Barua ya wazi kwa Serikali yangu: Misallocation of employment inasababisha upungufu wa ajira Tanzania

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Naomba nirejee kwenye mada moja kwa moja.

Kuna watumishi wanapangiwa vituo vya kazi na serikali alafu wanavikimbia na kuhamia private tena bila taarifa. Watu hao wanasababisha misallocation of employment, jambo ambalo linaongeza upungufu wa ajira inchini.

Kama watumishi hao wangebakia serikalini huko huko, hizo nafasi za private zilizo wazi zingeombwa na watu wengine ambao hawana ajira. Na hili lingepunguza tatizo la ajira inchini. Na tatizo moja ni kwamba wanakimbia vituo bila kutoa taarifa kwenye wizara (TAMISEMI).

Serikali yangu naomba mfanye check up juu ya hilo na ikiwezekana mtengeneze mfumo wa kutambua watu wanao kimbia vituo vya kazi na kuhamia private ili nafasi hizo zinapo kuwa wazi zijazwe kwa wakati na watu ambao hawana ajira. Itakua vizuri mkiwa na mfumo wa mtandao (online) na mfumo huo uendeshwe na wizara moja kwa moja. Wapo watumishi wengine huweza hata kutoa rushwa kwa wakurugenzi ili kukubaliwa kuondoka kituoni.

Pia tengenezeni mfumo wa utambuzi kwa kutumia namba ya kitambulisho cha NIDA ambayo itumiwe na kampuni na taasisi zote ili kuweza ku track taarifa za mtu yeyote anayeomba ajira katika kampuni au taasisi yeyote Tanzania ili kufahamu kama huyo mtu ameajiriwa au hajaajiriwa.

Na kama ameajiriwa asiruhusiwe kuomba kazi hiyo bila kuwa na utambulisho maalum kutoka wizara ya TAMISEMI kama mtu huyo ni mwaajiriwa wa serikali au private. Kampuni zote zinafanya kazi katika mazingira yetu hivyo lazima tuzifanyie monitoring ya kutosha sio kuchukua kodi tu hata kwenye swala la ajira pia.

Nilichogundua ni kwamba communication ni ndogo sana kati ya serikali na taasisi binafsi katika swala la ajira. Taasisi binafsi zinajiendesha zenyewe katika kuajiri wala serikali haizifuatilii na ndio sababu utakuta taasisi nyingi za binafsi zinaajiri watu wasio na qualification zinazo hitajika kwenye ajira fulani.

Mfano ukienda kwenye shule za private utakutana na walimu wanafundisha ila hawajasomea ualimu wengine ni form six lever, utakuta wengine wamesomea nursing, medicine, sociology, computer science, n.k.

Swala hilo linasababisha ukosefu wa ajira kwa watu walio somea ualimu inchini. Na hiyo ndio nasema ni misallocation of employment.

Hapo naomba serikali kupitia wizara ya TAMISEMI kaeni na Taasisi binafsi fanyeni check up, toeni watu wasio na qualification, ajirini wenye qualification kisha tengenezeni mfumo wa utambuzi na na hakikisheni mnatengeneza mfumo mzuri wa mawasiliano na hizo taasisi binafsi.

Sina shaka na wazee wa loan loan board na TRA, na NSSF hawa jamaa wanamasiliano mazuri sana Taasisi binafsi. Wizara ya ajira na nyinyi hii ndio kazi yenu waulizeni TRA, Bodi ya mikopo na NSSF wanawasilianeje na hizi taasisi binafsi.

Nije kwenye upande wa taasisi binafsi zingine hapa kuna mabenki, microfinances, viwanda mbalimbali (hapa tuna viwanda vingi sana, maabara mbalimbali), n. k. Ha huko pia fanyeni check up, na pia tengenezeni mawasiliano mazuri. Kuna watu huko hawana qualification ya hizo kazi wanazofanya, na huku kazi zao zipo.

Sishauri sana utambulisho utengenezwe na taasisi zinazo ajiri bali utengenezwe na wizara ili kuhakikisha kwamba nafasi ya kazi ina be allocated mahali husika bila kukosea.

Kwa kifupi recruitment is still zig zag in our country, haieleweki taasisi za private hazifuatiliwi katika swala zima la kuajiri na ndio sababu hatuwezi kujua tuanzie wapi ili kutatua tatizo la ajira. We still recruit in old fashioned way in private sectors. Tafadhari serikali tunawaomba mwingilie kati, it's not bad the government to interven in job market so as to regulate the system.

Employment is also our resource so let manage and allocate it efficiently.

By ellyskywilly.
 
