BASATA mnabeba lawama ya mmomonyoko wa maadili

Baraza la Sanaa la Taifa kwanini mmekuwa na kigugumizi kwenye muziki usio na maadili. Siku hizi nyimbo nyingi zina matusi, hazina maadili au zinachochea mmomonyoko wa maadili lkn cha kushangaza zinapigwa kwenye vituo vya redio na Televisheni.

Watoto wetu wanaimba nyimbo za ajabu kwa kuwa wanaziona zinapigwa. Nguvu inayotumika kushughulikia nyimbo zenye maudhui ya kisiasa itumike pia kushughulikia nyimbo zinazosifia ngono, pombe na mihadarati.

Mi ni mzazi na nikiangalia muziki wetu naogopa sana kizazi kijacho nchi hii kitakuwa cha aina gani!
Sihitaji kutaja nyimbo maana zipo nyingi sana, tafadhali BASATA okoeni maadili yetu kwa kuhakikisha kila wimbo kabla msanii hajautoa uwe umepita kwenu na umekuwa censored.

Kama hii kitu inafanyika sasa hv basi BASATA mjitathmini maana nyimbo nyingi zinatoka hazina maadili bado. Ni ngumu kuzuia wimbo kwa kutaka vituo vya redio na TV visiupige maana digital platforms na devices zipo nyingi, lkn mkiweka kanuni ya kutaka kila msanii ku submit wimbo wake kabla kusikika mtaani basi tunaweza kudhibiti nyimbo zisizo na maadili maana wimbo ukisikika popote na haujapita kwenu basi msaanii akamatwe.

Hatuwezi kuacha vijana wachache watuharibie vizazi vyetu kwa kisingizio cha sanaa!

Najua kuna vijana watapingana na mimi lkn ukiwa mzazi unayewaza future ya watoto wako mtaona hoja yangu.
Una hoja nzuri. Kwangu mimi, kulingana na nyakati za sasa (internet na utandawazi), tatizo kubwa kabisa lipo kwenye usikilizaji na siyo nyimbo zenyewe. Ni kama ilivyo pornography. Ponography ipo lakini juhudi zinafanywa kutoihusisha na watoto. Tanzania failuire yetu kubwa iko kwenye mazingira yanayochezwa na kusikilizwa hizi nyimbo. Inatakiwa zisipigwe sehemu za public kama kwenye daladala (infact serikali inatakiwa ipige marufuku muziki wa aina yoyote kwenye public transport) au mikusanyiko yenye watoto. Ukiwa eg kwenye jiji la Dar, masikio yako muda wote yanalamika kusikiliza nyimbo na vipindi vya redio vyenye maudhui mabovu. Mitaani, kwenye usafiri, hii haina afya kwa makuzi ya watoto.
 
Baraza la Sanaa la Taifa kwanini mmekuwa na kigugumizi kwenye muziki usio na maadili. Siku hizi nyimbo nyingi zina matusi, hazina maadili au zinachochea mmomonyoko wa maadili lkn cha kushangaza zinapigwa kwenye vituo vya redio na Televisheni.

Watoto wetu wanaimba nyimbo za ajabu kwa kuwa wanaziona zinapigwa. Nguvu inayotumika kushughulikia nyimbo zenye maudhui ya kisiasa itumike pia kushughulikia nyimbo zinazosifia ngono, pombe na mihadarati.

Mi ni mzazi na nikiangalia muziki wetu naogopa sana kizazi kijacho nchi hii kitakuwa cha aina gani!
Sihitaji kutaja nyimbo maana zipo nyingi sana, tafadhali BASATA okoeni maadili yetu kwa kuhakikisha kila wimbo kabla msanii hajautoa uwe umepita kwenu na umekuwa censored.

Kama hii kitu inafanyika sasa hv basi BASATA mjitathmini maana nyimbo nyingi zinatoka hazina maadili bado. Ni ngumu kuzuia wimbo kwa kutaka vituo vya redio na TV visiupige maana digital platforms na devices zipo nyingi, lkn mkiweka kanuni ya kutaka kila msanii ku submit wimbo wake kabla kusikika mtaani basi tunaweza kudhibiti nyimbo zisizo na maadili maana wimbo ukisikika popote na haujapita kwenu basi msaanii akamatwe.

Hatuwezi kuacha vijana wachache watuharibie vizazi vyetu kwa kisingizio cha sanaa!

Najua kuna vijana watapingana na mimi lkn ukiwa mzazi unayewaza future ya watoto wako mtaona hoja yangu.
Ukiwa msanii shabiki wa ccm hata ukanya viwanja vya basata utashangiliwa tu
 
Wapo tayari kufungia nyimbo zinazoponda Ufisadi wa Viongozi Lakini siyo zenye maudhui ya Matusi.Mbona Alli kiba nyimbo zake zina Maadili na watu wanazipenda
Walipoambiwa mnatuona NYANI mara moja wakakamata muimbaji na kumfunga baba yake jela.
Hapo tusi liko wapi?
 
RAIS tunaomba uvunje hiki chombo, ni kirusi kwa maadili ya watoto..Heri kubwa kuivu.ja BASATA kuliko hata kujenga barabara

Wale wenye watoto wanaelewa...
 
Najua kuna vijana watapingana na mimi lkn ukiwa mzazi unayewaza future ya watoto wako mtaona hoja yangu.
Chagua moja uimbe ngono, Pombe, bange, shisha, masuala ya kwa mpalange, kupromoti ushoga ushoga au uitukane Serekali uikosoe Serekali uimbe harakati zaidi

Mfano: Vitali Maembe alipoimba Sumu ya Teja alipewa airtime ya kutosha alipoanza kuipiga madongo Serekali akadakwa kaswekwa ndani varangati na nyimbo zake zikazuiwa zisipigwe popote hata redioni
 
RAIS tunaomba uvunje hiki chombo, ni kirusi kwa maadili ya watoto..Heri kubwa kuivu.ja BASATA kuliko hata kujenga barabara

Wale wenye watoto wanaelewa...
Nyimbo za bange, pombe na ngono ngono ndio zinazowalipa zaidi kuliko nyimbo zingine zozote ndio maana hawazizuii
 
Walipoambiwa mnatuona NYANI mara moja wakakamata muimbaji na kumfunga baba yake jela.
Hapo tusi liko wapi?
Kuikosoa na kuisema Serekali hata kwa mafumbo ni tusi kubwa, wewe kaimbeimbe bange bange huko sifia shisha, ngono ngono kushikana matako na kupakana mate nyoka anaingia pangoni imba hivyo utaitwa hata kwenye hafla za kitaifa uimbe wimbo huo mbele ya viongozi, sasa ole wako uimbe unaisema Serekali kwa lolote wewe hadi ukoo wako wote mtakua matatani
 
Back
Top Bottom