Barua ya wazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA juu ya Kampuni ya Vodacom Tanzania

Mimi nimekuwa mtumiaji wa siku nyingi wa huduma za vodacom kiukweli kampuni hii wamekuwa wahuni katika kutoa huduma zao kwa wateja, ningewashauri kabla hatujahama kutafuta watoa huduma wengine naomba badilikeni,of course nimshaenda kwa watoa huduma wengine na wako vizuri sana
 
Unanipa fidia ya MB 300 Wakati nimepoteza Zaid ya MB1000.Huu si wizi wa wazi? Walinisababishia usumbufu nikaunga bundle jingine nikijua like la awali limekwisha muda wake, sasa wataweza kurudisha bando langu?

Mimi nilijiunga mara nyinginyingi nikidhani tatizo ni mimi ndo mpaka baadae nikacheki na kuona kumbe bando zinaingia tu lakini internet hakuna, Sasa ukinipa MB 300 wakati nilikuwa nazo ziadi ya hizo maana yake umeniibia bando zangu nyingi na kunipa kidogo, Hii bado siyo fair
 
Voda ni kampuni ya matapeli. Wanauza airtime kwa wateja, kisha wanachukua tena hizo air time walizouza na kuzimiliki wao. Nina hakika matumizi yangu ya maneno matapeli ni sawa kabisa: yaani kujipatia kitu usichostahili au kwa njia za uanganyifu. Wanafanya hivyo almost kwa wateja wao wote kupitia hii kitu wanaita vifurushi.
 
Ndugu Mkurugenzi (TCRA)

Mnamo tarehe 23/02/2020

Kampuni ya Vodacom ilisitisha huduma ya Internet kuanzia alfajiri majira ya saa kumi na mbili na kurudisha usiku wa siku hiyo. Hakukutolewa taarifa kwa wananchi hadi saa 7 mchana.

Wakati hayo yanafanyika tayari kuna wananchi walikuwa tayari wameshajiunga vifurushi mbalimbali jana yake yaani tarehe 22/02/2020 ambavyo vingeisha muda wowote katika tarehe iliyofuata yaani tarehe hiyo ambayo mtandao haukuwepo.

Hata hivyo kutokana na kutokuwepo kwa mtandao wakati wananchi wangali na bando la data, kisha muda wa bando ulipoisha wananchi hawakunufaika chochote na bando lao kutokana na huduma ya internet kutopatikana na hivyo bando kuisha bure. Kutokana na hilo Kampuni ya Vodacom imewalipisha wananchi bila kuwapa huduma.

Ukiachilia mbali hilo, Siku nzima ambayo mtandao wa Vodacom ulikuwa haupatikani, Bado system za Voda ziliendelea kukubali kuingiza bando kwa njia ya kupiga *149*03# na namba zao nyingine za kuongeza salio la bando. Haya yalifanyika bila kuwataarifu wananchi na hivyo wananchi kuendelea kuweka vifurushi hivyo vilivyopotea bure.

Kibaya zaidi, Kampuni ya Vodacom haikutoa fidia (compensation) kwa wateja kutokana na kutowapa wananchi huduma hiyo.

Kutokana na hilo naiomba mamlaka ya TCRA ichukue hatua stahiki dhidi ya Kampuni hii ya Vodacom kwa kutwaa hela za vifurushi vya wananchi bure bila kuwapa huduma.

Kutokana na hiyo kampuni kutotupa huduma ya siku moja, bila shaka imetengeneza mabilioni ya bure kitu ambacho sio halali wala haki.

Ninaamini kuwa katika Serikali hii ya Mheshimiwa Rais Magufuli wananchi hatutoibiwa kirahisi rahisi na makumpuni ya aina hii na haki zetu zitalindwa.

Ni matumaini yangu barua hii ya wazi itafanyiwa kazi.

Wako katika ujenzi wa Taifa

Missile of the Nation (Kombora hatari la ulinzi wa Taifa)

Nakala kwa
Waziri wa Mawasiliano
Waziri Mkuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
TCRA nao ni sehemu
 
Hata mimi napiga hiyo menu ya kupata fidia sipati nakuna na vitu vingine au kuna menu nyingine zaidi ya hii *149*03*01#?? Harafu mimi sjapata sms yoyote kuhusu mtandao wao kuaumbua jana wakat ilinibidi niingie gharama ya kununua kifurushi kingine kweny mtandao mwingine ili ifanye mambo yangu, naomba wanipe fidia yangu skubali
Mbona mimi sijaona hiyo fidia?
Screenshot_20200224-140520_Phone.jpeg
 
Ndugu Mkurugenzi (TCRA)

Mnamo tarehe 23/02/2020

Kampuni ya Vodacom ilisitisha huduma ya Internet kuanzia alfajiri majira ya saa kumi na mbili na kurudisha usiku wa siku hiyo. Hakukutolewa taarifa kwa wananchi hadi saa 7 mchana.

Wakati hayo yanafanyika tayari kuna wananchi walikuwa tayari wameshajiunga vifurushi mbalimbali jana yake yaani tarehe 22/02/2020 ambavyo vingeisha muda wowote katika tarehe iliyofuata yaani tarehe hiyo ambayo mtandao haukuwepo.

Hata hivyo kutokana na kutokuwepo kwa mtandao wakati wananchi wangali na bando la data, kisha muda wa bando ulipoisha wananchi hawakunufaika chochote na bando lao kutokana na huduma ya internet kutopatikana na hivyo bando kuisha bure. Kutokana na hilo Kampuni ya Vodacom imewalipisha wananchi bila kuwapa huduma.

Ukiachilia mbali hilo, Siku nzima ambayo mtandao wa Vodacom ulikuwa haupatikani, Bado system za Voda ziliendelea kukubali kuingiza bando kwa njia ya kupiga *149*03# na namba zao nyingine za kuongeza salio la bando. Haya yalifanyika bila kuwataarifu wananchi na hivyo wananchi kuendelea kuweka vifurushi hivyo vilivyopotea bure.

Kibaya zaidi, Kampuni ya Vodacom haikutoa fidia (compensation) kwa wateja kutokana na kutowapa wananchi huduma hiyo.

Kutokana na hilo naiomba mamlaka ya TCRA ichukue hatua stahiki dhidi ya Kampuni hii ya Vodacom kwa kutwaa hela za vifurushi vya wananchi bure bila kuwapa huduma.

Kutokana na hiyo kampuni kutotupa huduma ya siku moja, bila shaka imetengeneza mabilioni ya bure kitu ambacho sio halali wala haki.

Ninaamini kuwa katika Serikali hii ya Mheshimiwa Rais Magufuli wananchi hatutoibiwa kirahisi rahisi na makumpuni ya aina hii na haki zetu zitalindwa.

Ni matumaini yangu barua hii ya wazi itafanyiwa kazi.

Wako katika ujenzi wa Taifa

Missile of the Nation (Kombora hatari la ulinzi wa Taifa)

Nakala kwa
Waziri wa Mawasiliano
Waziri Mkuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwangu mimi wameshanifidia bando la internet lililopotea siku ya jana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mfano Mimi mpaka jana wanasitisha huduma nilikuwa na bando ya entanet Mb 2098,na zilikuwa ziishe saa 4 usiku wa jana,eti leo wamenipa fudia ya mb 300,nimewapigia eti wakasema wataniludishia mb zangu ndani ya saa 24, kwa kweli huu ni uhuni uliopitiliza.
 
Back
Top Bottom