BASATA na Vibali: Uongozi wa Ada Kwanza, Huduma Baadaye

BASATA na Vibali: Uongozi wa Ada Kwanza, Huduma Baadaye

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Kwa hakika, Tanzania tunaendeshwa na aina mpya ya uongozi—uongozi wa “ada kwanza, fikiria baadaye.” Tanzania tuna viongozi vichwa maji kupita maelezo. Barua ya BASATA inayotaka MC wa sherehe na MaDJ wote kujisajili na kuwa na kibali hai ifikapo Januari 31, 2026 imepokelewa kwa mshangao mkubwa na maswali makubwa pia.
1767081372241.jpg

Kimsingi, wazo la kusajili na kutambua wadau wa sanaa si baya. Lakini tatizo haliko kwenye kusajili; liko kwenye kukamua pesa.

Ukweli mchungu ni huu: kujisajili si bure, na kibali hakitolewi kwa baraka za maneno pekee. Wizara ya Utamaduni inaonekana kukosa ubunifu wa kutafuta vyanzo mbadala vya mapato, wao wakaamua njia rahisi—kuwakamua wale wanaohakikisha sherehe zinaacha kumbukumbu. MC na DJ wamegeuzwa ATM za serikali, kwamba mwaka unaanza, muswada unaanza: “leta hela.”
images - 2025-12-30T111331.727.jpeg

Kaka Godfrey Rugarabamu (MC Garab), MC Cheni na wenzao najua mmepata taarifa hii na nyie mnaweza kulipa hizi ada ila hao MC waliopo Mbinga huko, MC wanaosimamia Sherehe yenye bajeti isiyozidi Milioni? Ujumbe ni mmoja: umaarufu haukupi msamaha. Hata kama uliimba, ulipiga debe, au uliunga mkono kampeni za CCM, bado unatakiwa ujisajili, ulipe, na uwe na kibali “hai.” Sanaa haina kumbukumbu; ada haina huruma.
12751533_164968127221419_1061224001_n_002.jpg

Kuna msemo mmoja wa waswahili: "Simba akimaliza kula watoto wa chui huanza kula watoto wake".
images - 2025-12-30T111457.448.jpeg

Kinachoumiza zaidi ni mwelekeo, yaani badala ya uwepo wa sera shirikishi zinazoinua sekta—mafunzo, mikopo nafuu, bima ya wasanii, mifumo ya haki za kazi—tunapata barua, muhuri na malipo ambayo hazina faida zozote. Ni rahisi kudhibiti kuliko kukuza. Ndiyo maana watu wanauliza kwa kejeli: je, BASATA ipo kwa ajili ya sanaa au kwa ajili ya vibali?
images - 2025-12-30T111540.287.jpeg

Katibu Mtendaji wa BASATA, Edward Buganga, anakosolewa vikali kwa kuendeleza mtindo unaodaiwa hata kuzidi ule wa mtangulizi wake, Dkt. Mapana. Tangu 1984, ni vigumu kuonyesha hatua ambazo BASATA imepata uungwaji mkono wa wananchi kwa zaidi ya asilimia 70. Labda kwa sababu faida zake huonekana zaidi kwenye makaratasi kuliko kwenye maisha ya wasanii.
images - 2025-12-30T111829.423.jpeg

Mwisho wa siku, hoja si kupinga usajili—ni kupinga ulafi wa sera. Serikali ikiamua kusikiliza, ianze kwa kuuliza: je, ada hizi zinawajenga au zinawabana? Kama jibu ni la pili, basi tumejifunza kitu kimoja—kwamba uongozi unaopenda vibali kuliko vipaji huua sanaa taratibu.
 
Back
Top Bottom