Barua yangu kwa Baba

Barua yangu kwa Baba

b191

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
742
Reaction score
1,032
S.L.P ........
NYUMBANI
...../..../.....

Baba Shikamo!...

Mimi ni mzima bukheri wa afya na hofu yangu ni wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu.

Dhumuni la barua yangu Baba ni kukutahadharisha juu ya mambo machache ambayo yanafanya siku hadi siku watu wazidi kukuchukia katika kijiji chetu ambacho wewe unakiongoza.

Mambo haya Baba ni;

1. VIWANDA.
Baba watu hawaoni kama kuna matumaini ya kujenga viwanda. Japo nasikia kuna kiwanda kimoja kimeanza kufanya kazi baada ya maagizo yako. Kiwanda hiki nasikia ni kile cha KUONGEZA BINADAMU KUZALIANA.

2. UONGO
Baba wanakijiji wanalalamika sana maana wanaona udanganyifu wako katika mambo mbalimbali. Naomba nikupe mfano,

a. Baba ulidanganya eti sisi kwenye kijiji chetu hatuhitaji msaada. Watu wamepiga hesabu,
BAJETI YA KIJIJI = Trilioni 29
MAKUSANYO YETU = Trilioni 19
UKITOA INABAKI = Trilio 11
Baba waambie wanakijiji Trilion 11 utazitoa wapi?

b. Hata zile njiwa mbili ulizonunua Baba nasikia bei yake ni kubwa sana ukilinganisha na ubora wake. Wanakijiji wanadai umewadanganya kwenye bei na hata takwimu zake pia.

c. Baba nasikia hata zile pesa walizochanga watu kwenda kwa wale waathirika hazijawafikia walengwa. Nasikia umetumia kwa mambo mengine.

d. Wanachuo wa kijiji chetu baba wanalalamika kuwa wengi wao hawajapata mikopo na wengine wamefaulu lakini wamekosa vyuo wakati wewe uliwaahidi mikopo na vyuo wote wenye sifa.

3. WASAIDIZI WABOVU
Baba nasikia umechagua wasaidizi wabovu ndiyo maana wanakijiji hawaoni kama wana msaada kwako. Japo nasikia wakati unachagua ulijitapa kuwa upo makini. Nasikia wakati unachagua uliangalia zaidi wale waliogombea vyeo katika chama chako na wakashindwa na hukuangalia sifa. Nasikia eti wengine,

a. Wanawadekisha walimu madarasa mbele ya wanafunzi

b. Wanawatishia walinzi wa kijiji

c. Wanaleta siasa hata kwenye mambo muhimu ya maendeleo

d. Wamefoji vyeti

e. Wamenunua majina ya watu na wanayatumia

f. Waliwahi kuiba mitihani na wakafutiwa matokeo.

4. UZUSHI
Baba nasikia siku hizi umekuwa unafuatilia sana maisha ya watu. Nasikia upo bize sana kujua mtu ana wake na watoto wangapi kuliko kujua matatizo ya wanakijiji.

NB: Baba wanakijiji nao wanamaswali mawili ya kizushi,

1. Eti ni kweli siku hizi Baba unatoka na umeshikwa masikio na yule Dada anayeshughulika na karo zetu. Eti ni kweli chochote anachokuambia lazima ufuate?

2. Eti kweli Baba huwa unaenda kwa Bibi kuosha nyota?

Baba natumaini utaisoma barua yangu.

Wako mwanao mpendwa.
 
Ngoja Nipite Zangu Kimya Maana Huyo Baba'ako Unaweza Mpa Ushauri Ukajikuta Umeishia Mahakamani!
 
S.L.P ........
NYUMBANI
...../..../.....

Baba Shikamo!...

Mimi ni mzima bukheri wa afya na hofu yangu ni wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu.

Dhumuni la barua yangu Baba ni kukutahadharisha juu ya mambo machache ambayo yanafanya siku hadi siku watu wazidi kukuchukia katika kijiji chetu ambacho wewe unakiongoza.

Mambo haya Baba ni;

1. VIWANDA.
Baba watu hawaoni kama kuna matumaini ya kujenga viwanda. Japo nasikia kuna kiwanda kimoja kimeanza kufanya kazi baada ya maagizo yako. Kiwanda hiki nasikia ni kile cha KUONGEZA BINADAMU KUZALIANA.

