Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema hivi karibuni kumetokea wimbi la Wasanii kuwa na tabia ya kupiga picha, kujirekodi au ku-rekodiwa video zenye maudhui kinyume na maadili ya Kitanzania kisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii kinyume na sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini.
“Baraza linatoa onyo kali kwa Wasanii wote kuacha tabia ya kujirekodi au ku-rekodiwa na kusambaza picha au video zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa na maadili ya Kitanzania”
“Baraza halitasita kuchukua hatua Kali ikiwemo kufutiwa leseni na kibali cha kujishughulisha na kazi ya sanaa kwa wote watakaoenda kinyume na tamko hili kwani itatafsiriwa kuwa ni uvunjaji wa sheria”