Umeyajua je hayo? Au hili ni kwa serikali ya UK? Si ulisema jwenu UK?

Hiiii bagosha!

Au yale yale ya Atlanta, Georgia; kumbe mtu yuko Ikungu lya Bashashi?
 
Serikali ya Awamu ya 5 imefeli kwenye nyanja karibu zote na kamwe kujaribu kuipamba ni kujivunjia heshima !!
 
Umeyajua je hayo? Au hili ni kwa serikali ya UK? Si ulisema jwenu UK?

Hiiii bagosha!

Au yale yale ya Atlanta, Georgia; kumbe mtu yuko Ikungu lya Bashashi?
nipo U.K ila habari za taifa langu nazifutilia kila siku
 
Acheni siasa kwenye mambo ya msingi, tatizo la ajira ni kubwa na halitasoviwa kwa siasa taka kama hizi.

Hivi unajua ni private employees wangapi wameachishwa/kuacha kazi tangu mwaka 2015?

Huko private kwenyewe hali ni mbaya sana.
Umeulewa uzi wangu vizuri mkuu, kile nilicholenga. Miss allocation of employment, hapo ndio nimesimamia.
 
nipo U.K ila habari za taifa langu nazifutilia kila siku

Au unamaanisha UK yaani Ukerewe mkuu?

Salimia Wakara wenzio wote huko. Mitano mingine tutapambana iwe awamu yenu. Labda nanyi mjenge ka airstrip.

Hawa wa chattle itabidi watuelewe kwa hilo.
 
Au unamaanisha UK yaani Ukerewe mkuu?

Salimia Wakara wenzio wote huko. Mitano mingine tutapambana iwe awamu yenu. Labda nanyi mjenge ka airstrip.

Hawa wa chattle itabidi watuelewe kwa hilo.
amini tu hivyo mkuu wala sidanganyi, nipo karibu na serikali yangu kwasababu nikitua tu hapo naanza kutumika moja kwa moja.
 
amini tu hivyo mkuu wala sidanganyi, nipo karibu na serikali yangu kwasababu nikitua tu hapo naanza kutumika moja kwa moja.

Ni jambo la aibu sana kwa nia chama wewe kujitanabaisha kuwa uko kwa mabeberu.

Nyinyi ndiyo mnaochelewesha mzee baba kuifanya Tanzania kuwa first world!

Wewe hujui sisi ni donor country? Wewe hujui kuwa hatuhitaji chochote cha Mabeberu hapa? Si dawa, chanjo, kwenda kwao, kukaa kwao, mitumba yao, nk?

Tumekwishaanza kukusanya mitumba yetu kuwapelekea nguo.

Kwanza wale ni maskini sana!
 
Au unamaanisha UK yaani Ukerewe mkuu?

Salimia Wakara wenzio wote huko. Mitano mingine tutapambana iwe awamu yenu. Labda nanyi mjenge ka airstrip.

Hawa wa chattle itabidi watuelewe kwa hilo.
sawa mkuu,
 
Pambana na hali yako. Umekaa nyumbani, badala ya kupambana uajiriwe! Unawaonea gere wenzako waliosomea sociology, sheria, walioishia form six, nk halafu wanapiga mpunga mrefu tu huko kwenye sekta binafsi!

Unadhani hao watu wa private wanaangalia hayo mavyeti ya kudesa chuo kikuu? Wenyewe wanaangalia output!!! Uache pia tabia yako ya kutuonea gere sisi tulio ajiriwa! Maana haitasaidia chochote, zaidi tu utapatwa na magonjwa ya moyo.
 
Pambana na hali yako. Umekaa nyumbani, badala ya kupambana uajiriwe! Unawaonea gere wenzako waliosomea sociology, sheria, walioishia form six, nk halafu wanapiga mpunga mrefu tu huko kwenye sekta binafsi!

Unadhani hao watu wa private wanaangalia hayo mavyeti ya kudesa chuo kikuu? Wenyewe wanaangalia output!!! Uache pia tabia yako ya kutuonea gere sisi tulio ajiriwa! Maana haitasaidia chochote, zaidi tu utapatwa na magonjwa ya moyo.
mkuu mimi sihitaji kuajiriwa bali nataka kutafutia ajira wengine, ndio maana nimezungumzia miss allocation of employment. Na sijawahi kuwaza kuajiriwa, ninaamini kama binadamu wenye akili kama zangu wanaweza kuajiri au kutafutia ajira wengine basi hata mimi naweza kuajiri na kutafutia ajira wengine. Kwamba kwa kifupi naweza kutengeneza ajira kwaajili ya wengine.
 
Back
Top Bottom