii Nay wa Mitego na kuchunguza jinai katika wimbo wake wa Wapo,” Basata walitweet.

Aliongeza, “Baada ya ushauri kutoka kwa Waziri Mwakyembe na baadaye taarifa ya jeshi la polisi na mazungumzo na msanii Nay kituo cha kati cha polisi.

Tunaruhusu wimbo wa ‘Wapo’ wa msanii Nay kuchezwa katika vyombo vya habari.
Kama taarifa yetu ilivyoeleza, ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi,”

Rapa huyo aliachiwa jana jioni na jeshi la polisi kwa kauli ya Rais Magufuli baada ya kushikiliwa kwa siku mbili.

Chanzo: bongo5
Basata ni wababaishaji tu, kama wimbo hauna maadili hauna maadili hata kama polisi au mtu mwingine wakisema una maadili, na kama una maadili una maadili tu hata kama polisi au mtu mwingine akisema una maadili. Hii ina maana kwamba BASATA ni genge la wanasiasa fulani wanaotumia mihemuko yao wasio na weredi wowote. Wanasikilizia nani anasema nini kuhusu sanaa fulani na sio kama wanavyoona wao.
 
Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.

View attachment 487823
Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.

Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kama kazi yake ikibainika kuwa na kosa la jinai.

“Tulifanya mazungumzo na wenzetu jeshi la polisi waliokua wanamhoji msanii Nay wa Mitego na kuchunguza jinai katika wimbo wake wa Wapo,” Basata walitweet.

Aliongeza, “Baada ya ushauri kutoka kwa Waziri Mwakyembe na baadaye taarifa ya jeshi la polisi na mazungumzo na msanii Nay kituo cha kati cha polisi.

Tunaruhusu wimbo wa ‘Wapo’ wa msanii Nay kuchezwa katika vyombo vya habari.
Kama taarifa yetu ilivyoeleza, ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi,”

Rapa huyo aliachiwa jana jioni na jeshi la polisi kwa kauli ya Rais Magufuli baada ya kushikiliwa kwa siku mbili.

Chanzo: bongo5
Hii ndio tabu ya kila idara ya serikali kufanya maamuzi kivyake, laiti BASATA ingelikua inashirikiana moja kwa moja na wizara ya Habari kabla ya kuja kulopoka kwa wananchi haya mambo ya haibu yasingetokea na kuwahaibisha kiasi hiki, hii style ya ONE MAN SHOW itawaumbua wengi sana
 
Sijui ni lini teknolojia itafikia pale ambapo madaktari wataweza kufanya operation ya kuhamisha ubongo.
Maana pale mwenye IQ ya 90 akifa basi wachukue ubongo wake na kuuweka kwe maidiot yenye IQ ya 1.5 mpaka 2!
 
Back
Top Bottom