Barua ya wazi kwa vyama vyote vya kisiasa tanzania

Domenia

JF-Expert Member
May 26, 2009
462
22
CCM Ni chama cha muda mrefu, ni chama chenye uzoefu,..ni chama maarufu,Ni chama ambacho kina beba historia ya nchi yetu ya baada ya uhuru hadi sasa…watoto watakua na kusoma habari za CCM tangu kilivyokua chama safi kabisa hadi kilipo chafuka..watasoma jinsi walivyo ibiwa…umasikini,ujinga na magonjwa yalivyo nyanyasa mababu zao..na jinsi gani watu walivyo itumia CCM kutunyonya kwa muda mrefu hadi hapo chama kilipo achia madaraka…
Ukitazama kusini mwa Jangwa la Sahara, nafikiri ni moja ya chama cha siasa cha zamani sana ambacho bado kipo Madarakani…
Tangu kuanzishwa kwake sasa yapata miaka 34…hata hivyo hakuna tofauti kubwa sana za kima endeleo ambazo chama hichi kimefanikisha …. Lakini hata hivyo UMOJA bado imebaki kama ngao na utambulisho wa Watanzania..Hata kama itaonekana aikua juhudi za CCM kudumisha Umoja kabla na baada ya uhuru , Mwenye busara na fikra chanya atakubaliana na mimi…………… , asipo kubali basi!!! ..
CCM Bado wana uwezo wa kukemea , kujenga pamoja na kuziba Nyufa Zinazo anza kujitokeza ndani ya umoja wetu!!
Kumbuka TANU na ASP ndivyo vyama vilivyo unganisha fikra zao na matarajio na hatimaye Kuunganisha Nchi na ikazaliwa Tanzania…Vyama vya siasa vilivyo kuja kujitokeza baadaye vilisajiliwa Tanzania kwenye inchi iliyo tengenezwa na wa asisi, wazee wetu!!!!..Huku CCM ikiwa bado ime sheheni historia nzuri za waasisi wa nchi na fikra zao…
Tunapofikiria CCM kushindwa uongozi .-lazima tuweke wazi, na tutambue imeshindwa wapi? Wapiga kura waelimishwe…!!
Na Hata CCM yenyewe iwe wazi na kuelekeza wapi ime shindwa na wapi ilichelewa kutoa maamuzi…UFISADI (WIZI)- ULIANZA LINI?....kwa misingi hiyo ya uwazi itakua rahisi pale ambapo chama kingine kilicho zaliwa Tanzania kita chukua hatamu za uongozi…bila matatizo…-MZAZI UKISHINDWA MUACHIE MWANAO-
Tumesha ona Nchi nyingi za kiafrika hasa Vyama kongwe vinapo shindwa uchaguzi…Vurugu zina anza na hata ina fikia hatua ya kugawana madaraka..Zimbabwe imesha tokea, hapa Tanzania haifai kurudia ujinga kama huo…
Natoa angalizo kwa vyama vya siasa…tunapo elekea uchaguzi 2015 tuzingatie Yafuatayo..
1.Vita zidi ya ufisadi…kuweni makini na mafisadi…kamwe hawato penda Mchukue nchi -ni hatari kwao..!!nani HATARI KWENU…
Na hata kama watapenda ni kwa manufaa yao…na familia zao..na sio kwa Mtanzania kama ilivyokua kwa CCM..
Mfano-Kama wame weza kubadilisha taswila ya chama hadi kufikia chama kikaonekana ni chama cha mafisadi basi wapo wazi kabisa kuhakikisha vyama vingine havi ingii madarakani au wana vibadilisha na kua vyama vya Kigaidi…Wataanzisha udini na ukabila…!!!Na wamesha anza…
CCM anza mapema kurekebisha…kwani atakae anzisha vurugu ni wewe na sio mwingine..kumbuka vyama vyote ni vidogo wewe ndio mkubwa bado unawajibika….hata baada ya uchaguzi….
Kumbuka kama sio wizi CCM Ungesambaratika?
2.Tengenezeni katiba ya kisasa kabla ya 2015…Wananchi, wanasiasa na vyama vya kisiasa na hata marafiki zetu tupeane nafasi kuandika Katiba itakayo leta usawa na sio ujanja….Hakika tukiwahi hakutakua na tatizo…
3.Matatizo Yote ya wizi ufujaji wa mali za mya tambuliwe na sehemu kubwa kama sio yote yatatuliwe kabla ya uchaguzi…Sheria ifuate mkondo wake ….kwasababu WIZI wa mali ya Umma ndio itakayo zua malumbano makubwa baada ya Uchaguzi…- Ni wazi kabisa Serikari ya CCM imeshindwa kusimamia sheria…na Kuacha Rushwa ishike hatamu za uongozi wa mabaraza ya hukumu Tanzania,kwenye Inchi ambayo ili tengenezwa na TANU na ASP…-
4.Kumbuka Kuishinda CCM kwenye uchaguzi sio utatuzi wa matatizo yote yanayo wakabili Watanzania…
5.Matatizo yalio ikumba CCM yanaweza yakakikumba chama kingine..vyama vyote vishirikiane kupambana na wizi na ufujaji wa mali ya uma na kuwa letea maendeleo wananchi wake…

KAMA VYAMA VYOTE VYA SIASA VITAWEKA UTAIFA MBELE TANZANIA ITAFANIKIWA
 
Back
Top Bottom