2. UONGO
Baba wanakijiji wanalalamika sana maana wanaona udanganyifu wako katika mambo mbalimbali. Naomba nikupe mfano,

a. Baba ulidanganya eti sisi kwenye kijiji chetu hatuhitaji msaada. Watu wamepiga hesabu,
BAJETI YA KIJIJI = Trilioni 29
MAKUSANYO YETU = Trilioni 19
UKITOA INABAKI = Trilio 11
Baba waambie wanakijiji Trilion 11 utazitoa wapi?

b. Hata zile njiwa mbili ulizonunua Baba nasikia bei yake ni kubwa sana ukilinganisha na ubora wake. Wanakijiji wanadai umewadanganya kwenye bei na hata takwimu zake pia.

c. Baba nasikia hata zile pesa walizochanga watu kwenda kwa wale waathirika hazijawafikia walengwa. Nasikia umetumia kwa mambo mengine.

d. Wanachuo wa kijiji chetu baba wanalalamika kuwa wengi wao hawajapata mikopo na wengine wamefaulu lakini wamekosa vyuo wakati wewe uliwaahidi mikopo na vyuo wote wenye sifa.

3. WASAIDIZI WABOVU
Baba nasikia umechagua wasaidizi wabovu ndiyo maana wanakijiji hawaoni kama wana msaada kwako. Japo nasikia wakati unachagua ulijitapa kuwa upo makini. Nasikia wakati unachagua uliangalia zaidi wale waliogombea vyeo katika chama chako na wakashindwa na hukuangalia sifa. Nasikia eti wengine,

a. Wanawadekisha walimu madarasa mbele ya wanafunzi

b. Wanawatishia walinzi wa kijiji

c. Wanaleta siasa hata kwenye mambo muhimu ya maendeleo

d. Wamefoji vyeti

e. Wamenunua majina ya watu na wanayatumia

f. Waliwahi kuiba mitihani na wakafutiwa matokeo.

4. UZUSHI
Baba nasikia siku hizi umekuwa unafuatilia sana maisha ya watu. Nasikia upo bize sana kujua mtu ana wake na watoto wangapi kuliko kujua matatizo ya wanakijiji.

NB: Baba wanakijiji nao wanamaswali mawili ya kizushi,

1. Eti ni kweli siku hizi Baba unatoka na umeshikwa masikio na yule Dada anayeshughulika na elimu yetu. Eti ni kweli chochote anachokuambia lazima ufuate?

2. Eti kweli Baba huwa unaenda kwa Bibi kuosha nyota?

Baba natumaini utaisoma barua yangu.

Wako mwanao mpendwa.
Duh..! Mi napita kimya..!
Maana sina milioni 7 za faini..!
Ndo kwanza naanza ujenzi![emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Mmmhh..! Hii barua nzito ujumbe tani 2000, ila baba bila shaka ana majibu siye watoto ujumbe mzito utatuvunja migongo.
 
Kwa kuwa barua yako kaka umenipa mm nimpelekee baba Mkubwa.....nimeifungua na kuisoma kuona haina uzito ...naichana chana na naenda kukuchongea kwa tabia ya utoro shuleni...........na kushinda vijiweni
 
Hii barua imelipiwa kodi..??
Maana stemp cja iona..?
[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]
Baba ata anza na maswali ayo..
 
Sema kuna hatari ukalipa mil 7 baada ya barua hii kumfikia baba yako [emoji126][emoji126][emoji126]
 
Kwa kuwa barua yako kaka umenipa mm nimpelekee baba Mkubwa.....nimeifungua na kuisoma kuona haina uzito ...naichana chana na naenda kukuchongea kwa tabia ya utoro shuleni...........na kushinda vijiweni
[emoji1] [emoji1] [emoji1] Kaka nahisi utanisaidia kuipeleka
 
Fanya kazi acha kuhangaika. Kila mtu nashida zake nyumbani. Acha kuzurula na kuangalia mambo ya kampeni remember slogan ya HAPA KAZI kula kwenu
 
Binadamu hata ungemtawaza Mara 100 au milele" bado atakwambia "Wakati unanitawaza mbona ulitumia mkono " kwann usingetumia dodoki " binadamu haturidhiki
 
Duh..! Mi napita kimya..!
Maana sina milioni 7 za faini..!
Ndo kwanza naanza ujenzi![emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Unajenga kwenye hii awamu kweli wewe kamanda Baba akikusikia Wenda akaja kuchukua mifuko ya cement ili umwambie pesa umeipata wapi Ding kavurugwa
 
Huyu baba sio kabisa
Ila tunamwambia subiri na yeye atakiona cha moto.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom