Baruti Dar: Mto Gide unaomeza watu, sasa kujenga Daraja la kudumu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
64eaccd3-97fa-4858-ad89-ae3e434f93bc.jpeg

Halmashauri imetoa milioni 200 na TARURA imetoa malioni 100 kwaajili ya mchango wa ujenzi wa daraja hilo la mto Gide ambalo watoto, Vijana, Wazee, huwa wanazima pindi wanapojaribu kuvuka. Inawalazimu kupita juu ya bomba (Picha)

Mkandarasi Nevablack Mwakalinga ambaye ndo anajenga Daraja hilo, amesema wanatarajia kukabidhi kazi ndani ya muda wa miezi mitatu au miezi miwili kama mvua haitanyesha kwa wingi.

“Daraja litakuwa na urefu wa mita kumi na moja na litakuwa la njia mbili ambalo lita ghalimu kiasi cha milioni 321 litakalo weza kupitisha magari ya uzito wa tani kumi” amesema Mwakalinga.

Sanjari na hayo Mwajuma Mnugila mwananchi wa eneo hilo la Baruti amesema mto huu umehama njia yake ya zamani, hivyo akataka waangalie njia yake ya zamani ili watakapojenga Usilete madhara.

“Wauangalie mto huu kabla ya kuanza ujenzi na waangalie njia yake ya zamani ili waweze kuurudisha ndipo waendelee na ujenzi wa daraja hilo”

Mwenyekiti wa mtaa wa baruti Mohammed Kilongo amesema Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kusikia kilio chake kwakuwa ujenzi wa daraja hilo ni moja kati ya ahadi yake katika kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2015.


Diwani wa kimara baruti Mh Pasco Manota wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo wakati akiwapa maelekezo kuhusu kuanza ujenzi wa daraja hilo amemuomba Mkandarasi kutumia Vibarua wa eneo husika katika Ujenzi wa wa Daraja hilo.

Daraja hili litaunganisha na kurudisha Mawasiliano kati ya Makoka na Baruti.
 
Back
Top Bottom